SAFARI BLACK MINERAL WATER YASHIKA SOKO MAREKANI

Safari Black Mineral Water gumzo Marekani Na CHRISTOPHER MSEKENA MTANZANIA anayekuja kwa kasi kwenye ulimwengu wa biashara duniani, Vincent Kiango, ametambulisha maji yenye chapa Safari Black Mineral Water katika soko la vinywaji baridi nchini Marekani. Bidhaa hiyo ya maji safi ya kunywa imegeuka kivutio kikubwa kwa wananchi huko ughaibuni kwa aina ya ladha tamu, chupa na chapa inayovutia machoni hivyo kuleta ushindani mkubwa kwenye soko la vinywaji baridi. Akizungumza na gazeti hili, Vincent Kiango alisema Safari Black Mineral Water ni bidhaa inayojitosheleza huku ikijikita katika ubora wenye kuzingatia afya kwa mnywaji tofauti na maji mengine ambayo hutuwa chemikali za kuhifadhia chakula.
"Wateja wanahitaji maji yanayojali afya zao, Safari Black Mineral Water ni bidhaa mpya mjini hapa Marekani lakini inapendwa na wengi hasa ndugu zetu wazungu ambao wanajali afya zao. Tumezingatia vifungashio vya maji yetu ni vizuri, chupa zake zinabebeka kirahisi lakini pia yanakata kiu vizuri bila kuwa na madhara kwa mnywaji," amesema Vincent. Aliongeza kuwa bidhaa hiyo kwa sasa inapatikana nchini Marekani na inasambaa ulimwengu mzima ikiuzwa online kupitia Amazon. Aidha alisisitiza kuwa kwa kuweka oda ya maji hayo wanafanyabiashara wa vinywaji baridi wanaweza kutembelea tovuti yao safariblackwater.com na kujipatia bidhaa hiyo mpya yenye wapenzi wengi. @@@

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA