KIKWETE MGENI RASMI MIAKA 50 YA CHUO CHA MAJI
Rais wa awamu ya nne wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, anatarajia kuwa Mgeni rasmi katika mahadhimisho ya miaka 50 ya Chuo Cha Maji, Januari 31 hadi Februari 2 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa chuo hicho, Dkt Adam Kalia amesema kuwa maadhimisho hayo yatahudhuliwa na wageni kutoka nchi mbalimbali.
Chuo cha maji kuadhimisha miaka 50 ya chuo hicho tangu kuanziahwa kwake na kusherekea mafanikio waliopata kupitia Chuo hicho tangu kuanzishwa kwake na kuleta mafanikia makubwa kwenye wizara ya maji.
Mahadhimisho hayo yatafanyika kwa siku tatu mfululizo Januari 31 hadi Februari 2 .

Comments
Post a Comment