Posts

Showing posts from May, 2024

HEINEKEN YATANUA WIGO ZAIDI

Image
Heineken yapanua wigo zaidi, Yatangaza uzinduzi wa bidhaa zake mpya mbalimbali kwenye orodha ya jadala lake nchini Tanzania. Kampuni inayoongoza duniani ya vinywaji, Heineken imesherehekea upanuzi wake zaidi wa vinywaji na kutangaza bidhaa mpya ikionyesha orodha za aina mbalimbali za chapa zilizoanzishwa nchini Tanzania katika hafla ya kipekee iliyofanyika jijini Dar es salaam siku ya Jumamosi, Mei 25, 2024. Hii inafuatia kukamilika kwa ununuzi wa kampuni ya Distell Group Holdings Limited (‘Distell’) na Namibia Breweries Limited (‘NBL’).   Waliohudhuria kwenye hafla hiyo ni wageni waalikwa, viongozi wa tasnia na wawakilishi wa vyombo vya habari, pamoja na Mgeni Rasmi, Mhe. Prof. Kitila A.K Mkumbo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji.  Wageni wengine mashuhuri waliuhudhuria katika kuadhimisha hatua hiyo muhimu kwa Kampuni ya Heineken Beverages Tanzania ilipozindua bidhaa zake za kusisimua katika soko la Tanzania. Meneja Mkazi wa Kampuni ya HEINEKEN nchini, Obabi...

HEINEKEN BEVERAGE VINYWAJI VYA KILEO

Image
WAZIRI wa Uwekezaji na Mipango Profesa Kitila Mkumbo amesema kwa Sekta ya Uwekezaji nchini inazidi kuimarika inayofanya kukua kwa maendeleo ya Uchumi. Profesa Kitila ameyasema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi muunganiko wa kampuni ya Bia ya Heineken na kampuni ya Namibia na kuwa Heineken Beverage itahusishwa vinywaji vya Vileo zaidi ya viwili katika hafla hiyo iliyofanyika Serena Hoteli jijini Dar es Salaam Mei 25, 2024. Amesema kuwa kampuni hiyo ilikuwa inatoa mapato ya kodi ya sh.bilioni 11 sasa wanakwenda kutoa mapato ya kodi ya sh.Bilioni 21. Amesema kuwa Sekta ya Uwekezaji inavyokua inakwenda sambasamba na kuongezeka kwa ajira nchini pamoja na biashara. Hata hivyo amesema kuwa Serikali imeweka mikakati ya kuvutia Uwekezaji na ndio inafanya kampuni za nje kuungana na kampuni zilizopo nchini kwetu kutokana na kuwa mazingira mazuri ya Uwekezaji na biashara. Profesa Kitila amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imeweka mikakati ya Uwekezaji ikiwa ni pamoja wadau wote wanaohusika na Uw...

HEINEKEN YASHIRIKIANA NA LEAD FOUNDATION KUREJESHA MISITU

Image
Heineken Tanzania yashirikiana na Lead Foundation ya Kupambana na Mabadiliko ya Tabianchi na Kurejesha MisituDodoma, 11/05/2024.  Katika kukabiliana na ongezeko la athari za mabadiliko ya tabianchi na uharibifu wa mazingira, kampuni ya Heineken Tanzania imeanzisha ushirikiano wa kimkakati na shirika la mazingira la Lead Foundation.  Lengo la ushirikiano huu ni kufanya mipango endelevu ya kurejesha misitu iliyoharibiwa na kulinda mazingira yetu.Meneja wa Kampuni ya Heineken Tanzania, Obabiyi Fagade akizungumza na waandishi mwishoni mwa wiki iliyopita walipotembelea moja ya mradi wa uhifadhi wa mazingira katika Kata ya Mpamantwa, wilayani Bahi. Fogade alisisitiza umuhimu wa ushirikiano huu katika kulinda mazingira na kuhakikisha mustakabali endelevu. Alisisitiza umuhimu wa utulivu wa mazingira katika kusaidia mfumo wa ikolojia na viumbe hai, akisisitiza umuhimu wa kushirikiana na Lead Foundation. "Mazingira ni muhimu kwetu, bila ya uhifadhi wake, shughuli zetu na jumuiya tunazoh...

KAMPUNI YA HEINEKEN YATANGAZA JARIDA JIPYA NCHINI.

Image
  WAZIRI wa nchi,Ofisa ya Rais,Mipango na Uwekezaji,Profesa Kitila Mkumbo,anatarajia kuwa mgeni rasmi wa uzinduzi wa jarida la vinywaji vya heiken linalotarajiwa kufanyika May 25 mwaka huu. Akizungumza na Waandishi habari mapema leo Jijini Dar es Salaam,Meneja Mkazi nchini wa Kampuni ya HEINEKEN,Obabiyi Fagade amesema mbali Waziri Mkumbo katika uzinduzi wanatarajia kuwepo viongozi mshuhuri,viongozi wa tasnia mbalimbali na wawakilishi wa vyombo vya habari kuadhimisha tukio hilo muhimu kwa kinywaji cha Heinek Tanzania. "Ununuzi wa hivi majuzi ambao umeongeza zaidi ya Euro bilioni 1 katika mapato halisi na Euro milioni 150 katika faida ya uendeshaji kwa nyayo zetu na Afrika bila shaka utachangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchuml nchini Tanzania,Tumepewa nafasi ya kipekee sio tu kufikia hadhira pana zaidi kutokana na upanuzi huo,lakini pia kutengeneza nafasi nyingi za kazi na kuwawezesha Watanzania"Amesema Fagade. Hata hivyo Fagade,amesema kwa sasa  Heineken inapatikana katika M...

RAIS DKT SAMIA KUONGOZA MKUTANO WA USALAMA

Image
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza mkutano wa siku mbili wa Baraza la Usalama la Umoja wa Afrika huku Tanzania ikiwa Mwenyekiti wa Baraza hilo kwa mwezi mmoja wote wa May. Akiongea leo Jijini Dar es salaama Waziri wa Mambo ya Nje January Makamba amesema kama Nchi imepewa fursa ya kuandaa kumbukizi ya miaka 20 l tangu Baraza hilo lianzishwe mwaka 2004 na sherehe hizo zitafanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam Amesema Viongozi mbalimbali wa Nchi za Afrika watahudhulia mkutano huo utakaoanza May 24 na 25 huku Rais wa Gambia, Msumbiji, Uganda na Marais wengine wastaafu wa Afrika wakiongozwa na Dkt. Jakaya Kikwete na Chisano wa Msumbiji wakialikwa katika mkutano huo wa Baraza la Amani la Umoja wa Afrika.

WIKI YA AZAKi 2024 YAZINDULIWA KUJIKITA DIRA YA MAENDELEO

Image
  Wananchi wamehimizwa kupaza sauti zao kikamilifu katika kutoa maoni yatakayosaidia upatikanaji bora wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050. Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society (FCS), Justice Rutenge baada ya uzinduzi rasmi wa Wiki ya asasi za kiraia nchini (AZAKi 2024) itakayofanyika jijini Arusha kuanzia Septemba 9 hadi 13, 2024 ambapo zaidi ya washiriki 500 watahusika. Maadhimisho ya wiki hiyo yamebeba kaulimbiu ya "sauti, maono na thamani" ikilenga kuwa, licha ya tofauti ya mitazamo na makundi, bado sauti zetu zinapaswa kuwa kitu kimoja ili kurahisisha mchakato wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050. Ameongeza kuwa, Wiki ya AZAKi  mwaka huu inafanyika mapema Septemba, tofauti na ilivyozoeleka awali kila ifikapo Oktoba tangu kuanzishwa kwake 2018, lengo likiwa ni kuhamasisha wananchi kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa. Kwa upande wake, Meneja wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald, amesema imekuwa rahisi kushiriki...

FCS, VODACOM KUDHAMINI WIKI YA AZAKi

Image
  Shirika la Foundation for ¹Civil Society (FCS) na Vodacom Tanzania Foundation wamesaini mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya shilingi Milioni 150, kwa lengo la kudhamini Wiki ya AZAKi 2024 itakayofanyika mwezi Septemba mwaka huu jijini Arusha. Akizungumza mkoani Dar es Salaam wakati wa hafla ya kusaini mkataba huo Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Justice Rutenge amesema fedha hizo kutoka Vodacom Tanzania Foundation, zimeongeza chachu ya ushirikiano katika kukuza maendeleo ya jamii kupitia Wiki ya AZAKi. Katika kufanikisha Wiki ya AZAKi, FCS wamechangia shilingi Milioni 250 ambapo michango mingine inatoka kwa wadau wa maendeleo zikiwemo asasi za kiraia. Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Foundation Tanzania, Zuweina Farah amesema ili kufanikisha dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, ushirikiano wa pamoja unahitajika kati ya AZAKi, sekta binafsi na Serikali. Kauli mbiu ya Wiki ya AZAKi kwa mwaka huu ni sauti, maono na thamani.

BONGO MUVI STARTIMES YAWAPA NEEMA

Image
  Filamu zaidi ya 120  za wasanii wa Tanzania zimenunuliwa na chanel mpya ya St Swahili Plus chini ya Startimes Media kwa ajili ya kuoneshwa kwa watazamaji. Akizungumza Dar es Salaam juzi kwenye uzinduzi wa chanel hiyo, Mkurugenzi wa Masoko na Maudhui wa Startimes David Malisa alisema hiyo yote ni kuunga mkono juhudi za wasanii katika kazi zao lakini pia,  kuhakikisha wanatoa burudani kwa Watanzania. "Tumeanisha chanel ambayo silimia 60 ya Maudhui yanatoka ndani ya nchi. Tumetoa fursa kwa wasanii kwa kununua kazi zao ili na wao waweze kunufaika lakini pia na watazamaji wetu waburudike, jambo la muhimu tumekuja na kampeni ya kamatia furushi watu walipie vifurushi kuanzia sh 23000 wanufaike,"alisema. Malisa alisema uzinduzi huo umeenda sambamba maudhui mengine ya chaneli nyingine mpya kama ST Toons, ST Toonie, ST Kids Plus, ST movies kwa ajili ya kuonesha vipindi mbalimbali vya tamthili, watoto nafilamu. Mwakilishi wa Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita) Edward Nnko aliwap...

JORDAN AWABARIKI WANAMITINDO

Image
MSHINDI wa shindano la Mr Jordani Frank Dionis Mizambwa amewataka wanamitindo wanaoshiriki katika mashindano ya mitindo kuacha dhana ya kuona mshindi amep angwa. Shindano Hilo ambalo limefanyika hivi karibuni katika chuo cha Jordani kilichopo Morogoro kwa lenye lengo la Kukuza vipaji vya wanafunzi na kutoa frusa mbalimbali chuo Ili hapo. Akizungumza na ukurasa huu amesema wakati wanaelekea fainal kulikuwa na maneno mengi ya kusema mshindi amepangwa jambo ambalo lilimkatisha tamaa ya Kitasa kuacha shindano. “Siku kadhaa Kabla ya kufika fainali nilitaka kuacha kushiriki kwa sababu kulikuwa na tetesi mshindi amepangwa Ila kunarafiki yangu alinitia moyo niendelee huenda ikawa bahati yangu,” anasema Frank Donis Mizambwa Aliongeza kuwa ushindi wake umetokana na jitihada zake hivyo kwa ambao wanataka kutimiza ndoto zao katika tasnia ya mitindo kinachotakiwa ni jitihada na kukubali kufundishwa na kupokea ushauri. Aidha ameahidi kuto wangusha mashabiki zake hususa katika chuo hicho atafanya maj...

NaCONGO KUFANYA UCHAGUZI WA VIONGOZI

Image
Baraza la Taifa la  Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO) limetangaza mchakato wa uchaguzi wa wajumbe na viongozi wa Baraza hilo, utakaofanyika kuanzia Mei 21 hadi Juni 26, 2024. Akizungumza  jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti Kamati ya Mpito ya Kuratibu Uchaguzi wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Christina Kamili Ruhinda,  ameyatangazia Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na umma kwa ujumla kuhusu kuanza kwa mchakato wa Uchaguzi wa Baraza, pamoja na ratiba na taratibu muhimu za kuzingatiwa ili kufanikisha mchakato mzima wa Uchaguzi huo. Ruhinda amebainisha ratiba ya uchaguzi huo, ambapo amesema mchakato wa uchaguzi ngazi ya Wilaya utafanyika kuanzia Tarehe 21 hadi 29 Mei, 2024. Mchakato wa uchaguzi ngazi ya Mkoa utafanyika Tarehe 3 hadi 11 Juni, 2024 na mchakato wa uchaguzi ngazi ya Taifa utafanyika kuanzia Tarehe 14 hadi 26 Juni, 2024. Aidha, Ruhinda ameeleza kuwa, wagombea wa nafasi mbalimbali katika Baraza hilo, sharti wakidhi vigezo ambapo taratibu zot...

DERA NI VAZI LA HESHIMA KWA KINA DADA LINAFANYA MWILI KUWA HURU

Image
  Dera ni vazi la heshima la kina dada linalofanya mwili kuwa huru. Vazi hili huvaliwa sehemu yoyote humfanya mtu kuheshimika na mwanamke kuonekana mstaarabu. Zamani tulizoea kuona madera yakivaliwa na wanawake wa Kiislam tu. Lakini siku hizi mambo yamebadilika na kila mwanamke anavaa na kuonekana kupendeza. Yapo madera ya aina tofauti tofauti kunayakushonwa kwa kutumia kitambaana yapo yanayotoka nchi za kiarabu n ahata Somalia.  Pia kuna madera ya kisomali ambayo ununuliwa Mombasa nchini Kenya. Haya yamepewa jina maarufu kama vijora. Ukienda katika harusi nyingi za kiislamu kijara huwa ndio sare maarufu kwa wadada. Dera huwa alimkatai mtu lakini pia ni vazi la heshima ambalo mwanaume akikuona mwanamke umevaa anakutafsiri kuwa ni mwenye heshima (hunajiheshima) na kama unafaa kuwa mke bora ndani ya familia. Vazi hili halimkatai  mtu si mnene mwembamba mtu mweusi mweupe, mrefu na hata mfupi akivaa anapendeza.

WEMA SITAACHA SANAA HADI NAINGIA KABURINI

Image
Staa wa filamu nchini Wema Sepetu amesema kuwa hawezi kuacha kuigiza sanaa ataibeba mpaka anakufa hata akizeeka ataigiza kama bibi, kipaji kipo kwenye Maisha yake. Kauli hiyo ameisema leo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa anatangaza kuirudisha rasmi tamthilia yake ‘Series ya 'Karma', ambayo ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa miaka kadhaa iliyopia,amesema kuwa watu wengi wanamuuliza kuhusu kuacha Sanaa yake ya uingizaji na kusema hawezi acha hadi hatakapo kufa. “Kumekuwa na maswali mengi kumuhusu muigizaji Wema ya kihoji kuhusu hatma ya career yangu kuwa nimeacha uigizaji baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu kwenye filamu na tamthilia. “Career ya uigizaji inaishi ndani yangu na nitaitumikia hadi kufa kwangu kwani uigizaji hauchagui rika wala umri! Ataninapoendelea hata nikizeeka naweza kuigiza kama mama, shangazi nikiambiwa niigize kama bibi nitaigiza”amesema Wema Sepetu

OMONDI NDANI YA MAISHA YA GIGY

Image
Mchekeshaji kutoka nchini Kenya Erick Omondi ametua nchini kwa ajili ya uzinduzi wa Reality Show ya msanii wa bongo fleva Gift Stanford ‘Gigy Money’ itakayozinduliwa leo Kilimanjaro Hotel jijini Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kupokelewa Erick Omondi amesema kuwa Kenya wanataka Diamond atoe mahari ya Ng’ombe 500 kwa ajili ya kumuoa Tanasha Dona na hawataki pesa. “Kama familia ya tanasha mimi kaka yake tumemwambia Diamond Platnums kuwa anatakiwa kulipia ngombe 500 kwa dada yetu Tanasha ng’ombe nasio pesa hatutaki kabisa.

KITENGE HAKIJAWAI KUMCHUCHA MTU

Image
  Katika ulimwengu wa mitindo ya mavazi ya Afrika, huwezi kukosa mavazi yaliyoshonwa kwa kutumia kitenge. Kitenge kimekuwa ni vazi maalumu linalomtambulisha mwafrika yoyote anapokuwa amevaa mahali popote duniani. Pia kitenge kinaweza kushonwa katika mitindo tofauti na kuvaliwa na watu wote, Watoto hata wakubwa wanawake na wanaume na kuonekana nadhifu machoni pa watu. Kupendeza ni jambo kubwa, ambalo wanamitindo na watu wanaopenda Kwenda na wakati hulizingatia. Kupendeza ni jambo kubwa ambalo wanamitindo na watu wanaopenda kwenda na wakati hupenda kuzingatia. Vazi la kitenge pamoja na kumfanya mvaaji kupendeza na kuvutia lakini pia umletea mvaaji heshima pindi anapovaa vazi hilo na kuingia sehemu yoyote. Vazi hilo linaweza kuvaliwa katika mikutano yoyote mikubwa, sehemu za ibada,kanisani kazini na hata katika sherehe mbalimbali hii ni kutokana na heshima ya kitenge.  Baadhi ya watu maaarufu wanaonekana wanavyotokelezea na vazi la kitenge huku wakijibebea heshima kubwa. Miongoni...

WAREMBO VYUONI WAANZA KUTIFUANA

Image
Wanafunzi wa vyuo watakiwa kujitokeza katika kushiriki shindano la urembo ili kutimiza ndoto zao wakiwa wasomi. Akizungumza na habari leo jijini Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa shindano hilo, Mkurugenzi wa 'The Look ' Kampuni inayoandaa Miss Tanzania, Basilla Mwanukuzi amesema kupitia shindano la Urembo ngazi ya vyuo vikuu  (MISS HIGHER LEARNING)  imekuwa likiacha alama nzuri kwani mara 3 mfululizo limekuwa likitoa washiriki katika ngazi hiyo na kufanikisha Miss Tanzania hadi kufika Miss World . Amesema anatambua kuwa urembo ni uongozi lakini haitoshi kukamilisha sifa za mrembo huyo ni lazima awe na ufahamu mzuri . "Miss Tanzania 2023 ametokea ngazi ya vyuo vikuu hivyo ni kielelezo tosha kuwa Miss Higher Learning inatoa Warembo wasomi ambao wanaandaliwa kuja kusaidia jamii na Taifa kwa ujumla". amesema Pia ameongeza kuwa jukwaa la Miss Tanzania limekuwa ni msaada mkubwa kwa sasa kuwatumia warembo katika nyanja mbalimbali ikiwemo kisiasa,sanaa pamoja na kijamii na...

BASATA WAONGEZA MUDA WASANII KUJISAJILI

Image
Katibu Mtendaji  wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Dk Keedmon Mapana ameongeza muda hadi Mei 30, 2024 kwa wasanii kuhuisha vibali vyao vya kufanya shughuli za sanaa nchini mara baada ya kupokea maombi kutoka kwa marais wa mashirikisho ya sanaa za ufundi, maonesho na muziki nchini Ameyaongea hayo mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Bwana Adrian Nyangamale ameahidi kutoa ushirikiano kwa kutemembelea wanachama wao waweze kutekeleza takwa la kiutaratibu lenye manufaa katika muendelezo wa shughuli za sanaa nchini. Ikumbukwe wiki moja iliyopita Baraza lilitoa tamko lililowataka wasanii kuhuisha vibali vyao ndani ya siku saba kabla ya kuweka hadharani orodha ya wasanii wote ambao vibali vimepitwa na wakati.

TMA WAONGEZA SIKU 5 KUMPELEKA KAZI ZAO

Image
Mwenyekiti wa Tuzo za Muziki Tanzania, David Minja ametoa tamko rasmi la kuongeza muda kwa wanamuziki kuwasilisha kazi zao katika vipengele wanavyotarajia kuwania katika msimu huu. Minja ameweka wazi kuwa wamefikia uamuzi huo kutokana na tatizo la kimtandao ambalo limeathiri mamilioni ya watu katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki, zoezi la uwasilishaji lilitarajiwa kufungwa Mei 12, 2024 saa 5:59 usiku hivyo litaendelea hadi Mei 20, 2024.

GNAKO HANA UTANI KAVUJISHA DUDE LA WEUSI

Image
Gnako hana Utani… hatimaye kaamua kulivujisha Dude la Weusi  Na hii ni baada ya muda wa zaidi ya mwaka kupita bila kupata wimbo mpya kutoka kundi la weusi na tumekuwa tukiwashuhudia wasanii wa kundi hilo wakitoa kazi za mmoja mmoja kitu kilichopelekea Gnako kudai atavujisha wimbo mpya endapo hawatakua Tayari kutoa…  Anasema “WEUSI NILIWAAMBIA DUNIA HAINA MUDA NA MIMI SINA MUDA NDO NALIACHIAAAA HIVYOOO WATAGINI WEUSI WAJE HAPA KINANUKAAA

MWAKA MMOJA WA MEMBE

Image
Ni mwaka mmoja sasa tangu kutokea kifo cha mwanasiasa mkongwe,Bernard Membe ambapo leo familia yake imefanya misa maalum ya kumbukumbu katika Kanisa la Mtakaifu Joseph Jijini Dar es Salaam. Akizungumza mara baada ya Misa hiyo maalum, Mjane wa Marehemu Membe, Dorcas Richard amesema kikubwa anachoomba kwa marafiki wa Membe ni kuendelea umoja, upendo na mshikamano aliowaachia marehemu. “Tarehe rasmi aliyofariki Mzee ni kesho Mei 12, familia ilipanga tufanye misa kijijini alikopumzishwa mzee, lakini kutokana na changamoto za miundombinu na mvua ndio maana tumeamua kuifanya ibada hii hapa St Joseph, lakini na kule kijiji ibada maalum kama hii inaendelea.”amesema Dorcas na kuongeza Amesema “familia tunawashukuru watu wote walioshiriki na sisi katika kipindi chote cha msiba, wamekuwa bega kwa bega na sisi  hadi katika kuandaa misa hii maalum ya mwaka mmoja, tunaomba ushirikiano huu uendelee, upendo, mshikamano uendelee kuwepo kati ya marafiki, ndugu na jamaa,”amesema Aidha, amesema kama f...

DAR CITY WAONGOZA KUFUATILIWA INSTAGRAM TEAM ZA KIKAPU, WAKIWA WANAONGOZA LIGI

Image
  Club ya Dar City @darcitybasketball kwa sasa inaongoza Ligi ya mpira wa kikapu Dar es Salaam inayofahamika kama Basketbol Daresalaam Lig ikiwa na Point 29 wakifuatiwa na timu ya Outsiders ambao na wao wanapoint 29  @darcitybasketball mpaka sasa ndio Timu ya mpira wa kikapu inayoongoza kwa kufuatiliwa kupitia mtandao wa Instagram kutoka Tanzania ikishika nafasi ya 10 katika list ya timu nyingine za kikapu afrika mashariki na kati huku timu kutoka Rwanda zikiongoza Ligi bado Inaendelea ikiwa anamalizia mzunguko wa kwanza kisha wapili kuanza na kuendelea mpaka itakapofika mwezi wa Nane mwaka huu..@darcitybasketball @darcitybasketball

UMOJA WA MABALOZI KUKUTANA MIAKA 61

Image
  UMOJA wa Mabalozi wa Nchi za Afrika wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini wameandaa Maadhimisho ya miaka 61 ya Siku ya Afrika yatakayoadhimishwa matukio makubwa  matatu. Matukio hayo ni Mbio za Mabalozi wa Afrika zikatazofanywa keshokutwa mjini Dar es Salaam na kuwashirikisha mabalozi wa nchi hizo,watumishi wa ofisi za ubalozi,watumishi wa wizara inayowahudumia na wadau wengine. Hayo yalibainishwa jana Dar es Salaam  na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ali Bujiku katika mkutano na waandishi wa habari akiambatana na baadhi ya mabalozi wa nchi hizo. Alisema tukio la pili kati ya matukio hayo matatu ni kutoa msaada kwa shule nne za Dar e Salaam zenye wanafunzi wenye mahitaji maalum na tukio la tatu la maadhimisho hayo ni viongozi hao na wadau wengine kushiriki maonesho ya vyakula vya kiafrika katika Hoteli ya Serena Dar es Salaam Mei, 20 mwaka huu. Balozi Bujiku alisema Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni ‘Kuj...

TCB YAZINDUA KIKOBA KIDIGITAL

Image
TANZANIA Commercial Bank BANK (TCB) imefanya mapinduzi yanayolenga Vikundi vya kuweka na kukopa yaani Vikoba ili kumwezesha wafanyabiashara wadogo wadogo kukopa Kidijitali ndani ya Kikoba kidigitali. Akizungumza wakati wa uzinduzi, huo leo Mei 09, 2024, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TCB Benki, Adamu Mihayo amesema kuwa Kikoba ni zaidi ya fursa ya kidigitali, kwani Kikoba inabeba dhana pana ya uwazi, ujumuishi na usalama katika uwekaji wa akiba na usimamizi bora wa kifedha. Amesema kuwa Maendeleo ya kiteknolojia yanayoyashuhudiwa yamewafanya watu wengi kuwa wajuzi wa mambo ya kidijitali na kuunganishwa pamoja. Hali hii imebadilisha namna wateja wengi wanavyofanya miamala na kutumia huduma za kibenki. "Mabadiliko haya yameisukuma sekta ya kibenki kuwekeza katika teknolojia mbalimbali ili kumpa mteja suluhisho la huduma za kibenki za kuaminika na salama. "Tukitumia nyenzo hi ya teknolojia tunaviwezesha vikundi nchini kote kusimamia mategemeo yao ya kiuchumi, kukua...