PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU
Wanandoa watashauriwa kuwa na mitoko ya pamoja kujua mwenzio anapenda kula nini kuvaa na kunywa ili kuendelea kudumisha ndoa yao, Ndoa bora ni ushirikiano, siyo mashindano.
Akizungumza mwaandaaji wa Usiku huo wa wanandoa The Pinnacle of Mentorship & Excellence Award (PIMEA) Dkt Christine Mbelwa amesema Lengo la Usiku wa Wanandoa nikuwakutanisha na kubadilishana mawazo kuhusiana na kukumbusha baadhi ya mambo ya ndoa.
"Moja ya majukumu ambayo Mungu amenikabidhi mimi pamoja na mume wangu ni kujenga ndoa na mahusiano imara kupitia uandishi wa vitabu, semina, makongamano na mafundisho mbalimbali.
"Usiku wa Wanandoa ni moja ya jukwaa kuu tunalotumia kwa lengo la kuboresha, kuponya na kuokoa ndoa. Tunawakusanya wanandoa pamoja, kuwapa mafundisho ya vitendo ana kwa ana, kuruhusu maswali na kutoa majibu ya moja kwa moja.
Amesema Zaidi ya mafundisho, wanandoa hupata nafasi ya kufurahi pamoja kwa kushiriki vinywaji, michezo na burudani mbalimbali. Shughuli hizi huleta uponyaji wa kihisia, furaha na mshikamano mpya katika mahusiano.
"Kwa njia hii, tunalenga kuimarisha afya ya ndoa na familia kwa ujumla, kuwapa wanandoa nafasi ya kujifunza, kushirikiana na kujenga mshikamano wa kifamilia na kiroho. Hatimaye, tunatarajia kuona migogoro ikipungua na ndoa zenye heshima na upendo zikijengeka.
Aidha amesema Historia na Mwendelezo wa Usiku wa Wanandoa, Tumekuwa tukiendesha Usiku wa Wanandoa kwa zaidi ya miaka kumi, ndani na nje ya nchi, na tumeshuhudia matokeo makubwa katika maisha ya waliohudhuria.
"Kwa kawaida, tukio hili hufanyika mara nne hadi sita kwa mwaka, ndani na nje ya kanisa, hasa kwa ajili ya kuwagusa kwa karibu wale ambao ni washiriki na wafuasi wetu wa karibu.
"Mbali na mikusanyiko hii mikuu, tunakuwa pia na semina ndogo na mikutano ya wanandoa mara mbili au tatu kwa mwaka. Hii ni kwa sababu tunaamini ndoa si tukio la siku moja, bali ni safari endelevu inayohitaji mwendelezo wa mafunzo na msaada wa kila hatua.
Ameongeza kuwa Hali za Ndoa kwa Sasa
Kupitia semina, makongamano na mafundisho mbalimbali ya mahusiano na ndoa, tumeshuhudia mabadiliko makubwa katika maisha ya wanandoa. Ndani ya kanisa, migogoro mingi ya kifamilia imepungua au kuisha kabisa, na badala yake amani, umoja na ushirikiano umeimarika kwa kiwango kikubwa.
"Kila mwezi tunapokea ushuhuda mwingi wa marejesho ya ndoa zilizokuwa zikiyumba, maendeleo mapya na ufanisi wa kifamilia. Hali hii imetutia moyo kuimarisha zaidi huduma za ushauri nasaha, mafundisho na maombi, ili kuendelea kushuhudia mabadiliko chanya: wanandoa wakipata faraja, maelewano mapya na mshikamano wa kudumu.
"Sababu Kubwa za Migogoro ya Ndoa,
Takwimu na uzoefu wa huduma zinaonyesha kwamba sababu kuu za migogoro ya ndoa ni:
Mawasiliano duni – wanandoa kushindwa kuzungumza kwa uwazi juu ya mambo yanayowasumbua.
"Changamoto za kifedha – tofauti za matumizi, mipango isiyo wazi, na shinikizo la kipato.Ukosefu wa uaminifu – kutoka nje ya ndoa au kuvunja makubaliano ya ndani.
"Mara nyingi matatizo haya huanza kidogo, lakini yakiachwa hukua na kuleta mgawanyiko mkubwa. Hata hivyo, tunaamini kuwa kwa msaada wa mafunzo, mshirikiano na sala, suluhisho linawezekana.
Kwanini Watu Wengi Hawadumu Kwenye Ndoa?Kuna sababu nyingi zinazochangia ndoa nyingi kushindwa kudumu, ikiwemo:
Kukosa maandalizi ya msingi kabla ya kuingia kwenye ndoa, na hata ndani yake. Wengi huanza safari ya ndoa bila maandalizi ya kiroho, kifamilia na kisaikolojia.
Kukimbia matatizo badala ya kuyashughulikia.
Ukosefu wa elimu ya ndoa – hali inayosababisha wanandoa washindwe kuwajibika na kutatua changamoto.
Mmomonyoko wa maadili na tabia katika kizazi chetu.
Kukosa hofu ya Mungu na kutopuuzia misingi ya kidini.
Tunashauri wanandoa na vijana wanaotarajia ndoa kuhakikisha misingi yao inajengwa juu ya imani, uwazi, elimu ya ndoa, na kujitolea kwa dhati.
Uzoefu Binafsi wa Ndoa
Ndoa yangu ina zaidi ya miaka 23, na nimepata nafasi ya kujifunza kupitia maisha yangu binafsi pamoja na masomo kutoka kwa walimu wabobezi wa ndoa. Uzoefu huo unanifundisha kwamba ujinga, mitazamo mibaya, tabia zisizojenga, kutowajibika, na ukosefu wa hofu ya Mungu ni sumu katika ndoa.
Ushauri wangu kwa wanandoa:
Tangulizeni Mungu katika kila jambo.
Tafuteni elimu na maarifa ya ndoa.
Jengeni tabia njema zinazoweza kubeba ndoa.
Kuweni wawazi katika fedha, kazi na matatizo. Fedha zisipangiwe kwa siri bali kwa mshirikiano; kazi zijulikane ratiba na changamoto zake; matatizo yashirikishwe mapema kabla hayajawa makubwa.
Ndoa bora ni ushirikiano, siyo mashindano.










Comments
Post a Comment