Posts

Showing posts from January, 2024

FLAVIANA MATATA FOUNDATION WAJENGA NA KUKABIDHI MATUNDU 12 YA VYOO SHULE YA MANYUNYU

Image
WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imezindua na kukabidhi mradi wa matundu 12 ya vyoo, sehemu ya kunawia mikono, chumba maalumu kwa wanafunzi wenye mahitaji, chumba maalum kwaajili ya wasichana kujisitiri, pamoja na sehemu ya kuchomea taka hususani taulo za kike zilizokwisha kutumika uliotekelezwa na Taasisi ya Flaviana Matata kwa ufadhili wa SEGAL FAMILY FOUNDATION na MFADHILI MWINGINE, katika shule ya sekondari Manyunyu iliyopo mkoani Njombe. Mradi huo utanufaisha jumla ya wanafunzi takribani 910 kila mwaka katika shule ya sekondari Manyunyu na sambamba na hilo miundombinu hiyo itatatua changamoto ya muda mrefu ya uhaba wa vyoo,kichomea taka na upatikanaji wa maji shuleni hapo. Hafla ya Uzinduzi huu imehudhuriwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Flaviana Matata, Bi. Flaviana Matata akiambatana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Njombe akiwemo Mkuu wa Mkoa, DAS , Mkurugenzi wa halmashauri , pamoja na mashirika na wadau mbalimbali ambao wanatekeleza miradi ya maji na usimamizi wa usafi ya...

UDSM NA VIPAUMBELE KUIMARISHA TAFITI KUWA VIWANGO VYA KIMATAIFA

Image
CHUO Kikuu cha Dar es Salaam, Ndaki ya Sayansi za Jamii wameadhimia kufikisha Tafiti zinazofanyika kusikika na kuchapishwa katika majarida ya Kimataifa kwa kuboresha machapisho na kuongeza nguvu katika majarida ya ndani kwa lengo la kuwa na maendeleo endelevu. Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 30,2024 katika kikao kujadili utafiti kuhusu machapisho na kitaaluma katika Vyuo- Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Christine Noe amesema ni vizuri kuzipatia thamani tafiti zinazofanywa nchini,kwa kuweka mazingira ya kuzipandisha katika viwango vya kimataifa katika majarida ya ndani. "Kila kitu unachokiona cha kimataifa kimeanzia katika mataifa fulani, kwahiyo na sisi tunachojifunza kikubwa ni vizuri kukipa thamani ya Kimataifa vitu na tafiti, kama tutaboresha machapisho yetu na tukipandisha majarida yetu kimataifa italeta sifa kwa nchi". Amesema Prof. Noe. Aidha Prof. Noe ameeleza kuwa majarida ya ndani yasi...

JAPAN PARTNERING WITH UNFPA TO SUPPORT MATERNAL HEALTH SERVICES IN KIGOMA

Image
  The Embassy of Japan in Tanzania and UNFPA, the United Nations sexual and reproductive health agency, today signed a funding agreement for support to sustain life-saving interventions to prevent maternal  death in Nyarugusu and Nduta refugees camps in Kasulu and Kibondo districts respectively as well as the host communities of the Kigoma region. The signed agreement allocates USD 359,964 (Equivalent to TZS 921,000,000) to supply reproductive health commodities in the refugee camps and the host community over 2024. Additionally, funds will procure essential medical equipment and train frontline health workers to ensure the delivery of quality sexual and reproductive health services. Over 113,000 individuals, encompassing women, adolescent girls and boys, first-time young mothers, among others, stand to benefit from this new partnership between Japan and UNFPA. At the signing ceremony in Dar es Salaam, His Excellency Mr. Yasushi Misawa, Japan’s Ambassador to Tanzania, emphasis...

BANKI YA CRDB IMEZINDUA MSIMU WA TATU WA SIMBANKING

Image
Katika jitihada zake za kuhamasisha  matumizi ya mifumo ya kidijitali nchini, Benki ya CRDB imezindua msimu wa tatu wa kampeni ya ‘Benki ni SimBanking’ na kutenga jumla ya zawadi zenye thamani ya Shilingi milioni 470 mamilioni kwa wateja wake mwaka huu. Akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Wateja wadogo na wakati wa Benki ya CRDB, Bonaventure Paul amesema lengo la kampeni hiyo ni kujenga utamaduni wa matumizi ya kidijitali katika huduma za kifedha ili kuendana na kasi ya maendeleo na kuondokana na matumizi ya fedha taslimu. “Maendeleo ya sayansi na teknolojia yanaihamisha dunia kutoka kwenye miamala ya fedha taslimu kwenda ile isiyohusisha fedha taslimu yaani cashless economy. Tanzania hatupaswi kuachwa nyuma, ni lazima twende na mabadiliko hayo tena kwa kasi inayostahili,” amesema Bonaventure. Kushiriki na kujiwekea nafasi ya ushindi katika kampeni hiyo mteja anatakiwa kutumia SimBanking kufanya miamala yake yote ya kibenki ikiwamo kulipia ankara za maji, ume...

MWAKA WA UBUNIFU NA UENDELEVU KWA SBL

Image
2023: Mwaka wa ubunifu na uendelevu kwa SBL Katika harakati za kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja, Serikali imedhamiria kupambana na umasikini kwa kujenga Uchumi wa Kiushindani wa Viwanda. Serikali imeweka jitihada za makusudi kwa kuanzisha Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano FYDP III (2021/22 – 2025/26). Mpango huo pia unatambua umuhimu wa sekta zingine katika kuleta maendeleo kama kudumisha utawala bora, elimu, maji safi na salama, pamoja na kuunda uchumi thabiti na wa ushindani. Kushughulikia utofauti wa mapato na matumizi katika jamii kunatambulika kama kipengele muhimu katika kufikia malengo yaliyoainishwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa. Mnamo 2023, kampuni ya Serengeti Breweries Limited iliimarisha zaidi dhamira yake ya kusaidia FYDP III(2021/22 - 2025/26). Wakazi 2,000 wa Mkoa wa Pwani wamepata maji safi Programu ya maji safi na salma kutoka SBL imekuwa na matokeo makubwa baada ya kujenga bwawa la usambazaji maji katika Wilaya ya Handeni, Mkoa wa Tanga, Tanzan...

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

Image
Kuelekea Tamasha la Pasaka mwaka 2024 Alex Msama Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion mwaandaaji wa Tamasha hilo amethibitisha waimbaji wa muziki wa injili kutoka mataifa  zaidi ya 8 watakuwepo kwenye Tamasha la Pasaka la mwaka huu. Akizungumza na waandishi wa habari Alex Msama kuwa maandalizi makubwa kuelekea Tamasha hilo yamekwisha fanyika kwa asilimia kubwa na watu wakae mkao wa kula kwani Tamasha la mwaka huu litakuwa na zuri na lenye shangwe kubwa sana kwa wakazi wa mkoa wa Dar es salaam. Tamasha la mwaka huu litafanyika siku ya Jumapili ya Pasaka, huku kauli mbiu ikiwa ni ASANTE MUNGU KWA KUTUPA RAIS SAMIA S HASSAN MCHAPA KAZI

FAMILIA KUMKUMBUKA KOMBA KIVINGINE

Image
Katika kumuenzi aliyekuwa muimbaji na mtunzi mahiri wa nyimbo za kijamii na kisiasa Captain John Damiano Komba familia imeandaa mkakati maalum kumuenzi Captain Komba Wakizungumza na waandishi wa habari wawakilishi wa familia ya Captain Komba wamesema mara nyingi hufanya kumbukizi ya kumuenzi Captain kila mwaka lakini kwa mwaka 2024 wangependa kuwa tofauti ambapo mwaka huu wamedhamiria kuungana na Rais Samia pamoja na Serikali kusapoti matibabu ya watoto wanaosumbuliwa na ugonjwa wa moyo na kujenga Makumbusho ya Captain Komba (Museum)

RAZACK AONDOKA NA MILIONI 30 ZA BSS NA KIWANJA

Image
Msimu wa 14 wa BSS ulikuwa safari ya kusisimua yenye mshangao na vipaji vya kipekee. Licha ya ushindani mkubwa, Razack Adam kutoka Arusha alijitokeza kama nguzo imara ya ujuzi wa muziki. Sauti yake yenye nguvu na uwasilishaji wa kuvutia uliteka hisia za majaji na mashabiki kwa pamoja. Razack amefanikiwa kuondoka na taji la ushindi pamoja na zawadi nono ya TZS milioni 30 baada ya kuingia tatu bora na King David pamoja na Frank, kisha fainali na King David   aliyeshika nafasi ya pili msimu huu. Kwa kutwaa ushindi huo, Razack Adam ameandika historia kwa kuwa mshindi wa kwanza wa BSS kuwakilisha mkoa wa Arusha, akiacha alama yake kwenye muziki na kuinua heshima ya eneo lake. Jukwaa hili la Bongo Star Search (BSS) , limeendelea kujizolea umaarufu mkubwa kwa kuchangia katika kuimarisha ujuzi na kuibua vipaji vya muziki kutoka maeneo tofauti ya Tanzania.

BOOMPLAY YAPELEKA VIBE VYUONI

Image
Boom Play Tanzania awameungana na Itel  kuwaunganisha pamoja Wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salam (UDSM) na Chuo Kikuu cha ARDHI na wapenda burudani wengine kupitia Power Up Your Life: Music Festival ambayo pia imejumuisha maonesho ya bidhaa mbalimbali kuanzia Marchi 3 viwanja vya mabibo hostel mwaka huu. Tamasha hili kubwa la muziki litafanyika siku ya kilele cha maonesho ya bidhaa viwanja vya UDSM - Mabibo Hostel, Jumamosi, Februari 3, 2024. Huku Wasanii maarufu Bongo kama Barnaba, Meja Kunta, Kontawa, Platform, Lony Bway, Lody Music, na wengine wengi watakuwa jukwaani kutoa burudani ya kipekee.

TAMASHA LA PASAKA KUANZA DAR

Image
Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion Alex Msama ametangaza Tamasha la Pasaka mwaka 2024  linatarajia kuanza kufanyika katika mkoa wa Dar es Salaam siku ya Pasaka Machi 31 mwaka huu Waimbaji mbali mbali wa muziki wa Injili watashiriki katika  Tamasha hili kubwa la Pasaka kwa mwaka 2024. Maandalizi makubwa yanaendelea kufanyika, na Tamasha la mwaka huu limekuja na kauli mbiu inayosema "  ASANTE MUNGU KWA KUTUPA RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN MCHAPA KAZI.

WAKAMATWA WAKISAFIRISHA BANGI

Image
  Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limefanikiwa kukamata gari ndogo aina ya Noah yenye namba za usajiri T 777 CBC  ikiwa inasafirisha  na magunia Kumi yakiwa na dawa za Kulevya aina ya Bhangi. Gari hiyo imekamatwa katika eneo la Kijiji cha Chamgata Kata ya Kalemela Wilaya ya Busega mkoani Simiyu. Dereva wa gari hilo alitelekeza gari hiyo pembezoni mwa barabara ya Mwanza - Musoma na kutokomea kusikojulikana na jitihada za kumtafuta bado zinaendelea.

TGNP YAENDESHA MAFUNZO YA UONGOZI KIJINSIA

Image
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) unaendesha programu ya mafunzo ya siku kumi kuhusu masuala ya uongozi wa kijinsia, lengo likiwa ni kuwawezesha wanajamii kuthamini nguvu za pamoja na kushirikisha wanawake katika nafasi za maamuzi kama sehemu ya mabadiliko katika jamii na kuwainua kiuchumi. Washiriki kutoka nchi mbalimbali za Afrika, ikiwa ni pamoja na Kenya, Uganda, Zimbabwe, Rwanda, Ghana, Burundi, Afrika Kusini, na Nigeria, wamejumuishwa katika mafunzo haya ya uongozi wa kijinsia, yakilenga kukuza mazingira ya kujifunza yenye ufanisi na ushirikiano. Anna Sangai, Afisa wa Programu ya Mafunzo wa TGNP, ameeleza , kwamba washiriki wamejifunza jinsi jamii inavyoweza kuenzi nguvu za pamoja na kushirikisha wanawake katika nafasi za maamuzi.  Aidha, washiriki walitembelea Kituo cha Taarifa na Maarifa huko Kipunguni kwa lengo la kuelewa jinsi wanawake wanavyojiwezesha kuleta mabadiliko katika jamii, hususan katika kukabiliana na ukatili wa kijinsia, mimba za utotoni, unyanyasaji wa kimwi...

BASHUNGWA ATAKA WATU KUPANDA MITI

Image
 Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameuagiza Wakala wa Barabara (TANROADS) kuendelea kupanda na kuhudumia miti iliyopandwa katika maeneo ya barabara kwa ajili ya kuendelea kupendezesha miji na kutunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Bashungwa amezungumza hayo katika Ofisi za Wizara zilizopo katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma leo Januari 29, 2024 wakati akiongoza zoezi la upandaji miti kwa ajili ya kuendeleza kampeni ya upandaji miti iliyozinduliwa na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango. Aidha,ameitaka TANROADS kuhakikisha inaendelea kuhudumia miti walioipanda katika barabara ya Chimwaga - St. Peter Claver (km 10), jijini Dodoma na kuwasisitiza kurudishia miti iliyokufa ili kuendelea kuboresha na kupendezesha eneo hilo. “Hakikisheni TANROADS mnaihudumia miti mliyoipanda katika barabara ya Chimwaga - St. Peter Claver (km 10), mnaiangalia kwa ukaribu na kupanda miti mipya kwa ile iliyokufa kama mlivyoelekezwa na Makamu wa Rais Dk Philip Mpango”, amese...

TARURA KUANA KUJENGAMBEYA BRIDGE

Image
Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) inatarajia kuanza usanifu wa daraja la kudumu la chuma (Mabey Bridge) litakalojengwa ili kuunganisha vijiji vya Nyali na Nzumbo katika kata ya Ulaya-Mikumi Wilayani Kilosa. Hayo yameelezwa  Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff wakati akiongea na wananchi wa kata hiyo kwenye ziara yake ya kikazi ya kukagua hali ya miundombinu wilayani Kilosa. “Nitawatuma wataalamu wangu wa TARURA Makao Makuu waje wafanye usanifu wa ujenzi wa daraja la kudumu la chuma ili kuunganisha vijiji hivi vya Nyali na Nzumbo”. amesema Seff  Pamoja na hilo, amemwelekeza Meneja wa TARURA Mkoa wa Morogoro kuanza mara moja ujenzi wa daraja la watembea kwa miguu (Kiteputepu) ili wananchi wa vijiji hivyo waendelee kupata huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi. Vile vile Mhandisi Seff ameelekeza kufanyika kwa tathimini ya uharibifu wa barabara za Mikumi  ili ziwekwe kwenye mpango wa dharura wa kurudisha mawasiliano haraka iwezekanavyo. Awali, Mbung...

SADCAS YATHIBITISHA MAABARA 4 TBS

Image
TAASISI ya Ithibati ya Jumuiya ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADCAS) imethibitisha na kuzipatia vyeti vya umahiri maabara nane za Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Akizungumza na HabariLeo leo Januari 25, 2024 jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Ithibati ya Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika ( SADCAS), Eva Christine Gadzikwa amesema vyeti hivyo vya umahiri vilivyotolewa na hatua nzuri kwa Tanzania ambayo inathihirisha kuwa maabara hizo zinaendelea kukubalika popote duniani jambo linaongeza chachu katika uwezeshaji biashara ndani na nje ya nchi. Amesema, maabara hizo nane zitaendelea kusaidia na kurahisisha biashara kwani majibu ya maabara hizo yataweza kukubalika na kutumika popote duniani. "Hakuna haja tena ya kupima bidhaa zilizoidhinishwa hapa Tanzania zitakaposafirishwa nje ya nchi ambapo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuokoa muda na kulinda wateja". Amesema Christine Ne, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) David Ndibalema amesema kuwa...

MAVUNDE AONGOZA MKUTANO CHAMA CHA MIGODI

Image
WAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde ameongoza mkutano maalum baina ya Serikali na Chama cha Migodi Tanzania, ambapo wadau wote wa sekta ya madini wamekutana kujiandaa kwa maonesho yatakayofanyika mjini Cape Town, Afrika Kusini. Madhumuni ya mkutano huo ni kuiwakilisha Tanzania kwenye jukwaa la kimataifa na kuvuta uwekezaji, hususan katika maeneo ya utafiti, na kuongeza ushiriki wa Watanzania katika huduma na usambazaji wa bidhaa mbalimbali. Waziri Mavunde amesisitiza umuhimu wa sauti moja kati ya Serikali na sekta binafsi katika kuitangaza nchi nakuonyesha matumaini kuwa fursa hii italeta uwekezaji mkubwa, kuongeza ajira kwa Watanzania, na kuchangia katika kuongeza mapato ya taifa. Hii ni mara ya kwanza kwa Serikali na sekta binafsi kukaa chini pamoja kwenye mkutano wa namna hii, na inaashiria hatua muhimu kuelekea ushirikiano wenye tija.  

MO DEWJI AKIMBIZAUTAJIRI AFRIKA MASHARIKI KASHIKA NAFASI 20

Image
Dar es Salaam. Jarida la Forbes limemtaja mfanyabiashara Mtanzania, Mohammed Dewji (Mo) kuwa miongoni mwa matajiri vijana zaidi katika kipindi cha miaka 10 mfululizo akishika nafasi ya 12 Afrika mwaka 2024. Tajiri huyo kijana ameajiri zaidi ya watu 40,000 katika kampuni na biashara anazoziongoza na kuzimiliki. Mo ambaye ni mmiliki wa biashara mbalimbali Afrika na duniani kwa ujumla ikiwemo kampuni ya Mohamed Enterprises Limited (MeTL) ametajwa na jarida hilo kupanda katika nafasi za utajiri afrika kutoka 15 hadi 12. Aidha jarida hilo maarufu na la kuaminika kwa upande wa habari za utajiri wa watu duniani limesema utajiri wa Mo umepanda kutoka Dola za Marekani 1.5 bilioni (Sh3.77 trilioni) mwaka uliopita hadi Dola 1.8 bilioni (Sh4.52 trilioni). Kulingana na takwimu hizo Mo anakuwa tajiri namba moja Afrika Mashariki. Pia jarida hilo limemtaja Mo kuwa bilionea pekee aliyetia saini ahadi ya kutoa angalau nusu ya utajiri wake kwa ajili ya misaada mwaka 2016. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa kwa ...

BENKI YA NMB YAZIPIGA JEKI SHULE SITA MKOANI RUVUMA

Image
BENKI ya NMB imekabidhi madawati yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 25 kwa shule sita mkoani Ruvuma ikiwa ni utekelezaji wa dhamira ya benki hiyo ya kuchangia uboreshaji wa sekta ya elimu nchini. Shule zilizonufaika na msaada huo ni pamoja na shule za msingi Kiburangoma, legele, lipuma Londoni na Mkuzo za Manisapaa ya Songea pamoja na Shule ya Msingi Mateteleka ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.   Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika Shule ya Msingi Kiburangoma jana, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kusini Faraja Ng’ingo alibainisha kuwa msaada huo pamoja na kuboresha mazingira ya wanafunzi kujisomea unalenga kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha sekta ya Elimu.   Ng’ingo alibainisha kuwa Sekta ya Elimu ni miongoni mwa vipaumbele vya benki hiyo katika mkakati wake kabambe wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSI) huku akisisitiza kuwa ni Benki ya NMB itaendela kushirikiana na wadau wote ikiwemo Serikali katika kutat...

BENKI YA CRDB YAZINDUA AKAUNTI YA 'HODARI' KWA WAJASIRIAMALI 'TUPO MTAANI KWAKO'

Image
Benki ya CRDB leo imezindua akaunti ya wajasiriamali iliyopewa jina la “Hodari,” ikiwa na lengo la kuwasaidia wajasiriamali katika sekta mbalimbali nchini kuboresha biashara zao. Uzinduzi wa akaunti hiyo umeenda sambamba na uzinduzi wa msimu wa pili wa kampeni ya “Tupo Mtaani Kwako” inayolenga kuhamasisha matumizi ya huduma za benki pamoja na kuwapa Watanzania elimu ya fedha na uwekezaji. Akizungumza katika uzinduzi huo ambao ulifanyika katika viwanja vya Mbagala Zakhiem jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile alisema akaunti hiyo ya “Hodari” itakwenda kusaidia kurahisisha biashara za wajasiriamali kwa kuwawezesha kuweka akiba kwa urahisi, kupokea malipo kidijitali kupitia CRDB Lipa Namba na kuunganisha na fursa za uwezeshaji kupitia mikopo ya wajasiriamali. Bruce alisema pamoja na kuboresha biashara za wajasiriamali, akaunti hiyo pia inakwenda kuleta unafuu mkubwa kwao kwani wateja hawata tozwa makato yoyote kwa miamala ambayo itafanyika ndani ya ...