Serikali Yatangaza Mpango wa Kuboresha Usalama wa Madereva wa Bolt
Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi imetangaza kuwa itajiandaa na utaratibu maalum wa kusaidia madereva wa mitandaoni kuepuka kuhusika katika uhalifu na kuhakikisha usalama kwa abiria.
Akizungumza na madereva wa Bolt katika Mkutano wa Kilele wa Usalama wa Madereva wa Mitandaoni nchini, Msaidizi wa Wizara ya Uchukuzi, Andrew Magombana, amesema kuwa utaratibu huu utahakikisha madereva wanapata msaada wa kutosha katika kutatua changamoto mbalimbali wanazokutana nazo.
"Tunajua kuwa moja ya changamoto mnayopitia ni abiria mwingine anayepakia kinyume na aliyetuita kupata huduma. Hii ni moja ya sababu za uhalifu," amesema Magombana.
Ameozngeza kuwa utaratibu utakaowekwa utawezesha madereva kuepuka kupakia abiria wasiotakiwa na kudhibiti uhalifu.
Pia, ameeleza kuwa Wizara ya Uchukuzi itashughulikia changamoto ya maegesho ya magari na maeneo ya kuegesha magari kwenye viwanja vya ndege kwa kuweka utaratibu mzuri utakaokuwa rafiki kwa madereva wa mitandaoni.
Mkurugenzi wa Bolt Tanzania, Dimmy Kanyankole, alikiri hatua za kampuni hiyo kuzuia madereva kutumia akaunti za madereva wengine, akisema kuwa hii imekuwa na manufaa katika kupunguza uhalifu na kudumisha usalama.
Kwa upande mwingine, Polisi Kanda ya Kinondoni, Solomoni Mwangamilo, amewasihi madereva waache tabia ya kuigiza ugonjwa wanaposimamishwa na askari kwa ajili ya ukaguzi.
Amesema kuwa madereva wanapaswa kushirikiana na vyombo vya usalama ili kuboresha hali ya usalama barabarani.
Huu ni mfano wa jitihada za serikali na kampuni za usafiri wa mitandaoni katika kuhakikisha kuwa madereva wanapata mazingira bora ya kazi na kuboresha usalama kwa abiria na madereva.
Kwa upande wake, Moja ya madereva wa Bolt nchini, Fay Mashallah, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Online Drivers Association (TODA), ameshukuru kwa serikali kwa kutambua mchango wa madereva na biashara ya mtandao, huku akieleza kuwa serikali imeangalia sekta hii kwa jicho la kipekee ili kuwasaidia madereva kuondokana na changamoto wanazokabiliana nazo.
"Jambo kubwa tunaloliomba ni kwa watu wa Bolt kutusaidia madereva kupata bima ya afya kwa bei nafuu, ambayo itawawezesha kupata matibabu pamoja na familia zao," ameongeza Fay Mashallah.




Comments
Post a Comment