DIRECTOR P AIBUKA UPYA NA MET YOU, REE NDANI

Director P aibuka upya na Met You, Ree anogesha Msanii wa kizazi kipya na mwandaaji wa filamu mwenye asili ya Zambia na Kongo anayeishi nchini Canada, Patrick Lupasa 'Director P', amesema ngoma yake mpya, Met You imezidi kupenya kwa mashabiki zake barani Afrika tofauti na matarajio yake. Director P, amesema wimbo huo uliotoka hivi karibuni akimshirikisha mwimbaji Ree mwenye asili ya Jamaica na Canada alitarajia utajipatia umaarufu ughaibuni peke yake lakini mashabiki wa Afrika wamevutiwa nao zaidi.
Akizungumza na AMNEWSONLI, Director P amesema huo ni ujio wake mpya wenye maudhui ya mapenzi na sasa yupo kwenye maandalizi ya kufanya video ili aendelee kuwapa raha mashabiki zake.
"Wimbo huu unahusu jinsi upendo unavyosikika unapozungumzwa kwa lugha nyingi, Ree alileta ladha ya Karibea kwenye kurekodi Met You, na mimi nimeleta ladha ya Afrika Mashariki jambo lililofanya wimbo uvutie mno hii ni zaidi ya hadithi ya mapenzi na muunganisho wa kitamaduni," amesema Director P.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA