MCHANGE: HATUWEZI KUUZA UHURU WETU KWA WAZUNGU
Mwenyekiti wa Kituo cha Wanahabari Watetezi wa Rasilimali za Taifa (MECIRA), Habibu Mchange, amekemea kauli za baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaodaiwa kutaka kuirudisha Tanzania katika mifumo ya kikoloni au ya utumwa mamboleo.
Akizungumza leo Desemba 12, 2025, jijini Dar es Salaam, Mchange alisema kuwa kauli hizo zinahatarisha misingi ya uhuru wa nchi na maslahi mapana ya Watanzania.
Ametoa msimamo huo wakati akijibu hoja za Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, kufuatia tamko lililotolewa na chama hicho hivi karibuni.
Mchange amesisitiza kuwa, kama sehemu ya jamii ya Watanzania, MECIRA inawakumbusha wanasiasa wote kwamba maslahi ya Taifa yanapaswa kupewa kipaumbele kuliko maslahi ya vyama vyao.

Comments
Post a Comment