LG MOSQUITO AWAY KUFUKUZA MBU
Imebainishwa kuwa uwepo wa teknolojia mpya ya kufukuza mbu Kwa njia ya kiyoyozi itasaidia Kwa kiwango Kikubwa kidhibiti ugonjwa huo ambao umekuwa ni changamoto Kwa nchi zinazoendelea Tanzania ikiwemo.
Serikali inaendelea na Mipango yake ya kupanga mikakati ya namna ya kupambana na ugonjwa wa Malaria na Mbu wanaoeneza Ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha inaweka mfumo mzuri wa namna ya kupambana na malaria ili kuweza kuokoa nguvu kazi ya Taifa na rasilimali zitakazotumika katika kutibu ugongwa huo.
Kauli hiyo imetolewa na Prof Amos Mwakigonja katika katika uzinduzi wa AC yenye teknolojia mpya ya kufukuza mbu Kwa njia ya kiyoyozi iliyobuniwa na kampuni ya LG ambayo inatajwa kuwa na ufanisi mkubwa na rafiki kwa mazingira.
Teknolojia hiyo ya kufukuza mbu Kwa njia ya kiyoyozi itawasaidia wa Tanzania kutokung’atwa na mbu na hivyo Kasi ya watu kupata malaria itapungua na magonjwa yanayoenezwa na mbu pia yatapungua kwa kiasi kikubwa.
Aidha Serikali na wadau wanaendelea kuweka nguvu na nia katika kutokomeza Malaria ifikapo mwaka 2030 ili kuboresha zaidi Afya za Watanzania na hivyo kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa Taifa .
Kwa upande wake Meneja Tanzania Aashim Wadhwa amesema kuwa kampuni LG itasaidia kwa kiasi kikubwa kufukuza na kuondoka wadudu ofisini na majumbani.



Comments
Post a Comment