MFALME MZEE YUSUPH KUPEWA MAUWA YAKE DISEMBA 8
MSANII wa muziki wa taarabu nchini Mzee Yusuph ‘Mfalme wa Taarabu’ anatarajia kupewa mauwa yake kwa kuupigania muziki huo katika tamasha la muziki huo linalotarajia kufanyika Disemba 8, 2024 jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na habarileo Mzee Yusuph alisema kuwa watu wengi wanapenda kuwapa watu mauwa yao wakiwa wametangulia mbele za haki kwake ni tofauti.
“Napewa mauwa yangu na ninayapokea kwa sababu najuwa kuwa nastaili maua haya, nimefanya muziki wa taabu kwa muda Mwingi lakini hakuna mwanaume yupo muda mrefu kwenye huu muziki zaidi yangu.
"Mashabiki zangu na watu mbalimbali wanaopenda kazi zangu niwaombe na niwakaribishe katika tamasha maalumu la kunipa mauwa yangu kwa Mchango wangu kwenye tasnia ya muziki wa taarabu.
“Kuna muda muziki wa taarabu ulikuwa kama umelala hakuna anayeweza kuuamsha kama Mzee Yusuph niwaambie tu watu wajitokeze kwa wingi Disemba 8 waone muziki unavyozaliwa upya huku nikipokea mauwa yangu.”alisema Mfalme Mzee Yusuph
Aidha ameongeza kuwa atahakikisha muziki wa amapiano unaingia upya katika Tasnia ya Taarabu kwa kuleta mabadiliko makubwa kwenye muziki huo pendwa.
"Lengo likiwa ni kuwavuta mashabiki wote kama nilivyofanya kazi na wasanii wa bongo fleva na wakati huu wajiandae kuona muziki wa amapino katika Taarabu, hili tamasha harijawai kutokea najipa mauwa na wanaotaka kunipa karibuni Disemba 8 nitayapokea."alisema Mfalme Mzee Yusuph

Comments
Post a Comment