MOI YAPOKEA RUNINGA KUTOKA AZAM TV NAR UK
Dar es Salaam
TAASISI ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imepokea msaada wa runinga sita kutoka Kampuni ya Ving’amuzi ya Azam TV kwa kushirikiana na kampuni ya vifaa vya kielektroniki, Mr UK.
Msaada huo ulikabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya, amewashukuru wahisani hao kwa kujali ustawi wa jamii kupitia sehemu ya faida wanayoipata katika biashara zao.
![]() |
“Tunawashukuru sana Azam na Mr UK kwa kazi nzuri, kwa kutambua kwamba katika faida wanayoipata, wanarudisha kwa jamii hiyo hiyo,” amesema Dkt. Mpoki.
Ameongeza kuwa runinga hizo zitawasaidia wagonjwa kupata taarifa mbalimbali wakati wa matibabu yao katika taasisi hiyo.
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi wa MOI, Fidelis Minja, ametoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kusaidia taasisi hiyo kwa kutoa misaada mbalimbali, ikiwemo vifaa vya ukarabati wa jengo na miundombinu mingine.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mr UK, Shedrack Theophil, amesema kuwa si mara yao ya kwanza kutoa msaada wa aina hiyo na wataendelea kushirikiana na MOI ili kuleta faraja kwa wagonjwa.
Naye Mwakilishi kutoka Azam Tv Christina Korosso amesema kuwa wameanza na tv 6 kutoka kwa wadau wao, awali MoI waliomba tv kumi na sita tumeanza na hizi ni Imani yetu lengo litatimia na wagonjwa watapata faraja kwa kuangalia taarifa mbalimbali zinazoendelea nchini.



Comments
Post a Comment