Posts

Showing posts from March, 2026

ASILIMIA 39.5 YA WANAWAKE WAATHIRIKA WA UKATILI; SERIKALI YATAHADHARISHA HATARI YA UKATILI WA KIDIJITALI

Image
DAR ES SALAAM: Serikali imesema ukatili wa kijinsia unaendelea kuwa moja ya changamoto kubwa za haki za binadamu nchini, huku takwimu za kitaifa zikionesha kuwa asilimia 39.5 ya wanawake wenye umri kati ya miaka 15 hadi 49 wamewahi kukumbwa na ukatili wa aina mbalimbali, ikiwemo wa kimwili, kihisia na kingono kutoka kwa wenza wao. Aidha, wadau wameitaka jamii kuimarisha usalama wa kidijitali na kushughulikia ukatili wa kijinsia unaowezeshwa na teknolojia (TFGBV), ili kuruhusu wanawake na wasichana kushiriki kikamilifu katika elimu, fursa za kiuchumi, uongozi na maisha ya kiraia. Akizungumza jijini Dar es Salaam katika mkutano wa kitaifa kuhusu viashiria vya ukatili wa kijinsia vinavyofanyika kupitia teknolojia (TFGBV), Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watu wenye Ulemavu Zanzibar, Abeda Rashid Abdallah, amesema kuwa tatizo hilo linaongezeka kwa kasi na linahitaji hatua za haraka. Mkutano huo umeandaliwa na Shirika la Kimataifa la Idadi ya Watu ...

ATIKI KUIPIGANIA DAR CITY

Image
PRETORIA, Afrika Kusini: DAR CITY itaanza rasmi safari yake ya kusaka mafanikio kwenye michuano ya Basketball Africa League (BAL) Kalahari Conference kesho, itakapomenyana na Johannesburg Giants nchini Afrika Kusini. Mabingwa hao wa Tanzania wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa wamejipanga kuonesha ushindani mkubwa, huku wakiimarisha kikosi chao kwa kusajili wachezaji wenye uzoefu wa kimataifa. Katika kujiandaa na michuano hiyo, Dar City imemtambulisha rasmi mchezaji wa kikapu wa Tanzania, Atiki Ally, ambaye kwa sasa anacheza kikapu cha kulipwa akiwa na klabu ya New Mexico nchini Marekani. Atiki, ambaye kwa muda mrefu ameishi Marekani, aliwahi kupata ufadhili wa kusoma na kucheza mpira wa kikapu huko, jambo lililomjengea uzoefu mkubwa wa kimataifa unaotarajiwa kuwa msaada kwa Dar City katika mashindano hayo. Mbali na Atiki, Dar City pia imeongeza nguvu kwa kuwasajili mastaa wengine wa kimataifa kwa ajili ya BAL Kalahari Conference, akiwemo David Michineau anayetokea AS Monaco...

CRDB YATOA BILIONI 2.3 KWA WATEJA KUPITIA KAMPENI YA SIMBANKING

Image
CRDB Yatoa Bilioni 2.3 kwa Wateja Kupitia Kampeni ya SimBanking DAR ES SALAAM Benki ya CRDB imetenga jumla ya shilingi bilioni 2.3 kwa ajili ya zawadi kwa wateja wake watakaofanya miamala na malipo kupitia huduma ya SimBanking, ikiwa ni sehemu ya kampeni maalum ya kuhamasisha matumizi ya huduma za kifedha za kidijitali. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya SimBanking Kimpango Wako, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo, amesema kuwa katika kampeni hiyo mshindi wa kwanza wa droo ya mwisho atajipatia shilingi milioni 30, huku mshindi wa pili akipata milioni 20 na wa tatu milioni 10. Amesema mbali na fedha taslimu, washindi wengine watajishindia zawadi mbalimbali ikiwemo safari za kwenda nje ya nchi, kutembelea mbuga za wanyama, vocha za manunuzi pamoja na vifaa kama simu za mkononi na kompyuta mpakato. “Kampeni hii inalenga kuwapa motisha wateja pamoja na watoa huduma kutumia zaidi mifumo ya kidijitali katika miamala yao ya kifedha,” amesema Nshekan...

TIMU YA WHEEL CHAIR TENNIS YAOMBA MILIONI 40 KUSHIRIKI MASHINDANO NCHINI MOROCCO

Image
Timu ya taifa ya tenesi kwa walemavu yaomba Milioni 40 kushiriki mashindano ya Morocco DAR ES SALAAM: TIMU ya Taifa ya wachezaji wa tenesi kwa walemavu (Wheelchair Tennis) imeomba msaada wa Shilingi milioni 40 ili kufanikisha safari ya kwenda kushiriki mashindano ya kimataifa yatakayofanyika nchini Morocco kuanzia Machi 30 hadi Aprili 3, 2026. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kocha wa timu hiyo ambaye pia ni Katibu, Riziki Salumu, amesema kuwa timu hiyo imejiandaa kikamilifu kushiriki mashindano hayo muhimu ya kimataifa. Salumu amesema jumla ya watu 10 wanatarajiwa kusafiri, wakiwemo wachezaji wanane, kiongozi mmoja pamoja na msaidizi wake. Ameeleza kuwa ushiriki wao katika mashindano hayo utasaidia kuitangaza Tanzania kimataifa, pamoja na kuwapa wachezaji fursa ya kupata nafasi za ufadhili endapo watafanya vizuri. Amesisitiza kuwa bado kuna uelewa mdogo kwa jamii kuhusu mchezo wa tenesi kwa watu wenye ulemavu, hali inayochangia kukosekana kwa s...

PROF MORI AWAITA WADAU WA KIMATAIFA UWEKEZAJI WANAWAKE BENKI YA CRDB IKISHIRIKI MKUTANO NCHINI URENO

Image
Profesa Mori awaita wadau wa kimataifa uwezeshaji wanawake Benki ya CRDB ikishiriki mkutano nchini Ureno Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Profesa Neema Mori ameshiriki mjadala wa Wanawake katika Biashara na Mitandao ya Ugavi uliofanyika pembezoni mwa mkutano wa Shirika la Fedha (IFC) wa Washirika wa Kimataifa wa Biashara unaondelea katika Jiji la Lisbon nchini Ureno. Katika mjadala huo, Profe Mori amebainisha kuwa uwezeshaji wa wanawake ni sehemu ya mkakati wa muda wa kati wa Benki ya CRDB katika kiuchumi, akieleza kuwa Benki imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 800 kufadhili biashara zinazoongozwa na wanawake. Uwezeshaji huu ambao umewafikia wanawake zaidi ya milioni 1 kote nchini, amesema unafanyika kupitia suluhisho bunifu kama CRDB Malkia, pamoja na programu jumuishi zinazotekelezwa na CRDB Bank Foundation kupitia Program ya IMBEJU, zinazojumuisha elimu ya fedha, mafunzo ya ujasiriamali, na kuwaunganisha wanawake na fursa za kimasoko. Aidha, ames...

WANARIADHA WATANZANIA WANG'ARA KIMATAIFA YAS KILI HALF MARATHON 2026

Image
Wanariadha wa Tanzania Wang’ara Kimataifa Yas Kili Half Marathon 2026 Wanariadha wa Tanzania wameendelea kuonesha kiwango cha juu cha ushindani katika mashindano ya YAS Kili International Half Marathon 2026, wakidhihirisha ubora wao katika mbio za masafa marefu barani Afrika. Mashindano hayo ya kilomita 21, ambayo ni sehemu ya tamasha kubwa la kila mwaka la Kili International Marathon, yameendelea kuwa jukwaa muhimu la kuhamasisha afya kupitia mazoezi pamoja na kukuza vipaji vya wanariadha wa ndani na nje ya nchi. Katika matokeo ya mwaka huu, upande wa wanaume ulitawaliwa na Mtanzania Michael Geay aliyenyakua medali ya dhahabu baada ya kumaliza mbio kwa muda wa saa 1:04:10. Alifuatiwa kwa karibu na Josephat Joshua Gisumo aliyetumia saa 1:04:14, huku Mkenya James Kairiuki akishika nafasi ya tatu kwa muda wa saa 1:04:30. Kwa upande wa wanawake, Hamida Musa aliibuka kinara kwa upande wa Watanzania, akifuatiwa na Failuna Matanga, huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Mkenya Vero...

MADAKTARI 30 WA KICHINA KUTOA HUDUMA ZA KITABIBU BURE MACHI 28 NA 29

Image
DAR ES SALAAM: Madaktari 30 kutoka China wanatarajiwa kuendesha kambi maalum ya siku mbili ya kutoa huduma za afya bure kwa wananchi wa Wilaya ya Ubungo, jijini Dar es Salaam. Kambi hiyo itafanyika katika Kituo cha Biashara cha EACLC mnamo Machi 28 na 29, 2026, ikiwa na lengo la kuwasaidia wananchi kupata uchunguzi na matibabu ya magonjwa mbalimbali bila malipo. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando, amesema madaktari hao watatoa huduma za upimaji na matibabu ya magonjwa mbalimbali ikiwemo kisukari, magonjwa ya moyo, saratani, shinikizo la damu pamoja na matatizo ya viungo kama pua na masikio. “Tunawaalika wananchi wote kujitokeza kwa wingi. Wazazi na walezi wahakikishe wanawaleta watoto wao ili waweze kupimwa na kupata matibabu bure,” amesema Msando. Kwa upande wake, Afisa Uhusiano na Habari, Linda Mtui, amesema kuwa kambi hiyo haitatoa tu matibabu bali pia ushauri wa kitaalamu kuhusu afya, pamoja na huduma m...

JONATHAN BUDJU KAJA WIMBO MPYA 'SAFE IN YOU'

Image
Jonathan Budju aibuka na wimbo mpya ‘Safe In You’ DAR ES SALAAM:STAA wa muziki wa Injili anayeishi Canada, Jonathan Budju, amewataka mashabiki wake kujiandaa na ujio wa wimbo wake mpya unaoitwa Safe In You, unaotarajiwa kugusa nyoyo za wengi. Msanii huyo ambaye mapema mwaka huu alifanya vizuri kwenye chati za muziki wa Injili kupitia wimbo wake sifa zake, sasa amekamilisha maandalizi ya kazi yake mpya ikiwemo audio pamoja na video yenye ubora wa hali ya juu. Akizungumza AMONLINE ujio wa wimbo huo, Jonathan amesema kuwa Safe In You utaachiwa rasmi Machi 27 kupitia majukwaa yote ya kidijitali, huku pia ukitarajiwa kuanza kuoneshwa kwenye vituo vikubwa vya televisheni Afrika Mashariki na Kati. “Niliachia EP mwezi Januari ambayo imefanya vizuri sana kwenye mitandao. Nawashukuru mashabiki wangu na nawaomba waendelee kuwa tayari kupokea Safe In You, wimbo wenye ujumbe wa nguvu za Mungu utakaowabariki wengi,” amesema Jonathan. Wimbo huo unatajwa kuwa na ujumbe wa matumaini, imani...

WAISLAM WATAKIWA KUENDELEZA MATENDO MEMA KAMA ILIVYOKUWA RAMADHANI

Image
Waumini wa dini ya kiislamu wametakiwa kuishi kama walivyokuwa wanaishi kwenye mwezi mtukufu SHEKHE Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Walid Alhad Omari amewataka waumini wa dini ya kiislamu kuyaenzi yale yote waliyoyafanya katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kuendelea kutenda yale mazuri na kuachana na maovu. Ameyasema hayo leo Machi 22, 2026 wakati alipokuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Michezo (Mama Samia Orphans Eid Day Out) lililoshirikisha watoto wenye mahitaji maalum (Yatima) kwenye viwanja vya gofu Lugalo Dar es Salaam. "Waislamu wanatakiwa kuishi kama walivyokuwa wanaishi katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani ni mwezi ambao umetukumbusha namna ambavyo tunatakiwa kuishi kwa kutenda mema na kuachana na yale maouvu," amesema Omari. Amesisitiza waumini hao waishi kwa kusaidiana, kusameheana pamoja na kufanya ibada usiku na mchana kama kama ilivyokuwa katika mfungo huo. Ameipongeza Kampuni ya Chocolate Princess kwa kuandaa Tam...

“JUA NAMBA ZAKO”: JKCI YAWASOGELEA WANANCHI KARIAKOO KUPAMBANA NA MAGONJWA YA MOYO

Image
DAR ES SALAAM: TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imeanzisha kampeni maalum ya “Jua Namba Zako” katika kliniki ya Kariakoo, ikiwa na lengo la kuwahamasisha wananchi kupima na kutambua mapema magonjwa ya moyo pamoja na magonjwa yasiyoambukiza. Kupitia kampeni hiyo, wananchi wanapata fursa ya kupima viashiria muhimu vya afya ikiwemo presha ya damu, mapigo ya moyo, kiwango cha sukari, mafuta kwenye damu, pamoja na urefu na uzito wa mwili. Akizungumza na waandishi wa habari Leo, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo, Dk. Peter Kisenge, alisema taasisi hiyo inaendelea kusogeza huduma karibu na wananchi ili kuwasaidia kugundua mapema magonjwa hayo. “Katika kuhakikisha tunawafikia wananchi walipo, leo tupo Kariakoo ambapo tunaendesha kambi ya siku tatu. Hadi sasa tumeshahudumia zaidi ya watu 226,” alisema Dk. Kisenge. Ameeleza kuwa magonjwa ya moyo na yasiyoambukiza yanaongezeka kwa kasi na kusababisha vifo vingi, hivyo kampeni hiyo inalenga kuyad...

LADY JAYDEE AINGIA MKATABA NA UNIVERSAL MUSIC GROUP EAST AFRICA

Image
Lady Jaydee aingia mkataba mkubwa na Universal Music Group East Africa DAR ES SALAAM:MSANII mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura maarufu kama Lady Jaydee, amepata dili kubwa baada ya Kampuni ya Universal Music Group East Africa kutangaza rasmi ushirikiano wake na nyota huyo wa Afrika Mashariki. Lady Jaydee anatambulika kama mmoja wa wasanii wenye sauti yenye ushawishi mkubwa na iliyodumu kwa muda mrefu katika tasnia ya muziki wa ukanda huu, hatua inayofanya ushirikiano huo kuwa wa kihistoria. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, ushirikiano huo unaakisi imani ya pamoja juu ya nguvu ya muziki wa Afrika Mashariki pamoja na wajibu wa wasanii wakubwa katika kuukuza na kuufikisha katika soko la kimataifa. Hatua hiyo pia imeelezwa kuwa ni sehemu muhimu ya mkakati wa Universal Music Group East Africa wa kuibua na kukuza vipaji bora zaidi kutoka katika ukanda wa Afrika Mashariki. Kupitia makubaliano hayo, pande zote zimejipanga kuinua ubora wa muziki, kupanua wigo wa us...

EACLC YAFUNGUA MILANGO KWA WASANII KUFANYA KAZI

Image
EACLC Yafungua Milango kwa Wasanii wa Filamu, Yatoa Fursa Mpya Dar es Salaam Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC), Dkt. Lissa Wang, amefanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dkt. Gervas Kasiga, kwa lengo la kufungua fursa mpya za ushirikiano zitakazonufaisha tasnia ya filamu nchini. Mazungumzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, yamelenga kuimarisha mahusiano kati ya EACLC na Bodi ya Filamu Tanzania, huku yakifungua milango kwa wadau wa filamu na michezo ya kuigiza kunufaika na miundombinu ya kituo hicho kikubwa cha kibiashara. EACLC ni kituo chenye zaidi ya maduka 2,000, kikiwa na mandhari ya kipekee pamoja na fursa mbalimbali zinazoweza kutumika katika utayarishaji wa filamu. Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Wang amesema kituo hicho kiko tayari kushirikiana na wanatasnia wa filamu kwa kuruhusu matumizi ya eneo hilo kama mandhari ya upigaji picha bila malipo. Hata hivyo, amesisitiza umuhimu wa kudumish...