UPENDO NKONE AWASHAURI WANAUME KUACHA KULA MAYAI
Upendo Nkone Atoa Ushauri wa Kiafya Kuhusu Ulaji wa Mayai ya Kisasa
Msanii wa nyimbo za Injili nchini, Upendo Nkone, ametoa ushauri kwa wazazi kuhusu lishe ya watoto wao wa kiume, akieleza athari zinazoweza kutokana na ulaji wa mayai ya kisasa.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Upendo ameonya kuwa mayai ya kisasa yanaweza kuchangia ukuaji wa matiti kwa wanaume kutokana na kemikali zinazotumika katika uzalishaji wake.
Amesisitiza umuhimu wa kula mayai ya kienyeji badala ya yale ya kisasa, akiwataka wanaume kuwa makini na vyakula wanavyotumia.
Mbali na hilo, amependekeza wanaume kula chipsi bila mayai kama njia mbadala ya kudhibiti athari hizo za kiafya.
Je, unakubaliana na ushauri wa msanii huyu? Wewe unapendelea mayai ya kienyeji au ya kisasa?

Comments
Post a Comment