Posts

Showing posts from October, 2024

LG MOSQUITO AWAY KUFUKUZA MBU

Image
Imebainishwa kuwa uwepo wa teknolojia mpya ya kufukuza mbu Kwa njia ya kiyoyozi itasaidia Kwa kiwango Kikubwa kidhibiti ugonjwa huo ambao umekuwa ni changamoto Kwa nchi zinazoendelea Tanzania ikiwemo. Serikali inaendelea na Mipango yake ya kupanga mikakati ya namna ya kupambana na ugonjwa wa Malaria na Mbu wanaoeneza Ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na  kuhakikisha inaweka mfumo mzuri wa namna ya kupambana na malaria ili kuweza kuokoa nguvu kazi ya Taifa na rasilimali zitakazotumika katika kutibu ugongwa huo. Kauli hiyo imetolewa na Prof Amos Mwakigonja katika katika uzinduzi wa AC yenye teknolojia mpya ya kufukuza mbu Kwa njia ya kiyoyozi iliyobuniwa na kampuni ya LG ambayo inatajwa kuwa na ufanisi mkubwa na rafiki kwa mazingira. Teknolojia hiyo ya kufukuza mbu Kwa njia ya kiyoyozi itawasaidia wa Tanzania kutokung’atwa na mbu na hivyo Kasi ya  watu kupata malaria itapungua na magonjwa yanayoenezwa na mbu pia yatapungua kwa kiasi kikubwa. Aidha Serikali na wadau wanaendelea kuweka ...

USAILI WA BSS KUANZA ARUSHA NO 9 NA 10

Image
  USAHILI wa Wasanii wa Shindano la  Bongo Star Search African kuanza kufanyika Mkoani Arusha Novemba 9 hadi 10 katika ukumbi wa SG Resourt Mianzini. Akitaja maeneo ambayo usahili utafanyika wa Bongo Star Search African Madam Ritha amesema kuwa Usaili utaanza Arusha na baadaye Mkoani Mwanza. "Mkoani Arusha Novemba 9 hadi 10 2024 SG Resourt Mianzini, Mwanza Novemba 16 hadi 17 mwaka huu La Kairo  Hotel, Kampala Novemba 23 hadi 24 mwaka huu, Nairobi Novemba 30 hadi 01DEC 2024 Little Thiether Babati Desemba 6 hadi 7 Olympic Lounge huku Dar es Salaam ikiwa Decemba 13 hadi 15, 2024 katika ukumbi wa Makumbusho ya ya Taifa Bongo Star Search Afrika! Madam Ritha aliongeza kwa kuwashukuru wadhamini kwa kuendelea kuwa shika mkono kwa juhudi wanazofanya kuendelea tasnia ya burudani nchini. "Kwa wadhamini wetu na washirika wa Bongo Star Search, tunatoa shukrani. Hamjawa tu wadau, bali ni sehemu muhimu ya mafanikio ya mpango huu. Ushirikiano wenu umetufanya kufikia malengo haya ya kupan...

S2KIZZY ZOMBI & MADAM RITHA MAJAJI BSS AFRICA

Image
JAJI Mkuu wa Shindano la kusaka Vipaji Bongo Star Search African 'BSSA' Ritha Poulsen  ametangaza majaji watakao jaji katika mashindano Projuza S2kizzy Zombi akiwa miongoni mwao. Akitaka majaji hao wa Bongo Star Search African jijini Dar es Salaam, Madam Ritha amesema kuwa mara zote wamekuwa na wasanii kwa mwaka huu mambo yamebadilika watakuwa na Projuza S2kizzy Zombi. 'Mashindano ya haya yataongozwa na  Kikosi kazi cha majaji watakao jaji msimu wa kumi na tano Jaji Mkuu Ritha Paulsen 'Madam Ritha', Johakim Kimario 'Master J' Jaji Produza S2KZ Zombi, Salama Jabiri majaji kutokaka Nchini Tanzania lakini kutakuwa na majaji wawili watakao jaji kutoka nchini Kenya Sanaipei Tande na Lilian Mbabazi kutokea Uganda" "Napenda kukukaribisha katika familia ya Bongo Star Search African naamini utakuwa na Mchango mkubwa katika kutafuta Vipaji vipya. "Watangazaji watakao sherehesha msimu wa kumi na tano wa Kipindi cha BSS ni Idris Sultan pamoja na Meena All...

BSS AFRICA YAZINDULIAWA RASMI KUONESHWA STARTIMES

Image
SHINDANO la kusaka Vipaji Tanzania Bongo Star Search 'BSS' misimu wa kumi na tano umezinduliwa rasmi kwa sasa ni Bongo Star Search African wataenda kimataifa Kenya, Uganda na Congo. Akizungumza na wakati wa uzinduzi wa misimu huo mpya Mkurugenzi Mkuu wa Benchmark 360 Limited Rita Paulsen amesema kuwa Msimu huu wa kumi na tano wa Bongo Star Search ni wa kipekee sana, na ni wa kihistoria.  "Kwanza kabisa, napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mungu na kuwashukuru wote  mliojitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hii kubwa, uzinduzi wa msimu mpya wa Bongo Star Search Afrika. "Kwa miaka mingi tumeweza kuibua vipaji kutoka Tanzania pekee, lakini msimu huu tunaingia hatua ya juu kabisa. Kwa mara ya kwanza, tunavuka mipaka ya nchi, tukifanya usahiri katika nchi zaidi ya tano, zikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, na Congo. "Lengo letu kuu ni kufungua fursa kwa vijana wengi zaidi kutoka ukanda mzima wa Afrika Mashariki na Kati, kuwapa jukwaa la kuonesha vipaji vyao na k...

FCS WAINGIA MKATABA NA LATRA CCC ULINZI WA USAFIRISHAJI

Image
Foundation for Civil Society (FCS) na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) wamesainiana Mkataba wa Makubaliano (MoU) wa miaka mitatu ili kuimarisha ulinzi wa walaji na haki zao ndani ya sekta ya usafiri ili kuwe na huduma bora kwa Wasafirishaji na wasafiri. Akizingumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Justice Rutenge amesema kuungana kw FCS na LATRA CCC wanakusudia kuunda mazingira bora ya walaji katika sekta ya usafiri wa ardhi, kukuza taratibu bora za kibiashara na kuhamasisha ukuaji wa biashara. Amesema ushirikiano huo unalenga kuwakilisha maslahi ya walaji wanaotumia usafiri wa ardhi ulio na udhibiti kwa ajili ya bidhaa na huduma katika nchini ambapo MoU itahakikisha wasafiri na wasafirishaji kwa njia ya ardhini wanapata huduma bora zenye kukidhi matakwa ya kitaifa na kimataifa. Pia  Ushirikiano huo wa kimkakati utahusisha kubuni na kutekeleza mipango inayokuza haki za walaji na kulinda bidhaa na hu...

BENKI YA ABSA TANZANIA YAFANYA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA HUDUMA ZA KIDIGITALI

Image
Benki ya Absa Tanzania imesema imefanya uwekezaji mkubwa katika huduma zake za kibenki kwa njia za kidigitali ili kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha huduma za kibenki zinawafikia watanzania wengi na kwa gharama nafuu. Hayo yalisemwa na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa benki hiyo, Ndabu Lilian Swere wakati wa droo ya kwanza ya Kampeni ianyoendelea ya ‘Tumia Ushinde’ (Spend & Win), ambayo lengo lake kubwa ni kuhamasisha wateja wa benki hiyo na watanzania kufanya miamala mbalimbali ya kibenki kwa kutumia kadi ama huduma za kibenki kwa njia za kidigitali. “Kampeni hii ya miezi mitatu ina lengo la kuwazawadia gari wateja wetu wanaofanya miamala ya kibenki kwa kutumia kadi za ATM ama huduma za kidigitali kwa kutumia mifumo yetu inayowawezesha wateja kupata huduma kiuharaka na kiurahisi hivyo kutimiza malengo yao. “Sisi kama Absa Benki Tanzania tumeimarisha huduma zetu za kidigitali ili kwenda sambamba na jitihada zinazofan...

VIONGOZI KUANZA KUCHUKUA FOMU ZA KUGOMBEA SERIKALI ZA MITAA

Image
Kuanzia Oktoba 26 hadi Novemba 1 mwaka huu wagombea wa ngazi mbalimbali za Serikali za Mitaa wanatakiwa kujitokeza kuchukua fomu ya kugombea nafasi hizo. Hayo amesema Leo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa Tamisemi Mohamed Mchengerwa alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kuwataka wananchi kujitokeze kugombea nafasi mbalimbali za serikali za mitaa. "0ktoba 26 hadi 1 Novemba mwaka huu wagombea wanatakiwa kujitokeza kuchukua fomu ya kugombea uongozi wa ngazi mbalimbali za  Serikali."amesema Mchengerwa  Pia amesema Novemba 27, 2024 wananchi wajitokeze kupiga kura kuchagua viongozi wanawataka wao ambao watakuwa wawakirishi wao katika kutatua changamoto zilizopo katika maeneo yao. Mchengerwa amesema Watu Milioni 32.9 sawa na asilimia 94.8 wamejitokeza kujiandikisha mwaka huu, ukilinganisha na mwaka 2019 ni sawa na asilimia 86 wamezidi kujitokeza kwa kuitikia wito wa kujiandikisha katika daftari la wapiga kura. Aidha ameo...

CELEBRATING WORLD TEACHER'S DAY: HONORING THE HEROES OF EDUCATION

Image
By Sunil Taldar During World Teachers’ Day, we come together to celebrate the invaluable contributions of teachers across the globe. This year’s theme, “The Teachers We Need for the Education We Want: The Global Imperative to Reverse the Teacher Shortage,” emphasizes a challenge that is both critical and urgent ensuring every child has access to quality education guided by dedicated and empowered educators. At Airtel Africa, we deeply appreciate the pivotal role that teachers play in shaping our future. They are the backbone of society, equipping our children with the knowledge, skills, and values needed to navigate an ever-changing world. Teachers are not just instructors; they are mentors, role models, and catalysts for innovation and change. Indeed, for effective learning to take place, there must be committed, trained, and motivated teachers in the value chain. The Power of Education Education is the cornerstone of societal growth and individual empowerment. It unlocks opportunitie...

ZANZIBAR KUCHUKUA HATUA UFUNGUJI KUKU

Image
  Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo wa Zanzibar, Shemata Khamis, amesema Serikali ya Zanzibar imechukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha sekta ya ufugaji wa kuku inakua na kuleta tija kwa wananchi, ikiwemo kuwajengea uwezo wataalamu wa ndani juu ya mbinu za kisasa za ufugaji bora na udhibiti wa magonjwa. Khamis alitoa kauli hiyo Oktoba 17, 2024, jijini Dar es Salaam, alipokuwa akihitimisha Mkutano wa Jukwaa la Tasnia ya Kuku na Ndege Wafugwao kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC). Alisema kuwa serikali imeimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa ya kuku na ndege wafugwao ili kudhibiti milipuko ya magonjwa na kuimarisha utekelezaji wa afua za afya. “Mikakati hiyo ni pamoja na kuanzisha mashamba ya kuku, uwekezaji katika maeneo ya kutotoleshea vifaranga vya kuku, kuanzishwa kwa kiwanda kipya cha vyakula vya mifugo, machinjio mapya ya kuku, na maabara za mifugo zinazowezesha uchunguzi na uzalishaji wa chanjo za mifugo. Pia, tumeanzisha vituo vya utafiti wa kuku,” ali...

MITIHANI ALIZOPITIA DR TAX

Image
Hii ndiyo mitihani migumu iliyowahi kumkabili Dk TAX Simulizi ya safari ya elimu na Utumishi wa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Stergomena Tax ni historia inayosisimua, ikihusisha nyakati ngumu na juhudi kama ufunguo wa nyakati hizo. Pengine kila anayeonekana na mafanikio leo, zipo nyakati ngumu alizopitia jana ambazo kama si kukomaa asingeupata umaarufu alionao. Katika hili, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Stergomena Tax ni kielelezo sahihi, anayesimulia magumu aliyowahi kupitia katika safari yake ya kuisaka elimu. Kwa mujibu wa waziri huyo ambaye ni mwanamke wa kwanza kuiongoza wizara hiyo, magumu hayo yalitokana na kigugumizi cha nini alipaswa kuchagua kati ya kulea mtoto au kwenda nje ya nchi kujiendeleza na elimu. Ingawa wakati huo, mwanawe huyo alikuwa na umri wa miaka minne, anasema kwa mzazi isingekuwa rahisi kukubali kumwacha kisha asafiri kwenda nje ya nchi kwa zaidi ya mwaka. Kudharauliwa kutokana na jinsi yake, maswali yenye chembechembe za uka...

BITEKO ANZISHENI MASHAMBA YA KUKU

Image
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa ujio wa Mkutano wa Jukwaa la Tasnia ya Kuku na ndege wafugwao kwa Nchi za Kusini mwa Afrika unadhihirisha  namna Tanzania chini ya uongozi wa Rais Mhe. Dkt.  Samia ilivyokuwa na mahusiano mazuri ambayo yamefungua milango katika sekta mbalimbali ikiwemo ya tasnia ya kuku na ndege wafugwao. Amesema hayo leo Oktoba 16, 2024 jijini Dar es salaam wakati akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdory Mpango katika ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Tasnia ya Kuku na ndege wafugwao Kusini mwa Afrika. Aidha ametaja faida za ufugaji kuku na ndege wafugwao kuwa ni pamoja na kuchangia usalama wa chakula na kuongeza pato la Taifa kikanda na kimataifa. Amesema kuwa asilimia 55 ya kaya nchini na katika nchi mbalimbali ni ufugaji unaofanywa zaidi na wanawake na vijana na kuwa Tanzania ina kuku milioni 103.1 wakiwemo kuku wa asili na kisasa. Kupitia Jukwaa hilo, Dkt. Biteko ameiagiza ...

MILLION 300 WATAKUWA WANATUMIA NISHATI

Image
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amesema ifikapo mwaka 2030 watu milioni 300 Afrika watakuwa wanatumia nishati safi ya kupikia. Amesema juhudi zinazofanyika katika kufikia lengo hilo zimepelekea Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Benki ya Dunia (WB) kuunga mkono Ajenda ya nishati safi ya kupikia Afrika. Dk Biteko ameyasema hayo alipozungumza katika mkutano wa siku mbili kuhusu majadiliano ya masuala ya nishati kwa Bara la Afrika kwa ngazi ya mawaziri unaofanyika Dar es salaam kwa siku mbili. Amesema AfDB imeichangua Tanzania kufanya mkutano huo wa majadiliano ikiwa Tanzania inazidi kupiga hatua kubwa ya mafanikio katika sekta ya nishati. “Mkutano huu pia ni sehemu ya maandalizi ya mkutano wa marais  wa nchi za Afrika unaotarajiwa kufanyika mwaka 2025 ikiwa ni mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye kinara wa ajenda ya Nishati safi ya kupikia Afrika,” amesema Dk Biteko. Ameongeza kuwa, mkutano huo u...

MSUKE HIVI MWANAO HASIUMIE

Image
Imekuwa ni jambo la kawaida katika jamii zetu kwa sasa, kuona hata watoto wadogo wakiwa katika mitindo mbalimbali ya nywele kichwani bila kujali umri wa watoto wenyewe, je kuna usahihi katika hili? Sio mbaya mtoto kupendeza, lakini unapaswa kuangalia aina ya urembo na mapambo unayomwekea. Kusuka kwa watoto si tatizo kama atakuwa amefikisha umri fulani, lakini tatizo la wazazi unakuta anamsuka mtoto wa miaka miwili au mwaka mmoja bila kujali kama utosi ama ngozi ya kichwa haijakomaa. Wazazi wamekuwa na tabia za kuwasuka watoto wa kike ama kwa hiari au kwa kuwalazimisha, lengo ni kuwapendezesha kimwonekano.Hakuna kipindi ambacho watoto wanaumia kama msimu ambao wazazi wanalazimisha mtoto asuke mtindo ambao unakuwa mgumu, mara nyingi inakuwa mitindo inayosukwa sana na watu wazima. Pamoja na kupata maumivu, pia unamfanya mtoto atumie muda mrefu kukaa. Siyo vizuri kuiga kila tunaloona bila kufuatilia na kubaini athari zinazoweza kutokea, kabla ya kutumia kitu ni vizuri kufanya utafiti na ua...

VILEMBA KINAVYO WATOA BOMBA WADADA

Image
Na Brighiter David  Karibu katika ya mitindo Leo tutaongelea viremba na kofia vinavyoweza kukufanya ukaonekana nadhifu huku ukienda na fashioni. Awali ufungaji wa vilemba ulikuwa ukionekana zaidi misibani, makanisani na mashambani lakini sasa hali imebadilika tofauti na zamani. Unaweza Kufunga kilemba ukaenda sehemu yoyote ile ya heshima hata kwenye mikutano mikubwa na  ukaonekana nadhifu. Kungunga kilemba kwenye shughuli mbalimbali kulitokana na wenzetu wa nchini Nigeria na Congo walivyoamua kuendeleza utamaduni wao huo na kila kukicha kubuni mitindo mipya ya ufungaji wa vilemba. Siyo wote tuna utaalamu wa kufunga vilemba licha ya kuwa tunapenda mtindo huo. Kama tulivyoona Sio wote wenye uwezo wa kufunga vilemba hivi kwa ushadi wenye uwezo wa kufunga vilemba hivi kwa ustadi. Wabunifu wa mitindo mbalimbali walipongeza utaalam kwa kutengeneza kofia za staili mbalimbali ambazo zinafanana na viremba. Ukiangalia kwa haraka unaweza usitambue kama aliye mbele yako amefunga kilemba a...

WANYECHE ATWAA TAJI LINGINE GOFU

Image
MCHEZAJI wa gofu, Enosh Wanyeche ameongeza taji lingine la heshima kwa jina lake, na kutwaa taji la NMB CDF 2024 lililofanyika kwenye mashindano ya Gofu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yaliofanyika Lugalo jijini Dar es Salaam. Mafanikio haya ya ajabu yanakuja wiki moja tu baada ya Wanyeche kutwaa taji la Lina Professional Golfers (PG) Tour Pro-Am katika Klabu ya Moshi Gymkhana mkoani Kilimanjaro. Mashindano hayo ya siku tatu ya shimo 54, yaliyoandaliwa na TPDF Lugalo Club kwa kushirikiana na Chama cha Gofu Tanzania (TGU), yalivutia zaidi ya wachezaji 250 wa kiume na wa kike na wataalamu wa mchezo wa gofu kutoka nchi nzima. Mashindano hayo kitaifa ilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya JWTZ, pia kumuenzi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerali Jacob Mkunda. Enosh alivutia katika mashindano yote alishinda kwa mikwaju miwili, akimaliza kwa jumla ya siku tatu ya mipigo 224.  Raundi zake zilijumuisha 75 katika siku ya ufunguzi, ikifuatiwa na 72 na 77 katika r...

WATANZANIA WATAKIWA KUTUNZA UTALII

Image
 es Salaam Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana amefunga Onesho la Nane la Utalii la Kimataifa la Swahili kwa kuwahimiza  Watanzania  kuzitunza na kuhifadhi rasilimali zilizopo nchini ili kuendelea kukuza Sekta ya Utalii. Balozi Dkt Chana ametoa rai hiyo  Jijini Dar es salaam wakati akifunga Onesho la nane la Utalii la Kimataifa la Swahili ( S!TE) ambalo limefanyika kuanzia Oktoba 11 ,2024 katika Ukumbi wa Mlimani City jijini humo Amesema kuwa utalii na ulinzi wa rasilimali za Nchi yetu ni kipaumbele cha Kila mtanzania,hivyo hakuna budi kuhakikisha kila mtanzania anafanya hivyo ili kukuza sekta ya utalii. Amebainisha kuwa sekta ya Utalii inachangia asilimia 17 za pato la Taifa(DGP),huku ikingiza fedha za kigeni ni asilimia isiyopungua 25,ambazo ni zaidi ya Dola bilion 3. "Tukizungumzia suala la utalii kila mtu ananufaika,kwanza shirika la ndege ATCL linapata abiria wengi wanaokuja kutalii nchini hapa,,pia mtalii anaposhuka anatumia usafiri wa ndani a...

SEKTA YA UTALII IMEPIGA HATUA

Image
 Salaam Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Dastan Kitandula amesema kuwa Sekta ya Utalii imepiga hatua kubwa kutokana na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuipa kipaumbele Sekta hiyo hali inayochangia kukuza uchumi wa nchi.   Ametoa kauli hiyo leo wakati akifungua Mkutano wa Jukwaa la Uwekezaji katika Sekta ya Utalii Nchini Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam,ikiwa ni sehemu ya onesho la 8 la Utalii la Kimataifa la Kiswahili( S!TE) 2024. Amesema kuwa kutokana na uwekezaji mzuri wa miundombinu rafiki katika sekta hiyo,imechangia kwa kiasi kikubwa kuwavutia watalii wengi kutoka mataifa mbalimbali kuja kuwekeza Nchini. Aidha Kitandula  amesema kuwa sekta ya Utalii inaingiza fedha nyingi za kigeni,pamoja na kuchangia kiasi kikubwa katika pato la Taifa( DGP) hivyo Serikali itaendelea kuweka jitihada za msingi katika kuimarisha uwekezaji kwenye sekta hiyo. "Sekta ya Utalii inaingiza fedha za kigeni,inatangaza utamaduni,inatoa ajira ,inachangia ...

KAMPUNI YA PAULHANS YAIPONGEZA SERIKALI

Image
o M Na  Kampuni ya Hanspaul Group imeipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwathamini wawekezaji wa ndani na Sekta binafsi kwani inawawekea mazingira rafiki na wezeshi ya kufanya shughuli zao. Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Satbir Singh Hanspaul katika Ufunguzi wa Onyesho la Nane la Kimataifa ya Utalii (S!TE EXPRO 2024) yanayofanyika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa Serikali imeonyesha nia ya dhati ya kuthamini sekta binafsi kwani imetengeneza mazingira rafiki yanayowafanya wafanye shughuli za uzalishaji kwa tija. " Naishukuru Serikali kwa jinsi inavyothamini sekta binafsi imeweka mazingira rafiki na wawekezaji wa ndani kwa kufanya hivi wawekezaji wataendelea kuongezeka," amesema Hanspaul. Amebainisha kuwa katika kuunga mkono juhudi za Serikali kuhamasisha matumizi ya nishati safi, kampuni hiyo imeleta magari yanayotumia nishati ya umeme katika sekta ya utalii. ...

RAIS MWINYI AFUNGUA MAONYESHO 8 YA SWAHILI MCITY

Image
  Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametoa pongezi kwa juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuimarisha sekta ya utalii nchini. Alisisitiza kwamba idadi ya watalii wa kimataifa wanaotembelea Tanzania imeongezeka kwa kasi, sambamba na ongezeko la mapato kutoka sekta hiyo. Katika hotuba yake iliyotolewa wakati wa ufunguzi wa Onesho la 8 la Utalii la Kimataifa la Swahili (S!TE 2024) , katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, Dkt. Mwinyi alieleza kuwa sekta ya utalii imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uchumi wa nchi. Alitaja takwimu za hivi karibuni zikionyesha kuwa, hadi kufikia mwezi Agosti 2024, Tanzania ilikuwa imepokea watalii 2,026,378, ikiwa ni idadi ya juu kabisa kuwahi kufikiwa katika historia ya nchi. Dkt. Mwinyi amebainisha  kuwa mapato yatokanayo na sekta ya utalii yamefikia Dola za Marekani bilioni 3.5, na sekta hiyo inachangia asilimia 17.2 ya Pato Ghafi la Taifa na asilimi...

HANSPAUL GROUP YANGAA MAONYESHO YA UTALIISWAHILI

Image
MAONESHO   ya Kimataifa ya Utalii ‘Swahili Internation Tourist Export 2024’ yameanza leo Mlimani, Dar es Salaam na yanatarajiwa kutamatika Oktoba 13. Akizungumza Mkurugenzi wa Kampuni ya Hanspaul Group, Satbir Singh Hanspaul ameishukuru serikali kwa kutoa kipaumbele kwa sekta binafsi na kusambaza magari ya utalii kwenye nchi 18 duniani kote. SOMA:  Kila la heri Burundi maonesho ya utalii EAC “Kampuni ya Hanspaul Group imepata nafsi ya kusambaza magari kwenye nchi 19 kutokana na jitahada za serikali. Naahidi kuendelea kushirikiana na serikali na wadau mbalimbali kuongeza uchumi wa nchi kupitia biashara ya kampuni hiyo,”amesema.