VETA YAJA NA KONA YA WATOTO SABASABA
Chuo Cha Mafunzo na Ufundi Stadi VETA) Songea imekuja na kona ya watoto katika
maonesho ya 49 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kwa lengo la kuibua vipaji
na kuwafundisha misingi ya maisha. Faulata Mutalemwa ambaye ni Mwalimu kutoa
VETA Songea amesema kupitia kona hiyo ya watoto wanajifunza vitu mbalimbali
ikiwemo stadi za mikono mbalimbali na kuondoka nazo.
Akitaja stadi hizo amesema ni pamoja na ushonaji, urembo pamoja na masuala ya
umeme. "Kupitia kona ya watoto mtoto anaweza kujifunza vitu mbalimbali vya namna
ya kuchana nywele, kutunza ngozi yake, namna ya kushona nguo zake pamoja na
kudhiifadhi"amesema Mutalemwa.
Kwa upande wa eneo la umeme amesema mtoto anajifunza namna ya gani taa inawaka
huku akifuata hatua nyepesi. Aidha ametoa wito kwa wazazi, walezj kutembelea
katika Banda la Veta ili watoto wao waweze kujifunza vitu mbalimbali vinavyohusu
maisha.



Comments
Post a Comment