DAR CITY YAANZA VIZURI KUFUZUKWA BASKETBALL
Timu ya mpira wa kikapu ya Dar City imeanza vizuri kampeni zake za kufuzu kwa Basketball Africa League (BAL) 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa pointi 102–50 dhidi ya Djabal kutoka Comoros.
Mchezo huo umechezwa leo katika viwanja vya shule ya IST, vilivyopo Masaki, Dar es Salaam, ambapo Dar City ilionyesha ubabe na kuutawala mchezo kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Kesho, Dar City itashuka tena uwanjan kwa mchezo wa mwisho wa hatua ya kufuzu dhidi ya Blazers kutoka Uganda.

Comments
Post a Comment