MSIMU WA AFCON 2025 DSTV KUONESHA MECHI ZOTE
Msimu wa AFCON 2025 wazinduliwa; DStv kuonesha mechi zote 52 ikiwemo za Taifa Stars
DAR ES SALAAM:MSIMU wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) umezinduliwa rasmi, ambapo DStv imethibitisha kuonyesha mubashara mechi zote 52, ikiwemo mechi za kundi la Taifa Stars, hatua ambayo imepokelewa kwa shamrashamra na mashabiki wa soka nchini.
Maandalizi ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika yanaendelea kupamba moto kuelekea kuanza kwake tarehe 21 Desemba 2025 hadi 18 Januari 2026 nchini Morocco.
Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni “Wanafamilia Tuna Kikao Chimbo ni SuperSport”, Mkuu wa Masoko wa DStv Tanzania, Ronald Shelukindo, amesema dhamira ya DStv ni kuhakikisha Watanzania wanafuatilia kwa ukaribu michuano hiyo na kufurahia utamaduni wa soka la Afrika.
Ameeleza kuwa "Mechi zitatolewa kwa lugha mbalimbali ikiwemo Kiswahili, Kiingereza, Kireno, Kifaransa na lugha za Kiafrika, ili kuhakikisha mashabiki wanapata burudani kwa uelewa mpana zaidi.
Katika hatua ya kuongeza msisimko, kampuni za Canal na SuperSport zimethibitisha kuonyesha mubashara michuano yote ya CAF TotalEnergies Morocco 2025, ambayo inatajwa kuwa moja ya michuano mikubwa na yenye ushindani barani Afrika.
Taarifa ya CAF, Canal na SuperSport imeeleza kuwa Canal imepata haki za urushaji kwa nchi zinazotumia lugha za Kifaransa, Kiingereza, Kireno na lugha mbalimbali za Kiafrika, huku SuperSport ikihakikisha mashabiki wa Afrika Mashariki, Kusini na maeneo mengine wanapata burudani bila mipaka.
Shelukindo ameongeza:“Wateja wa DStv watafurahia mechi zote kupitia chaneli za SuperSport ikiwemo SS AFCON (Channel 222), SS Football Plus Nigeria (Channel 202) na SS Football Africa 2 (Channel 228). Chaneli hizi zinapatikana kuanzia kifurushi cha DStv Bomba kwa shilingi 27,500/- tu.”
Aidha, kutangazwa kwa lugha ya Kiswahili kutawawezesha mashabiki wa Afrika Mashariki kufuatilia michuano kwa ukaribu zaidi.
Nyota wa Afrika watakaotikisa AFCON 2025Mashabiki watatarajia kuona mastaa wakubwa akiwemo:Victor Osimhen (Nigeria), Mohamed Salah (Misri), Sadio Mané (Senegal), Ronwen Williams (Afrika Kusini), Riyad Mahrez (Algeria), Achraf Hakimi (Morocco)
"Ofa Maalum ya Sikukuu kutoka DStv, Dishi + dekoda: TSH 65,000/,Dekoda pekee: TSH 25,000/Wateja watafurahia burudani ya soka, filamu, tamthilia za ndani na nje ya nchi, katuni, vipindi vya familia na pia watapata huduma ya kulipa akaunti, kubaki hewani na kutiririsha (stream) popote walipo.
"Kwa ujumla, msimu huu DStv imesisitiza kaulimbiu yake:“Wanafamilia wote tuna kikao Chimbo ni SuperSport.”Mashabiki wanasubiri kwa hamu kuanza kwa michuano mikali ya AFCON 2025."amemaliza Shelukindo


Comments
Post a Comment