Posts

Showing posts from December, 2025

KAJALA AFUNGUKA UKWELI KUHUSU LULU KUJITOA KUNDI lA BIG SIX

Image
Kajala Afunguka: Ukweli wa Kuvunjika kwa Kundi la “Big Six” na Brighitter Msanii maarufu wa filamu nchini, Kajala Masanja, amefunguka na kuweka wazi ukweli kuhusu kuvunjika kwa kundi lao maarufu lililojulikana kama “Big Six”, lililowakutanisha wasanii wakubwa wa kike nchini. Akizungumza kuhusu kundi hilo, Kajala amesema ni kweli walikuwa wasanii sita waliounda umoja huo, ambao ulihusisha Wolper, Aunty Ezekiel, Wema Sepetu, Kajala Masanja, Irene Uwoya na Elizabeth Michael (Lulu). Kajala amesema mwanzo wa kuvunjika kwa kundi hilo ulianza pale Elizabeth Michael alipokuwa wa kwanza kujiondoa. Kwa mujibu wa Kajala, Elizabeth aliwaeleza wenzake kuwa alikuwa anatarajia kuingia katika maisha mapya ya familia. “Elizabeth alituambia kuwa hivi karibuni anatarajia kuitwa mama, hivyo alihitaji muda mwingi kuwa karibu na mume wake na watoto wake,” amesema Kajala. Baada ya maelezo hayo, Kajala anasema wanakundi walikubaliana kumpa nafasi Elizabeth Michael ili ajikite kwenye familia ya...

MWAKINYO KUWANIA HESHIMA YA TAIFA LEO WARE HOUSE

Image
BONDIA wa kimataifa Hassan Mwakinyo leo anaipeperusha bendera ya Tanzania katika pambano kubwa la Boxing on Boxing Day dhidi ya mpinzani wake kutoka Nigeria, Stanley Eribo, litakalofanyika Desemba 26, 2025, katika Ukumbi wa Warehouse, Masaki jijini Dar es Salaam. Mwakinyo, ambaye ameongoza zoezi la upimaji uzito pamoja na mabondia wengine, amesema yuko tayari kikamilifu kwa pambano hilo, akiahidi ushindi kwa Watanzania. Akizungumza mara baada ya zoezi hilo, Mwakinyo alisema amejiandaa kwa kiwango cha juu na yuko tayari kumpambana mpinzani wake kwa nguvu zote. “Nimejiandaa vizuri sana kwa pambano hili. Nimemuandaa mpinzani wangu kikamilifu na nawahakikishia Watanzania ushindi mkubwa. Nitaingia ulingoni kuipigania heshima ya taifa,” amesema Mwakinyo. Kwa upande wake, bondia wa Tanzania Hamadi Furahisha amesema maandalizi yake yamekamilika na yuko tayari kukabiliana na mpinzani wake kutoka Malawi, Hanock Phiri. “Najua ninampinzani mkali, lakini niko tayari kumpa pambano gumu ...

STARTIMES YAZINDUA AGLIMPSE OF CHINA MSIMU WA TANO

Image
StarTimes Yazindua “A Glimpse of China S5” Kuimarisha Uelewano kati ya China na Afrika KAMPUNI ya StarTimes imezindua rasmi msimu wa tano wa kipindi cha “A Glimpse of China”, mradi wa pamoja kati ya StarTimes na Idara ya Kimataifa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), unaolenga kuimarisha mawasiliano, uelewano na ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2020, kipindi hicho kimekuwa chanzo muhimu cha taarifa kinachoelezea safari ya China katika maendeleo ya kisasa, kikitoa picha halisi ya mabadiliko ya kiuchumi, kijamii na kiteknolojia yanayoendelea nchini humo. Msimu wa tano unaangazia kwa kina mafanikio ya China katika ubunifu wa kiteknolojia, uhuishaji wa vijijini, ustawi wa wananchi pamoja na juhudi za uhifadhi wa mazingira. Maudhui hayo yanawasilishwa kupitia simulizi fupi, zenye mvuto na zinazolenga kuwafikia kwa urahisi watazamaji wa Afrika. Kwa mujibu wa waandaaji wake, mtindo huo wa uwasilishaji unawezesha watazamaji ...

MCHANGE: HATUWEZI KUUZA UHURU WETU KWA WAZUNGU

Image
Mwenyekiti wa Kituo cha Wanahabari Watetezi wa Rasilimali za Taifa (MECIRA), Habibu Mchange, amekemea kauli za baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaodaiwa kutaka kuirudisha Tanzania katika mifumo ya kikoloni au ya utumwa mamboleo. Akizungumza leo Desemba 12, 2025, jijini Dar es Salaam, Mchange alisema kuwa kauli hizo zinahatarisha misingi ya uhuru wa nchi na maslahi mapana ya Watanzania. Ametoa msimamo huo wakati akijibu hoja za Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, kufuatia tamko lililotolewa na chama hicho hivi karibuni. Mchange amesisitiza kuwa, kama sehemu ya jamii ya Watanzania, MECIRA inawakumbusha wanasiasa wote kwamba maslahi ya Taifa yanapaswa kupewa kipaumbele kuliko maslahi ya vyama vyao.

TANZANIA AND U.S. MOVE TO FINALISE MAJOR INVESTMENT AGREEMENTS

Image
Her Excellency Dr. Samia Suluhu Hassan, President of the United Republic of Tanzania, today held talks with the Acting United States Ambassador to Tanzania, Andrew Lentz, at Chamwino State House to advance key areas of bilateral cooperation and reaffirm the shared commitment to a modern, mutually beneficial partnership. Ambassador Lentz—accompanied by the Counselor for Political and Economic Affairs—underscored Washington’s determination to reset the relationship and deepen economic, political, and security collaboration with Tanzania. “The United States is committed to a partnership based not on aid dependency but on shared prosperity,” Ambassador Lentz said. The discussions centred on ongoing negotiations involving major U.S.-linked strategic investments. Both sides acknowledged that talks on two flagship projects—the LNG Project and Tembo Nickel Project—are now in their final stages, pending formal signing. A third investment, the Mahenge Graphite Project, remains under acti...

TANZANIA NA MAREKANI ZASONGA MBELE KUKAMILISHA MAKUBALIANO MAKUBWA YA UWEKEZAJI

Image
RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo amefanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Andrew Lentz, katika Ikulu ya Chamwino, kujadili maeneo muhimu ya ushirikiano na kuimarisha dhamira ya pamoja ya kujenga ushirikiano wa kisasa na wenye manufaa kwa pande zote mbili. Balozi Lentz—aliyefuatana na Mshauri wa Masuala ya Kisiasa na Uchumi—amesisitiza dhamira ya Washington kuhuisha mahusiano na kuongeza kina la ushirikiano wa kiuchumi, kisiasa na kiusalama kati ya mataifa haya mawili. “Marekani imejitolea kujenga ushirikiano usiotegemea misaada, bali unaojengwa juu ya ustawi wa pamoja,” alisema Balozi Lentz. Mazungumzo yamejikita katika hatua za majadiliano ya miradi mikubwa inayoongozwa na kampuni za Marekani. Pande zote mbili zimekubaliana kuwa majadiliano ya miradi miwili ya kimkakati—Mradi wa LNG na Mradi wa Tembo Nickel—yamefikia hatua za mwisho kabla ya kutiwa saini rasmi. Uwekezaji wa tatu, Mradi wa Mahenge Graphite, unaen...

JONATHAN BUDJU AFUNGA MWAKA NA ITURI

Image
Jonathan Budju afunga mwaka na 'Ituri Amani' Na Bright Davis Mwimbaji nyota wa Injili kutoka nchini Canada, Jonathan Budju, ameweka wazi kuachia wimbo mpya hivi karibuni maalumu kuhamasisha amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Budju amejizolea umaarufu mkubwa kwenye muziki wa Injili pamoja na kujihusisha na masuala ya kijamii kupitia taasisi yake ya JB Foundation inayofanya kazi Afrika Mashariki. Akizingumza na gazeti hili, Jonathan amesema wimbo huo utatoka Disemba 19, akiwa ameshirikiana na waimbaji wa Ituri Gospel Artist na utaitwa Itune Amani. "Lengo ni kuendelea kuhamasisha amani Mashariki mwa DRC maeneo ya Ituri na Kivu, naamini wimbo utagusa wengi na kubadilisha maisha yao, nitatoa video na audio kwa pamoja katika platforms zangu zote za muziki," amesema Jonathan.

MSAMA AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA HOTUBA YENYE KUIMARISHA UMOJA NA AMANI

Image
Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa hotuba yake iliyojaa hekima na weledi aliyoitoa mbele ya wazee wa Dar es Salaam. Msama amesema hotuba hiyo imeonyesha uwazi, ufasaha na dhamira ya dhati ya kulinda amani na utulivu wa Taifa. “Hakuna kiongozi anayetamani wananchi wake wapate shida au mashaka. Kila kiongozi mwenye busara hutaka kuona watu wake wakiishi kwa upendo, umoja na amani,” amesema Msama. Akitolea mfano kitabu cha Wafalme katika maandiko matakatifu, Msama alisema ni muhimu kwa wananchi kuheshimu maagizo na mamlaka zilizopo kwa manufaa ya Taifa. Amesisitiza pia umuhimu wa vijana kuondoa hofu na kuendelea kuheshimu mihimili ya nchi ikiwemo Rais, Bunge na Mahakama. Aidha, Msama aliwataka wazee kuzungumza na watoto na wajukuu wao ili kuhakikisha hawaingii katika vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani ya nchi. “Methali inasema: ‘Asiyefunzwa na wazazi hufunzwa na ulimwengu’. Nawaomba wana...

MSIMU WA AFCON 2025 DSTV KUONESHA MECHI ZOTE

Image
Msimu wa AFCON 2025 wazinduliwa; DStv kuonesha mechi zote 52 ikiwemo za Taifa Stars DAR ES SALAAM:MSIMU wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) umezinduliwa rasmi, ambapo DStv imethibitisha kuonyesha mubashara mechi zote 52, ikiwemo mechi za kundi la Taifa Stars, hatua ambayo imepokelewa kwa shamrashamra na mashabiki wa soka nchini. Maandalizi ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika yanaendelea kupamba moto kuelekea kuanza kwake tarehe 21 Desemba 2025 hadi 18 Januari 2026 nchini Morocco. Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni “Wanafamilia Tuna Kikao Chimbo ni SuperSport”, Mkuu wa Masoko wa DStv Tanzania, Ronald Shelukindo, amesema dhamira ya DStv ni kuhakikisha Watanzania wanafuatilia kwa ukaribu michuano hiyo na kufurahia utamaduni wa soka la Afrika. Ameeleza kuwa "Mechi zitatolewa kwa lugha mbalimbali ikiwemo Kiswahili, Kiingereza, Kireno, Kifaransa na lugha za Kiafrika, ili kuhakikisha mashabiki wanapata burudani kwa uelewa mpana zaidi. Katika hatua y...

WAHITIMU UDSM WAHIMIZWA KULINDA AMANI

Image
Wahitimu UDSM Wahimizwa Kulinda Amani na Kutumia Elimu Kuendeleza Taifa Katika duru ya nne ya mahafali ya 55 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), jumla ya wahitimu 2,046 kutoka ngazi mbalimbali za masomo walitunukiwa vyeti na shahada, zikiwemo Shahada ya Uzamivu, Shahada ya Umahiri, Stashahada ya Uzamili, Shahada ya Awali, Stashahada na Astashahada. Sherehe hizo zilizofanyika leo Desemba 1, 2025 jijini Dar es Salaam, zilitawaliwa na ujumbe wa kuhimiza vijana kulinda amani, kuendeleza mshikamano na kuutumikia vyema ujuzi walioupata kwa manufaa ya Taifa. Akizungumza katika mahafali hayo, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa William Anangisye, alisema uhai, usalama na maendeleo ya Taifa lolote duniani yanategemea nguvu ya vijana, hivyo ni wajibu wao kutumia ujana kwa manufaa ya jamii. “Hakuna asiyejua mchango wa vijana katika Taifa. Tumieni ujana wenu kwa faida na msichoke kulinda amani popote mlipo,” amesema Prof. Anangisye. Amesisitiza kuwa elimu waliyoipata inapaswa kuone...