Posts

Showing posts from October, 2025

MSAMA: ASILIMIA 70 YA WAPIGA KURA WAKO TAYARI KUMCHAGUA DKT. SAMIA.

Image
MSAMA: ASILIMIA 70 YA WAPIGA KURA WAKO TAYARI KUMCHAGUA DKT. SAMIA. Kada wa Chama cha Mapinduzi na Mkurugenzi wa Msama Promotion Ndugu Alex Msama amesema kuwa kwa takwimu zilizopo, Mgombea Urais kupitia CCM Dkt Samia Suluhu Hassan atashinda Uchaguzi wa kesho kwa kishindo kikubwa. Msama amesema hayo kutokanana na takwimu zilizotolewa jana na Katibu Mwenezi wa Chama hicho Ndugu. Kenani Kihongosi kuwa Watanzania Milioni 25 walifuatilia kwa karibu sana Kampeni za Mgombea Urais kupitia CCM Dkt Samia Suluhu Hassan. Msama ameongeza kuwa na Watanzania wengine zaidi ya Milioni 5 wamefuatilia Kampeni hizo bila kufika kwenye mikutano, hivyo kufanya jumla ya wafuatiliaji wa Dkt. Samia kufikia Milioni 30. Msama amemaliza kwa kusema kuwa kwa takwimu kama hizo basi Dkt. Samia atashinda Uchaguzi Mkuu kwa kishindo kikubwa na atavunja rekodi kuwa Rais aliyechaguliwa kwa kura nyingi kuliko yeyote yule.

USITAFUTE MATATIZO KUTAKA KUITWA SHUJAA

Image
Msanii wa filamu na Mwenyekiti wa Mama Ongea na Mwanao Steve Nyerere amewataka vijana kuwa waangalifu na nyakati ambazo serikali inapambana kuwaonganisha Watanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu October 2025. Amesema hayo yakiwa yamepita masaa machache Jeshi la Polisi litoe taarifa ya kumshikilia mfanyabiashara na Mwana Mitandao Niffer kwa madai ya kuhamasisha vurugu kuelekea Uchaguzi Mkuu. Steve ameandika “Angalia sana maisha yako. Utulivu ni njia ya mafanikio. Yawezekana kuna vitu huvipendi, lakini kuna utaratibu wa kuvipisha na kuviweka kando ili uwe na amani ya roho. Vijana wengi wameingia kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kwa kufuata mkumbo, wakiamini kuwa ‘mbona fulani anavuta, kwa nini mimi nisivute?’ Wakasahau kwamba madawa ya kulevya ni haramu na hayaruhusiwi. Kufuata mkumbo kunaweza kukupoteza, ukajiona uko juu ya sheria. Kila ukiambiwa kuwa madawa ya kulevya ni haramu — kwa afya yako, kwa sheria za nchi, na hata kwa utamaduni wetu unapuuzia. Sikio halisikii likishajaa ujua...

AGNESTA KAIZA AAHIDI MIKOPO KWA WANAWAKE, VIJANA NA WALEMAVU SIKU 100 ZA KWANZA

Image
Agnesta Kaiza Aahidi Mikopo kwa Wanawake, Vijana na Walemavu Ndani ya Siku 100 za Kwanza Mgombea Ubunge wa Jimbo la Segerea kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Agnesta Kaiza, ameahidi kwamba ndani ya siku 100 za kwanza baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge, atahakikisha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu wa jimbo hilo wanapata mikopo ya asilimia 10 kama inavyotakiwa kisheria. Kaiza alitoa ahadi hiyo wakati wa kufunga kampeni zake katika Jimbo la Segerea, akisisitiza kuwa fedha hizo ni haki ya makundi maalum na zitarudishwa kwao ili ziweze kujikwamua kiuchumi kupitia vikundi vya ujasiriamali. “Fedha hizo ni haki yao. Nitahakikisha zinarudi kwa walengwa ili ziweze kuwasaidia kuanzisha na kukuza biashara zao,” amesema Kaiza. Mbali na hilo, Kaiza aliahidi kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo, akibainisha kuwa tatizo la maji Segerea litakuwa historia endapo atapewa ridhaa ya wananchi. “Nitahakikisha wananchi wanapat...

WATAALAMU WA AUSTRALIA WAFANIKIWA KUFANYA UPASUAJI WA MOYO WAGONJWA 17 WA KITANZANIA

Image
JKCI na Wataalamu wa Australia Wafanikiwa Kufanya Upasuaji wa Moyo kwa Wagonjwa 17 wa Kitanzania Na Brighiter Dar es Salaam TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Shirika la Open Heart International la Australia, wamefanikiwa kufanya upasuaji kwa wagonjwa 17 wa Kitanzania. Wataalamu wa Open Heart International wapo nchini kwa kipindi cha siku 14 ambapo kati ya wagonjwa waliotibiwa, 13 ni watoto na wanne ni watu wazima. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk. Peter Kisenge amesema kuwa Open Heart International imekuwa ni moja ya washirika wakubwa wa taasisi hiyo, na hadi sasa wameitembelea JKCI takribani mara 14 tangu ilipoanzishwa. Dk. Kisenge amelipongeza shirika hilo kwa kujitolea na kujituma katika kuokoa maisha ya Watanzania, akisisitiza kuwa uhusiano huo mzuri unatokana na juhudi za serikali katika kuimarisha uhusiano na serikali ya Australia. “Serikali imechangia kwa kiasi kiku...

BSS NEXT LEVEL REVOLUTION KUONYESHWA SINEMA ZETU MSHINDI KUONDOKA NA MILlON 50, GARI

Image
BSS Next Level Revolution Yazinduliwa Rasmi, Mshindi Kuondoka na Milioni 50 na Gari Na Brighiter Masaki, DAR ES SALAAM:MSIMU wa 16 wa tamasha la kusaka vipaji la Bongo Star Search (BSS) Next Level Revolution mwaka huu umebeba sura mpya, likitarajiwa kuanza rasmi Novemba 22, 2025 mkoani Mwanza katika ukumbi wa La Kailo Hotel. Mshindi wa kwanza wa msimu huu ataondoka na zawadi ya Shilingi milioni 50 pamoja na gari jipya. Akizungumza na Spoti Leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa shindano hilo, Madam Rita Paulsen, amesema kuwa msimu huu utakuwa wa kipekee kwa kuwa utaangazia vipaji vyote ikiwemo uimbaji, uchoraji, sarakasi, uchekeshaji, upigaji vyombo na uchezaji. “Nimesimama kwa heshima kubwa na furaha isiyoelezeka kutambulisha rasmi msimu wa 16 wa Bongo Star Search msimu mpya wenye sura mpya, nguvu mpya na dira mpya,” amesema Madam Rita. “Pia ninayo furaha kutangaza rasmi ushirikiano wetu wa kimkakati kati ya Benchmark 360 na Azam Media, ambao tunauita ‘ndoa ya ma...

UDSM YATEKELEZA MRADI WA HEET ELIMU KIDIGITALI

Image
Na Brighitte, Dar es Salaam CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kinaendelea kutekeleza kwa mafanikio Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Uchumi (HEET), ambao unalenga kuboresha miundombinu, kuimarisha mitaala, na kuendeleza mfumo wa kujifunza kwa njia ya kidijitali. Mradi huo wa kimkakati una umuhimu wa kitaifa katika kubadilisha elimu ya juu kuwa chachu ya uchumi wa viwanda na maendeleo endelevu ya Taifa. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa William Anangisye, alisema mradi wa HEET ni mpango wa kitaifa unaotekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa thamani ya Dola za Marekani milioni 425. “Lengo kuu la mradi huu ni kuboresha mazingira ya kusomea na kuhakikisha mitaala ya vyuo inalingana na mahitaji ya soko la ajira,” amesema Prof. Anangisye. Aliongeza kuwa chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, UDSM imetengewa kiasi cha Dola m...

VIJANA WA TANZANIA HAWAPO TAYARI KUISHI BILA AMANI

Image
Steve Nyerere: Vijana msishiriki maandamano, tulinde amani ya taifa – Dar es Salaam Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanae, Steve Nyerere, amewataka vijana nchini kujiepusha na maandamano na badala yake kushikamana kulinda amani na utulivu wa taifa. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Steve alisema Tanzania imekuwa mfano wa nchi zenye amani barani Afrika, hivyo vijana wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuilinda na kuienzi hali hiyo. “Mtanzania yeyote hana tabia ya kuandamana, bali kushikamana. Nchi yetu ina amani ambayo imejengwa kwa muda mrefu; ikipotea, kuirudisha ni jambo gumu sana,” amesema Steve. Aliongeza kuwa vijana wanapaswa kuelekeza nguvu zao katika kujenga uchumi, kushiriki shughuli za maendeleo na kuunga mkono juhudi za serikali zinazoendelea kuimarisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa. “Vijana ndio nguvu ya taifa, tuitumie vizuri nguvu hiyo kwa manufaa ya taifa letu, siyo kujiingiza katika mambo yanayoweza kuvuruga amani,” ameisitiza.

MSAMA WANANCHI WA DAR TUJITOKEZE KUMPOKEA RAIS SAMIA

Image
Na Brighitte Dar es Salaam Aliyekuwa mtia nia wa Ubunge Jimbo la Ukonga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Production, Alex Msama, ametoa wito kwa wananchi wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kumpokea na kushiriki katika kampeni za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM na mgombea urais kupitia chama hicho. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Msama alisema ujio wa Rais Samia katika jiji hilo ni tukio muhimu linaloonesha dhamira yake ya kukutana na wananchi na kuwasikiliza moja kwa moja kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29. Amesema Rais Samia amekuwa akipokelewa kwa shangwe na hamasa kubwa katika mikoa yote aliyoitembelea, jambo linaloonyesha mapenzi makubwa ya wananchi kwake. “Rais wetu amezunguka katika mikoa mingi na kila alipofika amepokelewa kwa furaha kubwa. Sasa anakuja Dar es Salaam, hivyo ni jukumu letu wakazi wa jiji hili kujitokeza kwa wingi kumpokea na kumuunga mkono kat...

CHALAMILA ARUDISHA TABASAMU LA MJANE

Image
ARUDISHA TABASAMU KWA MJANE BI ALICE HAULE Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila amehitimisha mgogoro wa nyumba kiwanja namba 819 Msasani beach uliomhusisha mjane wa marehemi Justice Rugaobula, Bi Alice Haule na Muhammed Mustafa Yusuf Ali ambapo amemkabidhi hati maalum iliyotolewa na wizara ya Ardhi ambayo inamtambilisha Bi Alice Haule ndiye msimamizi halali wa mirathi kisheria baada timu ya wataalamu aliyoiunda kujiridhisha kuwa mjame huyo ndiye anaepaswa kukabidhiwa umiliki wa nyumba hiyo kama msimamizi wa mirathi Akizungumza leo Octoba 20,2025 Jijini Dar es Salaam RC Chalamila amesema baada ya kuibuka kwa mgogoro huo wa nyumba aliamua kuunda timu maalum ya wataalamu iliyohusisha wataalamu kutoka ofisi ya kamishna wa ardhi, jeshi la polisi na mawakili kutoka pande zote za mgogoro ambapo timu hiyo imejiridhisha kuwa Bi Alice ndio mwenye haki kwenye nyumba hiyo kama msimamizi wa mirathi ya marehemu mumewe bwana Justice Rugaobula Aidha RC Chalamila baada ya kumkabid...

DAR CITY YAANZA VIZURI KUFUZUKWA BASKETBALL

Image
Timu ya mpira wa kikapu ya Dar City imeanza vizuri kampeni zake za kufuzu kwa Basketball Africa League (BAL) 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa pointi 102–50 dhidi ya Djabal kutoka Comoros. Mchezo huo umechezwa leo katika viwanja vya shule ya IST, vilivyopo Masaki, Dar es Salaam, ambapo Dar City ilionyesha ubabe na kuutawala mchezo kuanzia mwanzo hadi mwisho. Kesho, Dar City itashuka tena uwanjan kwa mchezo wa mwisho wa hatua ya kufuzu dhidi ya Blazers kutoka Uganda.

SERIKALI KUZALISHA NGUVU KAZI YENYE UJUZI, UBUNIFU KWA KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA

Image
Na Brigitter DAVIS DAR ES SALAAM:SERIKALI imepongeza Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kwa kuandaa mkutano muhimu kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ubora wa elimu ya ufundi na kuongeza ujuzi wa nguvukazi nchini. Akizungumza katika mkutano huo kati ya VETA, wamiliki wa viwanda, waajiri na wadau wa ufundi stadi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo, alisema Serikali inaendelea kusimamia utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya mwaka 2014 (Toleo la 2023), inayolenga kujenga mfumo wa elimu unaozingatia ujuzi, ubunifu na tija katika soko la ajira. Amesema lengo ni kuhakikisha Tanzania inazalisha nguvukazi yenye ujuzi na umahiri unaokidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye ya soko la ajira na maendeleo ya viwanda nchini. Profesa Nombo alisema Serikali kupitia VETA imeendelea kuboresha mitaala, miundombinu na mbinu...

DAR CITY KUKIWASHA KESHO

Image
DAR City Yahitaji Sapoti Yenu Kesho Na Brigitter DAVIS, DAR ES SALAAM:NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma (Mwana FA), amewataka mashabiki wa michezo nchini kujitokeza kwa wingi kushuhudia mashindano ya kimataifa ya mpira wa kikapu “Road to BAL”, yatakayofanyika kesho (Ijumaa) katika Uwanja wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST), jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo ya raundi ya awali yatashirikisha timu ya Dar City kutoka Tanzania, pamoja na timu kutoka Uganda na Visiwa vya Comoro. Timu mbili zitakazoongoza zitasonga mbele hatua ya 16 bora, itakayochezwa nchini Kenya au Afrika Kusini, ambako timu nne bora zaidi zitafuzu hatua ya robo fainali. “Mashindano haya si jambo dogo kwa mchezo wa kikapu. Ni fursa kwa Watanzania kujionea mashindano ya kimataifa yakichezwa hapa nyumbani,” amesema Mwinjuma. Ameongeza kuwa serikali inafarijika kuona maendeleo ya mchezo huo nchini, huku akipongeza klabu ya Dar City kwa maandalizi bora na ushiriki wake ka...

WiLDAF TANZANIA NA GIZ WAWANOA WAANDISHI KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA MTANDAONI WAKATI WA UCHAGUZI

Image
WiLDAF Tanzania na GIZ Waandaa Kambi Maalum ya Mafunzo kwa Waandishi wa Habari Kupinga Ukatili wa Kijinsia Mtandaoni na Wakati wa Uchaguzi Brigitte Davis DAR ES SALAAM Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF Tanzania) kwa kushirikiana na GIZ limeendesha Kambi Maalum ya Mafunzo kwa Waandishi wa Habari kwa muda wa siku tatu, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea Kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia mwaka 2025. Mafunzo hayo pia yanalenga kuunga mkono juhudi za kitaifa kupitia Mdahalo wa Kitaifa kuhusu Ukatili wa Kidijitali na Ukatili Dhidi ya Wanawake katika Uchaguzi. Kambi hiyo imewaleta pamoja waandishi wa habari na wataalamu wa mawasiliano ili kuwajengea uwezo katika maeneo mbalimbali ikiwemo uhusiano kwa umma, maadili ya mawasiliano, uandishi wa habari wenye weledi, usalama wa kidijitali, na usimulizi wa maudhui yanayozingatia usawa wa kijinsia na haki za binadamu. Kupitia mafunzo hayo, washiriki wanatarajiwa kupata ujuzi ...

SWAHILI FASHION WEEK WAZINDUA NEMBO BRAVO COCO BEACH

Image
Swahili Fashion Week yazindua nembo mpya, yalenga mageuzi ya Kidijitali Na Brigitter Davis, DAR ES SALAAM:WIKI ya Mitindo ya Kiswahili (Swahili Fashion Week and Awards) imetangaza rasmi kuwa msimu wake wa 18 utafanyika kuanzia Desemba 5 hadi 7, 2025, katika Ukumbi wa Parthenon, Klabu ya Greek Hellenic, barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam. Jukwaa hilo lenye heshima kubwa katika tasnia ya mitindo barani Afrika linatarajiwa kuwakutanisha wabunifu zaidi ya 46 kutoka Tanzania, Kenya, Italia, Afrika Kusini, Trinidad & Tobago na mataifa mengine duniani. Mwaka huu, Swahili Fashion Week unaashiria hatua muhimu ya mageuzi kwa uzinduzi wa nembo mpya, ishara ya mabadiliko, ubunifu na mwanzo wa enzi mpya ya kisanaa. Akizungumza na Spoti Leo wakati wa uzinduzi wa nembo hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Bravo, Coco Beach jijini Dar es Salaam, Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Swahili Fashion Week and Awards, Mustafa Hassanali, alisema kauli mbiu ya mwaka huu inaangazia mch...

CRDB WAKUTANA NA MAWAKALA MIAMALA ZAIDI YA MILlONI 200 ZAPITIA KWA WAKALA

Image
Miamala Zaidi ya Milioni 200 Yenye Thamani ya Trilioni 70 Zapitia Mawakala wa Benki ya CRDB Zaidi ya miamala milioni 200 yenye thamani ya takribani Shilingi trilioni 70 imefanyika kupitia mawakala wa Benki ya CRDB nchini kote katika kipindi cha mwaka mmoja. Kati ya kiasi hicho, zaidi ya Shilingi trilioni 3 ni makusanyo ya Serikali yaliyopokelewa kupitia mfumo wa uwakala wa benki hiyo. Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kongamano na mawakala wa Benki ya CRDB, Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam, Muhinuliza Buberwa, amesema mafanikio hayo yanaonesha jinsi huduma za kifedha kupitia mawakala zinavyochangia kukuza ujumuishi wa kifedha na kuongeza mapato ya Serikali. Buberwa amesema kwa sasa Benki ya CRDB ina zaidi ya mawakala 45,000 nchini, sawa na asilimia 55 ya mawakala wote wa huduma za kifedha nchini. “Kuwepo kwa idadi kubwa ya mawakala ni jitihada kubwa ya Benki ya CRDB, lakini mafanikio haya yasingepatikana bila ushirikiano wenu mawakala. Kwa sasa, sehemu kubw...

VIJANA WAELIMISHWA UHIFADHI WA MAZINGIRA KUPITIA MRADI WA PLAY TO ZERO

Image
Vijana waelimishwa kuhusu uhifadhi wa mazingira kupitia Mradi wa Play to Zero Na Brigitter Kisarawe Wadau mbalimbali wa mazingira wamepanda miti 100 katika Shule ya Sekondari Minaki, Wilaya ya Kisarawe, kupitia Mradi wa Play to Zero, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhamasisha vijana kushiriki kikamilifu katika kulinda mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Zoezi hilo limehusisha wanafunzi na walimu wa shule hiyo pamoja na washiriki wa mradi, ambapo walipanda miti kwa vitendo na kutoa elimu ya mazingira kwa wanafunzi. Lengo ni kuwajengea vijana uelewa wa umuhimu wa misitu katika kuhifadhi hewa safi, kupunguza joto duniani, na kukuza utamaduni wa utunzaji wa mazingira shuleni. Mradi wa Play to Zero unatekelezwa kwa ushirikiano wa taasisi kadhaa zikiwemo Africa Carbon Agency, Klabu ya Mpira wa Miguu ya Africa Lyon, Swiss Tanzania Chamber of Commerce, na Hajakaa Ya Mwisho Foundation. Wadau hawa wamejipanga kukuza ushiriki wa vijana katika michezo na uhifadhi wa ma...