Posts

Showing posts from March, 2024

WATU 1404 WAATHIRIKA NA MAFURIKO

Image
JUMLA ya watu 1404 wameathirika na mafuriko ya mvua zinazoendelea kunyesha katika Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro na nyumba 351 zimeingia maji pamoja na vyoo 368 vimebomoka. Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka, kuwa kaya zilizoathirika ni 368 na nyumba 17 zimebomoka. Alisema kitongoji cha Kampala kaya 161 na watu 624 wameathirika, Kitongoji cha Madizi kaya 137 zimeathirika na watu 531, Kitongoji cha Estate kaya zilizoathirika 57 na watu 196 wameathirika. Kitongoji kingine ni cha Lugunga kata nane na watu 32 wameathirika, Kitongoji cha PWD kaya tano na watu 20 wameathirika. Shaka alisema nyumba 17 zilizobomoko tano zinatoka kitongoji cha Kampala, nyumba nane kitongoji cha Estate na nyumba nne kitongoji cha Madizini. Alisema jumla ya vyoo 368 vimeathirika kutokana na mafuriko, hivyo kufanya maji kuwa machafu baada ya vyoo hivyo kutapishwa na mafuriko baada ya kubomoka. Aidha, Shaka alisema jumla ya visima 30 vya maji vinavyotumika vimeathirika na mafuriko hayo ...

DIAMOND NA HARMONIZE USO KWA USO

Image
Wasanii wa Bongo fleva Naseeb Abdul 'Diamond na Rajab Abdul 'Harmonize' wamekutana na kupeana mikono walipokutana kwenye Iftar Ikulu jijini Dar es Salaam Harmonize alisikika akimwambia Diamond Platnumz' kuwa nitakupigia simu kesho naomba pokea basi. Wawili hao walikuwa pamoja mtu na boss wake pindi Harmonize alipokuwa WCB miaka tisa iliyopita tangu aondeke ni miaka minne sasa wawili hao hawakuwai kuongea wala kuonana na sasa wamekutana na akuzungumza rasmi.