NANCY SUMARI AMTAMBULISHA LYDIA CHARLE
Miss Tanzania na malkia wa Nguvu Nancy Sumari ameelezea safari ya mrembo Lydia Charles wakati anamkaribisha kabla ya kuzungumza safari yake ilipoanzia
Katika halfa ya kusheherekea Her Iniative iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuelezea safari ya Mkurugenzi wa taasisi huyo.
“Ingawa alikulia katika mazingira yenye rasilimali chache , alikuwa na dhamira kubwa kuliko wengi. Alisoma katika shule zenye vifaa duni.
Alikaa darasani bila walimu wa kutosha au maabara. Lakini bado alifanikiwa. Alikuwa mmoja wa wasichana watatu pekee kati ya 200 waliomaliza shule yake ya sekondari.”
“Alipofanikiwa, hakubaki na mafanikio yake peke yake. Alirudi kuwasaidia wengine. Alianza kuwaelekeza wasichana shuleni kwake. Kisha akajenga programu. Kisha akaunda shirika. Na sasa ni harakati.”
“Amefundisha wasichana vijana kote Tanzania ujuzi wa kidigitali, ujasiriamali, na uongozi. Si ili wawashukuru wengine, bali ili wawe tayari.
Tayari kumiliki sauti zao. Tayari kujenga biashara. Tayari kuketi kwenye meza yoyote na kuzungumza kwa mamlaka. Amejitahidi kwa ajili ya msichana aliyepuuzwa.”

Comments
Post a Comment