RAY GABO NA DUMA SIO LEVEL ZANGU
Msanii wa Filamu nchini Vincent Kigosi 'Ray' anashangazwa na watu kulinganishwa na Gabo na Duma ameomba kutoshindanishwa na msanii yoyote nchini.
Amesema kuwa ameshafanya makubwa katika Tasnia hii na sasa yeye yupo kimataifa.
Ray amesema hayo Jijini Dar es Salaam na kudai kuwa wasanii wanaofanya vizuri asilimia 90 amewatoa yeye hivyo Mwalimu hawezi kulinganishwa na mwanafunzi wake.
"Watu wanashindwa kutofautisha kwa sasa si shabiki sio nani naomba sitaki kushindanishwa na msanii yoyote yule nafasi yangu kwa sasa ni wasanii wa Kimataifa.
"Nishachukua tuzo nchini Kenya, Uganda hadi Nigeria halafu Bado unataka kunilinganisha na wasanii wa juzi niliowaleta mwenyewe kwenye tasnia hapana kwa kweli."
"Asilimia 90 ya wasanii unaowajua wewe hapa nchini Tanzania nimewatambulisha na kuwaleta kwenye tasnia ya filamu sasa unawezaje kumfananisha Mwalimu na mwanafunzi hao kina Gabo washindanisheni na kina Duma ila sio Ray sio level zangu kabisa."amesema Ray


Comments
Post a Comment