Posts

Showing posts from March, 2025

ALAFA APATA UFADHILI WA KUSOMEA UHANDISI WA NDEGE

Image
Arafa apata ufadhili wa kusomea Uhandisi wa Ndege ARAFA Mazige, msichana mwenye ndoto ya kuwa mhandisi wa injini za ndege, amepata ufadhili wa masomo kupitia taasisi ya UNI-AID AFRICA na atasoma Shahada ya Uhandisi wa Ndege Chuo Kikuu cha JAIN nchini India. Msichana huyo kutoka Mvomero mkoani Morogoro alipata msukumo kutoka kwa baba yake, Hashimu Mazige, ambaye ni mbunifu wa teknolojia licha ya kutosomea rasmi. Alishuhudia baba yake akifufua gari lililokuwa limeharibika kwa miaka mitatu, jambo lililomtia moyo kuamini kuwa kila kitu kinawezekana. Akizungumzia mafanikio yake, Arafa anawahamasisha wanafunzi wenzake wa kike kujituma kwa kufanya vizuri darasani na kutumia mitandao ya kijamii kutafuta fursa za kielimu. "Nitaendelea kujifunza zaidi ya yale yanayofundishwa darasani ili kuleta maendeleo ya kiteknolojia na kuwasaidia wengine kama mimi,"amesema. Baba yake Hashim Mazige amesema kila mtoto anaweza kufanikisha ndoto yake ikiwa atapewa mazingira sahihi. ...

UPENDO NKONE AWASHAURI WANAUME KUACHA KULA MAYAI

Image
Upendo Nkone Atoa Ushauri wa Kiafya Kuhusu Ulaji wa Mayai ya Kisasa Msanii wa nyimbo za Injili nchini, Upendo Nkone, ametoa ushauri kwa wazazi kuhusu lishe ya watoto wao wa kiume, akieleza athari zinazoweza kutokana na ulaji wa mayai ya kisasa. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Upendo ameonya kuwa mayai ya kisasa yanaweza kuchangia ukuaji wa matiti kwa wanaume kutokana na kemikali zinazotumika katika uzalishaji wake. Amesisitiza umuhimu wa kula mayai ya kienyeji badala ya yale ya kisasa, akiwataka wanaume kuwa makini na vyakula wanavyotumia. Mbali na hilo, amependekeza wanaume kula chipsi bila mayai kama njia mbadala ya kudhibiti athari hizo za kiafya. Je, unakubaliana na ushauri wa msanii huyu? Wewe unapendelea mayai ya kienyeji au ya kisasa?

WATANO WAKAMATWA KWA KOSA LA UBAKAJI

Image
Wasimamizi watatu wa baa nchini Ubelgiji ni miongoni mwa wanaume watano ambao wamekamatwa kuhusiana na uchunguzi wa vitendo vya ubakaji na unyanyasaji wa kingono kwa makumi ya wanawake, polisi wa eneo hilo wamesema. Waendesha mashtaka walisema washukiwa hao walihusishwa na unywaji pombe wa waathiriwa wa kike 41 kuanzia Desemba 2021 hadi Desemba 2024. Washukiwa hao watatu waliendesha biashara katika mji wa kaskazini-magharibi wa Kortrijk ambapo vitendo vya kuweka vilevi kwenye vinywaji vilifanyika. Wachunguzi wanasema wanaamini walijadiliana kuhusu mashambulizi hayo. Ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma ilisema kwa jumla wanaume watano walikamatwa Jumatano na Alhamisi. Wanaume wawili waliokamatwa walifika mbele ya hakimu siku ya Alhamisi, waendesha mashtaka walisema. Wanaume wengine wawili bado wanahojiwa na wapelelezi huku mtu wa tano akiachiliwa baada ya kuhojiwa. Wanaume hao wanashukiwa kwa ubakaji, unyanyasaji wa kijinsia na usimamizi haramu wa vitu vyenye madhara, ofisi ...

GWAJIMA MAZINGIRA RAFIKI KWA MABINTI

Image
Waziri wa Maendeleo ya Jamii , Jinsia ,Wanawake na makundi maalumu Dkt Dorothy Gwajima amesema kadri siku zinavyoenda ndivyo ambavyo mazingira yanazidi kuwa rafiki kwa mabinti na wanawake nchini. “Tanzania imepiga hatua kubwa katika uwakilishi wa wanawake, idadi yao bungeni imeongezeka kutoka 8% mwaka 1995 hadi 35% mwaka 2020, Tutaendelea kuimarisha uwakilishi huu” “Tunajenga mazingira yanayowezesha wanawake kustawi kama viongozi, wajasiriamali, na mawakala wa mabadiliko, Uwezeshaji wa kiuchumi ni msingi wa kushiriki kwao katika jamii” “Tutaendelea kuhakikisha wasichana na wanawake wanapata nafasi ya kuongoza na kuandika mwanzo mpya katika historia yetu, Ni wakati wa kuvunja vikwazo na kuleta mabadiliko makubwa”

LYDIA AELEZEA SAFARI YAKE YA KUSAIDIA MABINTI

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa herinitiative Lydia Charles akielezea lilipotokea wazo la kuwasaidia mabinti kutoka chini na kwenda ngazi za juu kijamii, kisiasa na kiuchumi “Siku moja, nikiwa safarini kwenda Dodoma, nilisimama barabarani kupata kifungua kinywa, Msichana mdogo aliniletea supu. Nilimuuliza, Kwa nini hauko shuleni au nyumbani? Alinijibu, Ningetamani iwe hivyo, lakini niko kwenye hali ngumu sana.” “Maneno ya yule msichana yalinifanya nitafakari, Kuna wasichana wengi wenye ndoto kubwa, lakini umasikini ni kikwazo kikubwa, Nikakumbuka hadithi yangu mwenyewe, safari yangu kutoka shule ya kata isiyo na maktaba, maabara, wala walimu wa kutosha” “Shule yangu ilikuwa na changamoto nyingi masaa mawili ya kutembea kila siku, wanafunzi wengi wakiacha shule kwa sababu ya umasikini, ndo a za utotoni, na mimba za mapema, Tulianza 200, lakini ni 9 tu tulifika kidato cha sita, 3 tu tukiwa wasichana” “sikuwa na Uwezo mkubwa lakini nilihitaji kufanya kitu, Mimi na marafiki zangu ...

NANCY SUMARI AMTAMBULISHA LYDIA CHARLE

Image
Miss Tanzania na malkia wa Nguvu Nancy Sumari ameelezea safari ya mrembo Lydia Charles wakati anamkaribisha kabla ya kuzungumza safari yake ilipoanzia Katika halfa ya kusheherekea Her Iniative iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuelezea safari ya Mkurugenzi wa taasisi huyo. “Ingawa alikulia katika mazingira yenye rasilimali chache , alikuwa na dhamira kubwa kuliko wengi. Alisoma katika shule zenye vifaa duni. Alikaa darasani bila walimu wa kutosha au maabara. Lakini bado alifanikiwa. Alikuwa mmoja wa wasichana watatu pekee kati ya 200 waliomaliza shule yake ya sekondari.” “Alipofanikiwa, hakubaki na mafanikio yake peke yake. Alirudi kuwasaidia wengine. Alianza kuwaelekeza wasichana shuleni kwake. Kisha akajenga programu. Kisha akaunda shirika. Na sasa ni harakati.” “Amefundisha wasichana vijana kote Tanzania ujuzi wa kidigitali, ujasiriamali, na uongozi. Si ili wawashukuru wengine, bali ili wawe tayari. Tayari kumiliki sauti zao. Tayari kujenga biashara. Tayari kuketi...

HER INITIATIVE ILIANZA NA WADADA 3 SASA WAPO 31000

Image
Ikiwa ni muendelezo wa kusherehekea Mwezi wa Wanawake Duniani , Mwenyekiti wa Taasisi ya herinitiative Vanessa Anyoti ameelezea lengo la kuwakutanisha pamoja wanawake wa kada mbalimbali. Amesema kuwa lengo la kuwasherehekea mabinti na wanawake wanaofanya vizuri kwenye nafasi mbalimbali lakini pia ameelezea maendeleo ya Taasisi yao tangu kuanzishwa kwake. “Niko hapa kwa ajili ya kufungua event hii na nina furaha sana kuwakaribisha siku ya leo , Mgeni wetu rasmi , wanufaika wetu na wanafunzi karibuni sana “ “Her initiative ilianza kama movement chuoni na ilikua wasichana watatu waliokua wanaandaa event ili kuwajulisha wenzao kuhusu haki zao na mpaka leo tumefikia zaidi ya wasichana 31,000 na tumedhamiria kuifanya kesho ya mabinti wa Tanzania kuwa bora zaidi”

LAMATA NILITAKA KUWA TRAFFIC

Image
Lamata ndoto yangu ilikuwa kuwa askari wa usalama barabarani Mwandishi na Muandaaji wa Filamu nchini Tanzania, Leah Mwendamseke 'Lamata', amefunguka kuhusu ndoto yake ya awali ya kutaka kuwa askari wa usalama barabarani (Traffic Police), kabla ya kujikuta akijiingiza kwenye tasnia ya filamu. Akizungumza kuhusu safari yake ya maisha, Lamata alieleza jinsi hali ilivyobadilika na kumlazimu kuchagua mwelekeo tofauti na aliokuwa ameupangilia awali. "Maisha bwana ni tofauti na unavyotaka. Nilikuwa natamani sana kuwa Askari wa Usalama Barabarani, lakini sasa nimeibukia kuwa mtayarishaji wa filamu hapa Tanzania," amesema Lamata. Ameongeza kuwa wakati mwingine mtu anaweza kuwa na ndoto fulani lakini asifanikiwe, hivyo ni muhimu kutafuta njia nyingine ya kufanikisha maisha. "Unachotamani kuwa usipofanikiwa, angalia njia nyingine, utatoboa kimaisha zaidi kuliko unavyodhania," amesisitiza Lamata. Kwa sasa, Lamata ameendelea kufanya vizuri katika se...

LAMATA KUWAUNGANISHA KAJALA NA HARMONIZE

Image
Penzi la Kajala na Harmonize lamata kuwaunganisha Mtayarishaji wa filamu Leah Mwendamseke 'Lamata' amefunguka juu ya sababu ya kuwakutanisha msanii wa filamu nchini Frida Kajala na msanii wa Bongo Fleva nchini Rajab Abdul 'Harmonize'. Wawili hao, ambao hapo awali walikuwa wapenzi hadi walifikia hatua ya kuvalishana pete, lakini mahusiano yao yalikatishwa njiani na wakaishia kutupiana maneno mitandaoni, walifanikiwa kukutana tena uso kwa uso katika mechi za Samia Cup zinazoendelea. Lamata amesema, "Kweli nilikuwa kiunganishi cha wawili hao kwa kuwa wote ni watu wangu wa karibu, hivyo wakawa pamoja. Yalioendelea baada ya hapo ni yao wenyewe." Mbali na hilo, Lamata ameongelea pia maendeleo ya timu yake, Lamata Village SC, akieleza safari yake tangu mwanzo wa mawazo yake hadi leo ambapo timu hiyo inapata Shilingi Milioni 5 kutoka Selcom. "Nilianzisha timu ya Lamata Village kama utani, lakini naona wakiendelea kufanya vizuri hadi kufikia hatu...

COLETHA SIPANGIWI MAISHA NAISHI NITAKAVYO

Image
Msanii wa filamu nchini, Coletha Raymond maarufu kama 'Coletha,' amesema kuwa anaishi maisha yake kwa namna anavyotaka na hataki kupangiwa na mtu yeyote jinsi ya kuishi. Coletha ametoa kauli hiyo baada ya kushambuliwa mitandaoni kufuatia picha zake akiwa kanisani huku amevalia suruali. "Kuvaa suruali kanisani si dhambi. Kitu muhimu ni matendo yako, si mavazi. Na hata hivyo, suruali niliyovaa haikuwa imenibana, ilikuwa ya heshima," amesema Coletha. Akiendelea kujibu wakosoaji wake, alisisitiza: "Nawaambia watu wanaonizungumzia mitandaoni kuwa sipangiwi maisha. Ninaishi ninavyotaka, si kama wanavyotaka wao. Najua kuwa sijafanya kosa lolote." Aidha, Coletha ameongeza kuwa ni kawaida kwa watu kuzungumza au hata kuzusha mambo kuhusu wengine, lakini hilo halitomwathiri katika maisha yao.

TUZO ZA KARIAKOO BUSINESS AWARDA KUKUZA USHINDANI WA BIASHARA

Image
Mwandaaji wa tuzo hizo, Frank Mbwana, amesema lengo la tuzo hizo ni kutambua mchango wa wafanyabiashara wa Kariakoo na kuwapongeza kwa juhudi zao katika kukuza uchumi. Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amewataka Watanzania kuwaunga mkono wafanyabiashara wa Kariakoo na kushirikiana nao kwa maendeleo ya biashara nchini. "Tuzo hizi zimekuja wakati muafaka na katika sehemu muhimu ya biashara. Sikutarajia kuona muitikio mkubwa wa wafanyabiashara," alisema Mpogolo. Naye Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Kumbilamoto, amepongeza mshikamano wa wafanyabiashara wa Kariakoo na juhudi zao za kuendeleza biashara. Kwa upande wake, Seveline, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo, amepongeza kuanzishwa kwa tuzo hizo, akisema zitachochea ushindani wa kibiashara na kuongeza ufanisi katika sekta hiyo.

KESI YA NICOLE YAPIGWA KALENDA APRILI 14

Image
Kesi ya uhujumu uchumi ya msanii nicole yaahirishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni imeshindwa kuendelea na kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili msanii Joyce Mbaga, maarufu kama Nicole, kutokana na upelelezi wa kesi hiyo kutokamilika. Mbali na Nicole (32), mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Rehema Mahanhu. Wawili hao walifikishwa mahakamani hapo Machi 10, 2025, na kusomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ramadhan Rugemalira, kwa mujibu wa Wakili wa Serikali, Rhoda Maingu. Katika kesi hiyo iliyotajwa leo, upande wa Jamhuri umeieleza mahakama kuwa bado wanakamilisha upelelezi, hivyo wameomba ahirisho. Kutokana na maombi hayo, kesi imeahirishwa hadi Aprili 14, 2025. Nicole na Mahanhu, ambao wako nje kwa dhamana, wanakabiliwa na mashtaka matatu, ikiwa ni pamoja na: Kuongoza genge la uhalifu Wanatuhumiwa kuendesha biashara haramu kwa lengo la kujipatia faida isiyo halali kutoka kwa jamii. Kupokea amana bila leseni Inadaiwa kati ya Julai 2024 na Machi 2025, wakiwa...

Ben Pol atoa wito kwa wasanii kuzingatia taratibu za Sanaa

Image
Msanii nyota wa muziki wa R&B, Ben Pol, ametoa wito kwa wasanii wote kuhakikisha wanakuwa na kibali halali cha BASATA na kuendeleza utamaduni wa kutembelea Baraza la Sanaa la Taifa ili kujifunza zaidi. Ben Pol alitembelea ofisi za BASATA na kukutana na Katibu Mtendaji, Dkt. Kedmon Mapana, ambapo alihuisha kibali chake cha sanaa. Kupitia ziara hiyo, aliwahimiza wasanii kuhakikisha wanazingatia taratibu za kisheria na kusajili kazi zao rasmi ili kulinda haki zao na kuimarisha tasnia ya sanaa nchini. Akiipongeza BASATA kwa juhudi zake katika kukuza na kulinda sanaa Tanzania, Ben Pol alisisitiza kuwa ushirikiano mzuri kati ya wasanii na taasisi hiyo ni nyenzo muhimu kwa mafanikio ya sekta ya sanaa. Ameahidi kuendelea kufanya kazi kwa weledi na pia kushirikiana na BASATA katika kukuza vipaji vya wasanii chipukizi, akihamasisha utii wa sheria na ubunifu wenye maadili.

VETA YAFADHILI MAFUNZO LWA WANAWAKE 3000 DODOMA

Image
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imetoa ufadhili wa mafunzo ya muda mfupi kwa wanawake 3000 jijiji Dodoma, yatakayotolewa katika Chuo cha VETA Dodoma. Akizungumza jana, tarehe 24 Machi, 2025 wakati wa hafla ya uzinduzi wa mafunzo hayo yanayotolewa kupitia kikundi cha Wanawake na Samia, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mheshimiwa Rosemary Senyamule amemshukuru Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore kwa ufadhili wa mfunzo hayo. Senyamule amesema wanawake wengi, hawana ujuzi, hivyo mafunzo ya stadi kwao ni muhimu ili kuwawezesha kujiajiri au kuajiriwa. “Dodoma sasa ni mji wa kitalii na watu wengi wanakuja kwa ajili ya kupata huduma sa Kiserikali. Wapo wengine kutoka mataifa mbalimbali. Hivyo tunahitajika kutoa huduma za kiwango cha kimataifa na hilo linawezekana ikiwa tutapata mafunzo,” Senyamule amesema. Kwa upande wake Mwenyekiti wa wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma, Bi Fatuma Madidi ametoa pongezi kwa Mkurugenzi Mkuu wa VETA na Mkuu wa chuo cha VETA Dodoma kwa ...

Waitara NBC Trophy yavuta wachezaji 147

Image
MWENYEKITI wa Klabu ya Gofu Lugalo Brigedia Jenerali mstaafu Michael Luwongo amesema shindano la Waitara NBC Trophy limepata mafanikio baada ya kuwavutia wachezaji 147 kujitokeza kushiriki katika vipengele tofauti. Kivutio kikubwa zaidi katika shindano hilo ni aliyeshinda ushindi wa jumla ni Mtu mzima kidogo kwa mara a ya Mzee ukilinganisha na idadi kubwa ya washiriki ni vijana. Mshindi wa jumla alikuwa Dk Edmund Mndolwa ambaye alipata pointi za juu akishinda Gross 78 HCP 12 na Net 66 ambaye hata yeye mwenyewe hakuamini na kusema atawaonesha wajukuu zake Kombe alilopata. Luwongo amesema shindano hilo la kumuenzi Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali George Waitara lilikuwa lifanyike mwaka jana lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao hawakufanikiwa na ndio lilifanyika mwishoni mwa wiki huku akitangaza lingine litafanyika tena hapo baadaye. "Tumepata mafanikio kwasababu washiriki wamekuwa wengi katika vipengele lakini mwisho wa siku washindi ni wachache, tunawapongez...

TAMASHA LA KUOMBEA UCHAGUZI MKUU KUFANYIKA MIKOA 26

Image
Tamasha la kuombea Uchaguzi Mkuu linatarajiwa kufanyika katika mikoa 26 ya Tanzania, likianza jijini Dar es Salaam mwaka huu. Tamasha hilo litapambwa na waimbaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi, likiwa na lengo la kuhimiza amani na mshikamano kuelekea uchaguzi mkuu. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Machi 24, 2025, Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama, amesema ibada hiyo ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. "Lengo ni kuweka umoja na ushirikiano miongoni mwa Watanzania, kuwaombea viongozi watakaochaguliwa ili waweze kutuongoza kwa hekima na busara," alisema Msama. Tamasha hilo litashirikisha waimbaji kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, na Rwanda, ambao wanatarajiwa kutoa burudani na kushiriki maombi maalum kwa ajili ya uchaguzi. Aidha, Msama amewaomba viongozi wa vyama vya siasa kuhakikisha wanatumia lugha zenye heshima katika mikutano yao ya kampeni badala ya ...

MNEC JUMAA ASEMA MIAKA MINNE YA RAIS SAMIA IMEKUWA YA MAFANIKIO MAKUBWA ,ATAJA MAMBO MAKUBWA MANNE MUHIMU.

Image
Na Mwandishi Wetu MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi Hamoud Jumaa( MNEC), amesema kuwa miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt .Samia Suluhu Hassan imekuwa na mafanikio makubwa kwa Taifa na Wananchi wake. Jumaa amesema mafanikio hayo yametokana na sera na mikakati ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo imekuwa ikilenga kuongeza ushirikiano na maendeleo ya jamii kwa ujumla. Kauli hiyo ya Jumaa imekuja ikiwa ni sehemu ya kumpongeza Rais Samia kwa kazi alizofanya katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake tangu aliporidhi kiti hicho kutoka kwa mtangulizi wake Hayyati John Pombe Magufuli (JPM) aliyefariki Machi 2021. Jumaa amesema kwa maoni yake Rais Dkt. Samia amefanikiwa kutokana na kusimamia mambo makubwa manne ambayo kimsingi yamesaidia kuleta tija na faida kwa Watanzania na Taifa nzima kiujumla. Jumaa, ametaja jambo la kwanza kuwa ni ushirikiano katika jamii, ambapo amesema Serikali imehamasisha ushirikiano wa jamii ka...

JENGO LA CHUO CHA USTAWI LAKAMILIKA ASILIMIA 35

Image
CHUO cha Ustawi wa Jamii, kimesema kitakamilisha kwa wakati mradi wa ujenzi wa ujenzi ukumbi wa jengo la mihadhara la chuo hicho. Mkuu wa chuo hicho Dk. Joyce Nyoni amesema hayo wakati akitoa taarifa ya ujenzi huo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii jijini Dar es Salaam leo. Kamati hiyo ilitembelea mradi huo ikiongozwa na mwenyekiti wake, Fatma Taufiq akiwepo pia Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mwanaid Ali Khamis. "Pamoja na changamoto tunazokutana nazo za mtiririko ili kusaidia mradi huu, lakini tutaukamilisha kwa wakati ili ukumbi uweze kufanya kazi," amesema Dk. Joyce. Amefafanua kuwa mradi huo unaojengwa katika kampasi ya Kijitonyama Dar es Salaam kwa mapato ya ndani kwa gharama ya Sh. 626,405, 367, ulianza Julai mwaka jana, na kwamba inatarajiwa kukamilika Juni mwaka huu. "Ukumbi wa mihadhara utakuwa na uwezo wa kuingiza watu 400. Meneja wa mradi ni wataalam WA ndani ya chuo, laki...

STEVE NYERERE KUMSAIDIA NICOLE

Image
  MWENYEKITI wa Mama ONgea na Mwanao Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ ametangaza kusimama na  mwigizaji Joyce Mbaga ‘Nicole’  ili kumsaidia kupata dhamana. Kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii, Steve Nyerere ameweka ujumbe na kusema hakuna sababu ya kuangalia makosa yake kwa kuwa hakuna aliyekamilika. Nicole yuko chini ya ulinzi na ameshtakiwa kwa makosa  ya kuendesha genge la uhalifu na kupokea pesa shilingi milioni 185.5 za Tanzania kutoka kwa umma bila kibali kutoka Benki Kuu ya Tanzania. Steve amesema hakuna haja  ya kuangalia amefanya nini, bali kuangalia uwezekano wa kumsaidia kupata dhamana yake kwani anapitia kipindi kibaya sana ambacho anahitaji faraja. “Tusimame kumuombea dhamana tunajua na kutambua sheria na kuheshimu sheria kwenye Taifa letu, “Niombe sio muda wa kuliangalia kosa ni muda wa kulitibu kosa nani mkamilifu hapa Duniani, “Mimi Binafsi kama Steven Mengele nipo tayari kumsaidia kutoka ndani kwa kufuata taratibu zote na akipata dhamana ba...

TAMASHA LA PASAKA KUFANYIKA APRILI NA kUOMBAE TAIFA

Image
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Kuombea  uchaguzi mkuu  2025 ndugu Alex Msama leo ameongea na wandishi wa habari kuwa Maandalizi ya Tamasha la kuombea uchaguzi yanaendelea vizuri na  kuwa Tamasha hilo lipo na litafanyika Tarehe 20, Aprili 2025 katika jiji la Dar es Salaam na baadae kufanyika Mikoa 26 ya Tanzania Ameyasema hayo leo alipongea na waandishi wa Habari kuhusiana na maandalizi ya Tamasha hilo. “Maandalizi ya tamasha yanaendelea vizuri na tunakaribisha wadhamini kuja kusaidia kufanikisha Tamasha hili kubwa ambalo litafanyika Mikoa yote ya nchi yetu ya Tanzania tukianzia  na Mkoa wa Dar es Salaam.   Alex Msama Mwenyekiti wa Kamati ya Mandalizi ya tamasha hilo amesema kwasasa jambo kubwa linalofanyika ni kuendelea kuzungumza na wafadhili na tukifanikiwa tu kupata wadhamini basi tamasha  litakuwa halina kingilio litakuwa bule.  Tamasha la Kuombea   uchaguzi litafanyika hivi karibuni na kuwaunganisha waimbaji mbali ...

Serikali Yatangaza Mpango wa Kuboresha Usalama wa Madereva wa Bolt

Image
Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi imetangaza kuwa itajiandaa na utaratibu maalum wa kusaidia madereva wa mitandaoni kuepuka kuhusika katika uhalifu na kuhakikisha usalama kwa abiria. Akizungumza na madereva wa Bolt katika Mkutano wa Kilele wa Usalama wa Madereva wa Mitandaoni nchini, Msaidizi wa Wizara ya Uchukuzi, Andrew Magombana, amesema kuwa utaratibu huu utahakikisha madereva wanapata msaada wa kutosha katika kutatua changamoto mbalimbali wanazokutana nazo. "Tunajua kuwa moja ya changamoto mnayopitia ni abiria mwingine anayepakia kinyume na aliyetuita kupata huduma. Hii ni moja ya sababu za uhalifu," amesema Magombana. Ameozngeza kuwa utaratibu utakaowekwa utawezesha madereva kuepuka kupakia abiria wasiotakiwa na kudhibiti uhalifu. Pia, ameeleza kuwa Wizara ya Uchukuzi itashughulikia changamoto ya maegesho ya magari na maeneo ya kuegesha magari kwenye viwanja vya ndege kwa kuweka utaratibu mzuri utakaokuwa rafiki kwa madereva wa mitandaoni. Mkurugenzi wa Bolt Tanzania,...

TANESCO YAZINDUA NAMBA MPYA KWA HUDUMA BORA KWA WATEJA

Image
Wapokeaji simu wa TANESCO wametakiwa kutoa majibu mazuri kwa wateja ili kuboresha huduma kwa Watanzania. Serikali imesisitiza kuwa haitavumilia huduma zisizokidhi mahitaji ya wananchi. Katika juhudi za kuboresha huduma kwa wateja, TANESCO imezindua namba mpya ya simu  180 , ambayo ni bure kupiga kwa mitandao yote isipokuwa mtandao wa Yas, ambao bado uko kwenye marekebisho ya huduma zao. Akizungumza kuhusu hatua hiyo, Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema kuwa namba ya awali iliwakwamisha wananchi wengi kutoa taarifa kwa sababu ya ukosefu wa salio. "Kwa sasa, kupitia  180 , wateja wanaweza kutoa taarifa na kutatua changamoto zao bila malipo," alisema Kapinga. Pia, Naibu Waziri amesisitiza kuwa serikali inaendelea kutekeleza mpango wa kuboresha upatikanaji wa umeme nchini katika maeneo mbalimbali. "Umeme utasaidia siyo tu katika shughuli za nyumbani kama kupika kwa haraka na usafi, bali pia katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi," aliongeza. Hatua hii inat...

MOI YAPOKEA RUNINGA KUTOKA AZAM TV NAR UK

Image
Dar es Salaam  TAASISI ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imepokea msaada wa runinga sita kutoka Kampuni ya Ving’amuzi ya Azam TV kwa kushirikiana na kampuni ya vifaa vya kielektroniki, Mr UK. Msaada huo ulikabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya, amewashukuru wahisani hao kwa kujali ustawi wa jamii kupitia sehemu ya faida wanayoipata katika biashara zao. “Tunawashukuru sana Azam na Mr UK kwa kazi nzuri, kwa kutambua kwamba katika faida wanayoipata, wanarudisha kwa jamii hiyo hiyo,” amesema Dkt. Mpoki. Ameongeza kuwa runinga hizo zitawasaidia wagonjwa kupata taarifa mbalimbali wakati wa matibabu yao katika taasisi hiyo. Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi wa MOI, Fidelis Minja, ametoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kusaidia taasisi hiyo kwa kutoa misaada mbalimbali, ikiwemo vifaa vya ukarabati wa jengo na miundombinu mingine. Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mr UK, Shedrack Theophil, amesema kuwa si mara yao ya kwanza kutoa msaada w...

Punguzo la bei kwa Abiria Linagharamiwa Kikamilifu na Bolt

Image
  Dar es Salaam, Tanzania Bolt, jukwaa linaloongoza katika huduma za usafiri wa mtandaoni, linathibitisha rasmi kwamba punguzo linalotolewa kwa abiria linagharamiwa kikamilifu na Bolt. Taarifa hii inakuja wakati ambapo kuna dhana potofu kuhusu punguzo la safari zinazotolewa kwa abiria. Wengi wanadhani kuwa punguzo hizi zinaathiri mapato ya madereva, lakini kampuni inafafanua kuwa hali ni kinyume na mawazo hayo. “Abiria anapopata punguzo kwenye nauli, Bolt hulipa dereva mara moja kwa kiasi kilichopunguzwa. Malipo haya huonyeshwa papo hapo kwenye mapato ya dereva, kuhakikisha kuwa hakuna hasara yoyote ya kifedha inayopatikana. Tumebuni mfumo huu kwa uwazi ili madereva waweze kufuatilia mapato yao kwa urahisi kupitia programu ya Bolt kwa madereva,” amesema Dimmy Kanyankole, Meneja Mkuu wa Bolt Kenya na Tanzania. "Licha ya hatua hizi, bado kuna madai yanayoendelea kuwa punguzo la Bolt linapunguza mapato ya madereva. Hata hivyo, ukweli ni kwamba madereva hupokea nauli kamili kabla ya B...

ROSE MHANDO :MSAMA NI BABA KWANGU ACHENI KUNIGOMBISHA NAYE.

Image
  Mwimbaji nguli wa Muziki wa Injili Afrika Mashariki na Kati, Rose Mhando amesema amekiri kwamba Mkurugenzi wa Msama Promotions ambaye ni mwandaaji  wa matamasha mbalimbali ya Muziki wa Injili  Alex Msama,  ni zaidi ya Baba kwake kwani tangu alipoanza kazi zake za Uimbaji wa nyimbo za  Injili amekuwa akifanya naye kazi kwa wema bila dhuluma na Msama hajawahi nidhulumu.   Muhando alisema yeye pamoja na baadhi ya wasanii wenzake wa muziki wa Injili, hawawezi kujivunia mafanikio yao bila kutaja jina la Alex Msama ambaye hivi karibuni alipata tuzo ya Muandaaji Bora wa Muziki wa Injili wa wakati wote Rose ametoa  kauli hiyo baada ya hivi karibuni kuwapo  taarifa kwenye mitandao ya kijamii, zikidai msanii  huyo aliwahi kudhulumiwa haki zake na Msama. Akizungumzia kuhusu madai hayo, Rose alisema ameshitushwa sana na kusikitishwa sana na tarifa hizo na kuongeza kuwa hajui zimetokea wapi na watunzi wa uzushi  huo wana lengo gani. Alisema ka...