MSAMA AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA HOTUBA YENYE KUIMARISHA UMOJA NA AMANI

Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa hotuba yake iliyojaa hekima na weledi aliyoitoa mbele ya wazee wa Dar es Salaam. Msama amesema hotuba hiyo imeonyesha uwazi, ufasaha na dhamira ya dhati ya kulinda amani na utulivu wa Taifa.
“Hakuna kiongozi anayetamani wananchi wake wapate shida au mashaka. Kila kiongozi mwenye busara hutaka kuona watu wake wakiishi kwa upendo, umoja na amani,” amesema Msama. Akitolea mfano kitabu cha Wafalme katika maandiko matakatifu, Msama alisema ni muhimu kwa wananchi kuheshimu maagizo na mamlaka zilizopo kwa manufaa ya Taifa. Amesisitiza pia umuhimu wa vijana kuondoa hofu na kuendelea kuheshimu mihimili ya nchi ikiwemo Rais, Bunge na Mahakama.
Aidha, Msama aliwataka wazee kuzungumza na watoto na wajukuu wao ili kuhakikisha hawaingii katika vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani ya nchi. “Methali inasema: ‘Asiyefunzwa na wazazi hufunzwa na ulimwengu’. Nawaomba wananchi tarehe 9 watulie nyumbani na kuendelea na shughuli zao kama kawaida,” amesema. Vile vile, aliwataka viongozi wa dini kuepuka kufanya siasa madhabahuni na badala yake wahubiri injili kama alivyofanya Nabii Yona, akiwataka kutokutumiwa vibaya katika kuvuruga amani ya nchi.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA