WANAMITINDO WAPATIWA ELIMU YA FEDHA CRDB BENKI KUINUA BIASHARA NA KUTOA AJIRA
Washonaji Wapatiwa Semina ya Elimu ya Fedha Kuinua Biashara na Kutoa Ajira Washonaji na wabunifu wa mitindo nchini wamepatiwa semina ya elimu ya fedha yenye lengo la kuwawezesha kukuza biashara zao, kutoa ajira kwa vijana na kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa. Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Jafari Hassanali, amesema tasnia ya mitindo ipo katika safari ya kutoka kwenye kipaji cha kawaida na kuelekea kuwa biashara endelevu yenye mchango mkubwa katika uchumi wa taifa. Amesema ubunifu ulio sambamba na maarifa ya biashara na usimamizi wa fedha ni msingi muhimu wa kushikilia na kuimarisha uchumi wa nchi, akibainisha kuwa sekta ya ubunifu ni miongoni mwa sekta zinazokua kwa kasi na zenye uwezo mkubwa wa kutoa ajira kwa vijana. Akizungumza katika Jukwaa la Tanzania Fashion Forum, Hassanali amewataka wabunifu kutumia mikopo kama nyenzo ya uwezeshaji wa biashara badala ya kuifanya kuwa mazoea. “Unapokopa lazima uelewe kuwa mkopo ...