STARTIMES YAZINDUA KAMPENI MPYA ZOTE NDANI.
Startimes Yazindua Kampeni Mpya ya Zote Ndani, Yaja na Ofa Maalum kwa Watazamaji Na Brighitte Davis, DAR ES SALAAM Kampuni ya Startimes imezindua kampeni mpya iitwayo Zote Ndani, ikiwapa watazamaji ofa maalum kupitia vipindi mbalimbali vya burudani, michezo, tamthilia na vipindi vya watoto. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi, Meneja Masoko wa Startimes, David Malisa, alisema kampeni hiyo inaleta vipindi vya kipekee sambamba na michezo ya kimataifa itakayorushwa kupitia kisimbuzi cha Startimes. “Tumejipanga kuonesha mechi kali kutoka Ligi Kuu ya England, La Liga na Bundesliga kupitia kisimbuzi chetu cha familia,” amesema Malisa. Mbali na michezo, Startimes pia imetambulisha tamthilia mbili kubwa kutoka Uturuki ambazo zimetafsiriwa kwa Kiswahili, ikiwemo Shadel T na Sagado Hadel Queen. Kwa upande wake, Godfrey Lugalabamu maarufu kama ‘Mc Gara B’, amesema msimu mpya wa Hello Mr. Right utarejea na maudhui mapya yenye msisimko. “Nimekuwa sehemu ya Hello Mr. Right tangu...