Posts

Showing posts from April, 2025

MSANII CHEMICAL SASA NI DKT LUBAO

Image
Msanii Chemical apata shahada ya udaktari: “Nimeamka Kama Dkt. Lubao!” Kwa muda mrefu, wasanii wamekuwa wakitazamwa kama watu waliopungukiwa na elimu ya juu. Lakini msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Claudia Lubao maarufu kama Chemical, amevunja dhana hiyo kwa kishindo baada ya kufanikiwa kutunukiwa shahada ya uzamivu (PhD) kutoka Chuo Kikuu cha St Andrews, Uingereza. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Dr. Lubao alitangaza habari hiyo njema kwa mashabiki wake akieleza kuwa amefanikisha mtihani wa mwisho wa Viva, hatua ya mwisho kabla ya kutunukiwa shahada hiyo ya heshima. "Niliwahi kuwa na ndoto… na leo, nimeamka kama Dkt. Lubao! Najihisi kuheshimiwa sana na nina shukrani za dhati kwa msaada mkubwa nilioupata kutoka kwa wasimamizi wangu, idara nilizoshirikiana nazo, marafiki, muziki wangu, na familia yangu ya mtandaoni," aliandika. St Andrews ni miongoni mwa vyuo vikongwe na vinavyoheshimika zaidi barani Ulaya, na mafanikio ya Dr. Lubao yanamweka katika kundi adimu...

BOLT YAZINDUA HUDUMA SCHEDULED RIDES

Image
Bolt Yazindua Huduma ya "Scheduled Rides" na Ufuatiliaji wa Safari za Ndege kwa Ufanisi Zaidi Dar es Salaam, Tanzania – 30 Aprili 2025 Katika juhudi za kuendelea kuboresha huduma zake za usafiri nchini Tanzania, kampuni ya Bolt imezindua dirisha jipya la kupanga safari mapema (Scheduled Rides), sambamba na huduma ya kisasa ya kufuatilia safari za ndege (Flight Tracking), hatua inayolenga kuongeza ufanisi na urahisi kwa watumiaji wake. Kuanzia jana, wateja wanaotumia programu ya Bolt sasa wanaweza kupanga safari zao za usafiri mapema kwa urahisi kupitia kitufe cha “Schedule” kwenye app. Hii ni sehemu ya maboresho ya kidijitali yanayolenga kuongeza ufanisi na kupunguza usumbufu kwa wasafiri, hasa wale wanaoelekea au kutoka uwanja wa ndege. Akizungumza kuhusu huduma hiyo mpya, Dimmy Kanyankole, Meneja Mkuu wa Bolt Tanzania na Kenya, alisema: "Teknolojia inabadilika kwa kasi na Bolt inaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuleta ubunifu unaotatua changamoto hal...

AIRTEL YAZINDUA HUDUMA KUPAMBANA NA MATAPELI TANZANIA

Image
Airtel Yazindua Huduma Kupambana na Utapeli Tanzania Dar es Salaam, Airtel Tanzania leo imezindua huduma mpya inayotumia teknolojia ya Akili Mnemba, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha mapambano dhidi ya utapeli wa mitandaoni nchini. Huduma hiyo, inayojulikana kama Airtel Spam Alert - Kataa Matapeli, inalenga kuwatahadharisha wateja kuhusu jumbe za kitapeli kupitia simu janja na simu za kawaida bila hitaji la kupakua programu yoyote. Huduma hiyo imeanzishwa kufuatia mafanikio yaliyopatikana nchini Nigeria na Uganda, ambapo Airtel imekuwa ikiboresha huduma zake za kulinda wateja dhidi ya ulaghai. Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Jerry Silaa, aliipongeza Airtel kwa hatua hiyo, "Huduma ya Airtel Spam Alert - Kataa Matapeli, inayotumia Akili Bandia kugundua ulaghai mtandaoni, inaendana na juhudi za serikali za kuhakikisha wananchi wanakuwa salama dhidi ya matapeli wa simu," amesema. Waziri Silaa ...

ENDELEENI KUOMBEA VIONGOZI NA TAIFA

Image
Waimbaji wa Nyimbo za Injili na Viongozi wa Dini Watakiwa Kuendelea Kuliombea Taifa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Emmanuel Nchimbi, amewataka waimbaji wa nyimbo za Injili pamoja na viongozi wa dini nchini kutokata tamaa katika kulitumikia Taifa kwa maombi, huku akisisitiza umuhimu wa kuwaombea viongozi wa nchi ili kuendelea kudumisha amani, furaha na mshikamano. Akizungumza katika tamasha la Mtoko wa Pasaka lililoandaliwa na mwimbaji wa Injili Christina Shusho kwa kushirikiana na Mama Ongea na Mwanao, Balozi Nchimbi alisema maombi ni silaha muhimu na yanapaswa kuwa endelevu. "Msichoke kuliombea Taifa, kuwaombea viongozi wetu ili tuendelee kuwa na nchi ya amani na furaha. Msiache pia kuwakumbusha wanasiasa, maana mara nyingine tunapokuwa kwenye vipaza sauti tunajisahau. Tukikaa pembeni tunajiuliza, 'Je, ni mimi niliyesema haya yote?'," alisema Nchimbi. Alisisitiza kuwa si vibaya kiongozi kukiri makosa pale anapoteleza kwa kauli, kwan...

STEVE, JEMBE NI JEMBE WAKABIDHI VITI VYA WALEMAVU

Image
Jembe ni Jembe na Steve Nyerere wakabidhi viti vya walemavu mtoko wa Pasaka Na Brighit Meneja wa msanii Harmonize, Sebastian Ndege maarufu kama Jembe ni Jembe, kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao, Steve Nyerere, wamekabidhi viti vya magurudumu kwa watu wenye ulemavu katika tamasha la Mtoko wa Pasaka lililofanyika jijini Dar es Salaam. Akizungumza wakati wa tukio hilo, Steve Nyerere amemshukuru Jembe ni Jembe kwa moyo wake wa huruma na kujitolea kwa jamii. "Nikushukuru ndugu yangu kwa kujitoa kwa dhati kuwasaidia watu wenye ulemavu. Kwa kuwapatia viti vya magurudumu, umeweza kugusa maisha ya Watanzania wenye uhitaji mkubwa. Umetoa faraja na matumaini kwao," alisema Nyerere kwa hisia. Aliendelea kwa kusema kuwa awali alikuwa mzito kiroho, lakini kupitia huduma na ibada zilizofanyika kwenye Mtoko wa Pasaka, amejiona mwepesi na mwenye furaha ndani ya ibada za kusifu na kuabudu. Kwa upande wake, Jembe ni Jembe alisema kuwa Mtok...

MONGELLA: WANAWAKE TUMUWEKE SAMIA MADARAKANI KULINDA BEIJING

Image
Na Bright DAR ES SALAAM: Mwanasiasa mkongwe na mwanaharakati wa haki za wanawake, Gertrude Mongella, amewahimiza wanawake nchini kuhakikisha Rais Samia Suluhu Hassan anarudi madarakani katika uchaguzi ujao ili kuendeleza na kukamilisha mpango kazi wa kuwawezesha wanawake, unaotokana na maazimio ya Mkutano wa Beijing. Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka 30 ya Mkutano wa Beijing, Mongella alisema wanawake wanapaswa kuona nafasi ya kuwa na Rais mwanamke kama agenda yao kuu. “Ninajivunia sana. Juzi nilikuwa nje ya nchi, nikiona jinsi dunia inavyotazama mafanikio yetu. Sasa tunaye Rais mwanamke, tusipolinda hili kama ajenda yetu, ni bahati tunayoipoteza,” amesema Mongella kwa msisitizo. Aliongeza kuwa kurejea kwa Rais Samia si suala la kisiasa pekee, bali ni suala la kiuchungu kuhusu mwelekeo wa ajenda ya usawa wa kijinsia kama ilivyoainishwa katika Beijing Platform for Action. “Naomba Samia arudi ili kuimarisha ajenda yetu kwamba mwanamke an...

RAIS SAMIA KUWA MGENI RASMI HALFA YA UTOAJI TUZO

Image
Na Bright Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Wanahabari, maarufu kama Samia Kalamu Awards. Tuzo hizi zinalenga kuhamasisha uandishi wa habari za maendeleo kwa kufanya uchambuzi na utafiti wa kina, kuongeza maudhui ya ndani, kuzingatia weledi, maadili, uwajibikaji wa kitaaluma, kukuza uzalendo na kujenga taswira chanya ya nchi. Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo ambalo linatarajiwa kufanyika Aprili 29, 2025 Jijini Dodoma, ambalo limeandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Dkt. Rose Reuben, amesema kuwa jumla ya washindi 79 watatunukiwa tuzo. Amesema walengwa wa tuzo hizo ni waandishi wa habari, wachapishaji wa maudhui ya mtandaoni, maafisa habari, watangazaji pamoja na vyombo vya habari kwa ujumla. Dkt. Reuben ameeleza kuwa tuzo hizo zimegawa...

MAJALIWA KUONGOZA MATEMBEZi YA KUOKOA KILIMANJARO

Image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika matembezi ya kuhamasisha upandaji miti kwa ajili ya kuokoa mazingira ya Mlima Kilimanjaro, yatakayofanyika Mei 17, mwaka huu katika geti la Marangu, mkoani Kilimanjaro. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Nessa, Dobora Nyakisinda, amesema kampeni hiyo inayojulikana kama “Okoa Mlima Kilimanjaro” inalenga kupanda miti bilioni moja ifikapo mwaka 2050. Ameeleza kuwa hatua hiyo inalenga kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na ongezeko la joto duniani, hali inayosababisha kuyeyuka kwa kasi kwa barafu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro. “Watafiti wanasema katika kipindi cha miaka 30 hadi 50 ijayo, barafu tunayoshuhudia leo huenda ikatoweka kabisa. Ni jukumu letu Watanzania kushirikiana katika kulinda Mlima wetu,” amesema Nyakisinda. Amesema katika miaka mitano ya awali ya kampeni hiyo, wanatarajia kuanzia na mikoa minne ya Kanda ya Kaskazini ambayo ni...

DAR ES SALAAM KUOMBEA UCHAGUZI MKUU JUNI 21,

Image
Tamasha la Kuombea Uchaguzi Kuanza Dar es Salaam Juni 21, 2025 Tamasha kubwa la kuombea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 linatarajiwa kuanza rasmi Juni 21, 2025 jijini Dar es Salaam, likihusisha waimbaji wa nyimbo za injili kutoka ndani na nje ya Tanzania. Tamasha hilo litaendelea katika mikoa yote 26 ya Tanzania. Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Msama Promotions na muandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama, amesema lengo kuu ni kuliombea taifa libaki katika hali ya amani, upendo na usalama hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu. "Tamasha ni sehemu nzuri ya kuliombea taifa letu. Tunamuomba Mungu atupatie viongozi walioteuliwa na yeye mwenyewe – viongozi wa haki, wenye maono na hofu ya Mungu," alisema Msama. Amebainisha kuwa tayari mazungumzo yamekamilika na baadhi ya waimbaji kutoka mataifa mbalimbali, ikiwemo Afrika Kusini na Nigeria, huku mazungumzo yakiendelea na waimbaji kutoka Rwanda. Waimbaji wa ndani ya nchi nao wamejiandaa kush...

MAASKOFU KUSHIRIKI NA MSAMA PROMOTION LA KUOMBEA UCHAGUZI MKUU

Image
MAASKOFU na wachungaji wa Makanisa ya Pentecoste wameungana na Msama Promotion kushiriki kuwaombea viongozi wa taifa na Uchaguzi Mkuu katika tamasha litakaloanza Juni 21, Dar es Salaam na kuelekea mikoa mingine. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Aprili 13, Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama amesema viongozi hao wanashirikiana kuliombea tamasha liweze kufanikiwa. “Tumefanya kikao na baadhi ya watumishi wa Mungu wakiwemo Maaskofu, wachungaji na mitume na tutaendelea kushirikiana nao kuhakikisha tamasha linafanikiwa,”amesema. Amesema bado wanaendelea kuomba eneo la kufanyia tamasha hilo lakini wanasubiri kuona ombi lao la kutumia Uwanja wa Mkapa au Uhuru. Pia, wanaendelea kuzungumza na waimbaji wa muziki wa injili kutoka Afrika Kusini, Nigeria, Rwanda, Zambia na mataifa mengine wameshakubaliana nao. Kuhusu waimbaji wa ndani wameshamalizana nao. Msama amesema anaendelea kufanya mazungumzo na wadhamini mbalimbali kwani kuwaleta wasanii wa k...

ONYO KALI USIPOSTI PICHA YA MTOTO AU MTU YOYOTE BILA RUHUSA

Image
Usiposti Picha za Wengine Bila Ridhaa – Polisi Watoa Onyo Kali Dodoma – Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Wilfred Willa kutoka Kitengo cha Dawati la Jinsia, Ulinzi na Mtoto, Makao Makuu ya Polisi Dodoma, amewaonya wananchi dhidi ya tabia ya kuposti picha za watu wengine mitandaoni bila ridhaa yao, akibainisha kuwa kitendo hicho ni kosa la kisheria. Akizungumza katika mahojiano maalum, Willa amesema kuwa mtu yeyote anayeposti au kusambaza picha ya mtu mwingine mitandaoni bila idhini, anavunja Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 23 cha s heria namba 14 ya mwaka 2022. Sheria hiyo inalenga kulinda haki ya faragha ya mtu na kuzuia matumizi mabaya ya picha au taarifa binafsi kwenye mitandao ya kijamii. “Kosa hili linaweza kumgharimu mtu kifungo cha hadi miaka mitatu jela, faini ya Shilingi milioni tano, au adhabu zote kwa pamoja,” amesema Willa. Ameeleza kuwa watu wengi hawajitambui kuwa wanakiuka sheria wanapochukua na kusambaza picha za watu wengine mtandaoni bila ruhusa, jambo l...

UKWELI WA URAFIKI WA DIAMOND PLATNUMZ NA CHRISTIAN SHUSHO

Image
Christina Shusho: Sina Tofauti na Diamond Platnumz, Ni Mtu Mwema na Mwenye Mchango Mkubwa Katika Sanaa Msanii mahiri wa muziki wa Injili, Christina Shusho, amefunguka kuhusu uhusiano wake na msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz, akieleza kuwa hana tofauti naye na kumtaja kuwa ni mtu mwema mwenye mchango mkubwa katika tasnia ya muziki nchini. Akizungumza na vyombo vya habari, Shusho amesema kuwa hakuna tatizo lolote baina yao na kuwahimiza Watanzania kutambua umuhimu wa Diamond katika kukuza sanaa ya uimbaji. "Diamond Platnumz ni mtu mwema, sina shida naye hata kidogo. Kama tukipata nafasi ya kufanya kazi pamoja, niko tayari. Haijalishi anakuja kwa nafasi gani au anaomba wimbo wa aina gani — sote ni wanadamu, ni watu wa Mungu, tumeumbwa na Mungu, na tukiimba pamoja naamini tutamtukuza Mungu," alisema Shusho. Kauli hiyo imekuja kufuatia uvumi ulioenea kwamba kuna sintofahamu kati ya wasanii hao wawili katika maandalizi ya tamasha...

HUYU HAPA WEMA SEPETU WA MAMA SAMIA

Image
Mwigizaji nyota nchini WemaSepetu ametangaza hatua za kampeni yake ya kitaifa 'Wema wa Mama' inayolenga kuonyesha mafanikio makubwa ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Kupitia usahidi wa picha kila hatua kwa makala mbalimbali watazamaji watapata fursa ya kusikia moja kwa moja kutoka kwa wananchi waliofaidika na miradi ya serikali. Aidha, Wema Sepetu pia kwa atazungumza na kujionea miradi mikubwa ya maendeleo katika sekta za maji, afya, na elimu kwa lengo lingine la kuelewa namna fursa za maendeleo zilivyoanzishwa na zinavyohitaji nguvu kazi, uwekezaji, na ushirikiano wa wananchi. Kampeni hii inaadhimisha juhudi na mafanikio ya serikali, ikiwemo maeneo ya kipaumbele kama vile miundombinu, afya, elimu, na kilimo. Lengo ni kuhamasisha, kuunganisha na kuongeza ari ya maendeleo katika jamii nzima ya Watanzania.

BOLT IMEZINDUA HUDUMA ZAKE KAHAMA

Image
Kampuni ya usafiri wa mtandaoni Bolt, inayoongoza nchini Tanzania, imezindua rasmi huduma zake katika mji wa Kahama, hatua inayochukuliwa kuwa mafanikio makubwa katika juhudi zake za kuleta suluhisho la usafiri wa kisasa, wa kuaminika na nafuu kwa mikoa mingi zaidi nchini. Uzinduzi huu ni sehemu ya mkakati mpana wa Bolt wa kuimarisha usafiri mijini na kuwa wezesha jamii za nje ya miji mikuu. Uwepo wa Bolt Kahama unatarajiwa kubadilisha namna ambavyo wakazi, wafanyabiashara wadogo na wasafiri wa kila siku wanavyohama kutoka eneo moja kwenda jingine katika mji huu wenye shughuli nyingi za biashara na uchimbaji madini. Kwa mujibu wa taarifa ya mwaka 2023 kutoka UN-Habitat, miji ya Tanzania ni miongoni mwa miji yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika, hasa kutokana na uhamiaji kutoka vijijini kwenda mijini. “Utafiti wa mwaka 2015 ulibaini kuwa asilimia 61.4 ya wakazi wa mijini walihamia kutoka vijijini, huku asilimia 38.6 walizaliwa mijini,” inaeleza ripoti hiyo, ikisisitiza ...

IRENE UWOYA AZUA GUMZO MTANDAONI KWA PICHA NA MPENZI WAKE

Image
Msanii wa Filamu Irene Uwoya 'Mama Mchungaji ameposti picha zikionyesha yupo kwenye mapozi na mkaka black wakiwa wamevalia mavazi flani kama unavyoona picha. picha hizo zimezia mjadala mlubwa mitandaoni na kuanza kuuliza kama ameshaulowa au anatarajia wengine wakimpongeza na wengine wanasema uenda ikawa ni tamthilia mpya ameigiza. Hadi sasa Uwoya mwenyewe hajatoa ufafanuzi wowote kuhusu picha hizo, jambo linaloacha mashabiki wake kwenye sintofahamu.

LAMATA NILIKUWA CHAWA MBEBA POCHI ZA WASANII NA KUWAPIGIA PASI

Image
Mwongozaji na Mtayarishaji wa Filamu nchini Leah Mwendamseke 'Lamata' amesema kabla ya kuwa mwongoza tamthilia alikuwa anabeba bochi za wasanii location. Lea amesema kuwa kipindi hicho anabeba pochi lakini alikuwa akiandika stori zake na kuzihifadhi Kuna msanii maarufu alikataa nisimdirect. "Zamani nilikuwa naandika story hivyo kazi yangu nyingine ilikuwa kubeba pochi za wasanii na kunyoosha nguo zao na mara ya kwanza napewa kazi ya ku-direct movies msanii mkubwa aligoma siwezi kumuongoza kwenye movie sababu nabeba pochi zake"Lamataleah Kunachakujifunza haijalishi unapitia nini Fanya ili kufikia lengo lako unalotaka dhahabu lazima ipite kwenye moto ili kujulikana kuwa ni dhahabu.