TECNO NA AIRTEL BUSTI KIPAJI KWA WENYE UHITAJI

Kampuni ya uzalishaji na uuzaji wa simu ya Tecno kwa kushirikiana na airtel Tanzania imezindua kampeni ya Busti kipaji inayolenga kutoa watoto wenye uhitaji na na wenye vipaji vya kucheza mpira kwa kuwapatia viatu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkufunzi wa Kampuni ya TECNo Shakila Mkima  amesema kuwa anayetaka kuchangia atachangia kwa kununua simu ya TECNO Spack 20 moja utakuwa umemsaidia mtoto mmoja.



Amesema kuwa uzinduzi wa kampeni hii ni muendelezo wa dhamira ya TECNO katika kuleta athari chanya kwa jamii ya watanzania.

"Wadau na mashirika mbalimbali kuunga mkono kwa dhati juhudi hii, akisema kwamba pamoja, tunaweza kuleta tofauti kubwa katika maisha ya watoto wenye vipaji nchini."

Aidha Shakira amewekawazi kuwa kampuni yaTECNO inawaalika watu wote

kujiunga na kampeni hii kwa kununua simu mpya yaTECNO SPARK 20,ambapo kwa

kila ununuzi, TECNO itatoa viatu vya michezo kwa mtoto mwenye uhitaji.

"Juhudi hii ya ushirikiano unalenga kuwa wezesha kizazi cha vijana ,kukuza ndoto na matarajio yao

kupitia furaha ya michezo."amesema 



"Kwa kutambua hamasa kubwa iliyopo kwenye michezo kwa sasa, TECNO leo tuna watambulisha rasmi maafisa habari wa Simba Sports Club Ahmed Ally na msemaji wa timu ya Young Sports Club, Ally Kamwe kuendesha kampeni hii ya busti kipaji kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu."amesema

Kwa upande wake Afisa habari wa Simba Sports Club, Ahmed Ally amesema kuwa watoto wengi wanashindwa kutimiza ndoto zao kutokana na kukosa viatu na vifaa vya kuchezea mpira hata wakipata wanakuwa wanashindwa kutumia kutoka na kuzoea kucheza bila viatu hivyo wanapaswa kupewa hili waweze kuvifanyia mazoezi viatu na wavizoee.

"Wadau na mashirika mbalimbali kuunga mkono kwa dhati juhudi hii, kwa  pamoja, tunaweza

kuleta tofauti kubwa katika maisha ya watoto wenye vipaji nchini."

"Mfano mzuri ni Ally Kamwe alikuwa akijakucheza mpira ukimpa viatu anashindwa kucheza kwa sababu hajazoea kucheza na mpira na viatu akawa anashindwa hadi alipofanya mazoezi kwa kutumia viatu akawa anafanya vizuri."amesema Ahmed 

Naye Ally Kamwe amesema kuwa ni vizuri kusaidia watoto waweze kutimiza ndoto zao kupitia vipaji vyao kwa kuwa mpira wa miguu ni mchezo namba moja duniani unaoweza kubadilisha maisha ya mtu.

"Ninasababu kubwa kuwapasapoti watoto kuweza kutimiza ndoto zao kama shabiki wa timu yoyote na unapenda kuona vipaji vipya unaweza kusaidia watoto kupitia vipaji vyao kwa kununua simu moja utakuwa umemsaidia mtoto mmoja mwenye uhitaji kupata kiatu cha kuchezea mpira."amesema Ally Kamwe

Pia ameongeza kuwa mtoto wa mwenzio ni wako anauhitaji mpende mthamini akuze kipaji chake kwa kumpatia kiatu cha michezo.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA