RAIS SAMIA MGENI RASMI TWENZETU SONGWE
Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatajarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye tamasha la kimataifa la utamaduni litakalofanyika Mkoani Ruvuma .
Tamasha hilo ambalo litafanyika kuanzia tarehe 20 mpaka 27 Mkoani humo linatarajia kufungua fursa mbalimbali, katika nyanja ya kiutamaduni, kiutalii, pamoja na upatikanaji wa mapato.
Hayo ameyasema Naibu wa waziri wa utamaduni sanaa na michezo Hamis Mwinjuma leo Juni 20,2024 Katika ufunguzi wa tamasha hilo Jijini Dar es salaam
Mwinjuma amesema tamasha hilo litakuwa la kihistoria kwani wageni wengi wanatarajiwa kutoka nje na ndani ya nchi na itawakutanisha makabila zaidi ya 120 nchi nzima .
Awali akiongea muandaaji wa Tamasha hilo Mwesigwa Selestine kutoka Drum- Beats amesema tamasha hilo limekuwepo kwa takribani mwaka wa tatu na lina lengo la kutunza pamoja na kuhifadhi utamaduni pamoja na asili ya mtanzania .
Tamasha hilo lenye kauli mbiu ya twenzetu Ruvuma twenzetu Songwe.

Comments
Post a Comment