SERIKALI KULETA MAPINDUZI KATIKA TASNIA YA HABARI
SERIKALI inakusudia kushirikiana na sekta binafsi kufanya mabadiliko na maboresho makubwa kwenye sekta ya habari kwa kutunga na kuhuisha sera, sheria, miongozo inayosimamia sekta za habari, mawasiliano na teknolojia ya habari. Serikali pia inakusudia kuimarisha huduma za mawasiliano ya simu na posta kote nchini kwa kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya kukuza na kuimarisha biashara mtandao nchini, kuimarisha miundombinu itakayowezesha utekelezwaji wa uchumi wa kidigitali, kuimarisha ulinzi na usalama wa anga. Hayo yamesemwa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Thobias Makoba ambaye alimwakilisha Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye leo Juni 27,2024 kwenye kongamano la uhuru wa kujieleza na sheria za vyombo vya habari lililoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC). Msemaji huyo wa Serikali amesema mwaka 2024/2025 Wizara imepanga kukamilisha uhuishwaji wa sera mbalimbali ikiwamo sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003 na kutunga Sera mpya ya Taifa ya...