JENGO LA CHUO CHA USTAWI LAKAMILIKA ASILIMIA 35
CHUO cha Ustawi wa Jamii, kimesema kitakamilisha kwa wakati mradi wa ujenzi wa ujenzi ukumbi wa jengo la mihadhara la chuo hicho.
Mkuu wa chuo hicho Dk. Joyce Nyoni amesema hayo wakati akitoa taarifa ya ujenzi huo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii jijini Dar es Salaam leo.
Kamati hiyo ilitembelea mradi huo ikiongozwa na mwenyekiti wake, Fatma Taufiq akiwepo pia Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mwanaid Ali Khamis.
"Pamoja na changamoto tunazokutana nazo za mtiririko ili kusaidia mradi huu, lakini tutaukamilisha kwa wakati ili ukumbi uweze kufanya kazi," amesema Dk. Joyce.
Amefafanua kuwa mradi huo unaojengwa katika kampasi ya Kijitonyama Dar es Salaam kwa mapato ya ndani kwa gharama ya Sh. 626,405, 367, ulianza Julai mwaka jana, na kwamba inatarajiwa kukamilika Juni mwaka huu.
"Ukumbi wa mihadhara utakuwa na uwezo wa kuingiza watu 400. Meneja wa mradi ni wataalam WA ndani ya chuo, lakini fundi ni Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam," amesema.
Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya jamii Jinsia na Wanawake na Makundi Maalum Mwanaidi Ali Khamis amesema chuo hicho kimepiga hatua na kwamba jengo hilo likikamilika litasaidia wanafunzi kuwa na mazingira rafiki ya kufanyia mihadhara.
Mwenyekitii wa kamati hiyo, Fatma Taufiq amesema anapongeza juhudi zinazofanywa na chuo za kukiboresha ikiwamo mradi huo walioukagua.
"Kwa niaba ya kamati niupongeze uongozi wa chuo na wizara kwa ujumla kwa jinsi ambavyo mnafanya kazi ya kuboresha mazingira ya chuo na pia Asante kwa taarifa yenu, mtatukabidhi tuipeleke bungeni, " amesema Fatma.


Comments
Post a Comment