TRC YAOMBA RADHI HITILAFU NYINGINE YA TRENI
Shirika la Reli Tanzania (TRC) imewaomba radhi abiria waliosafiri na treni ya kawaida kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam Agosti Mosi,2024 kwa kuchelewa kuwasili kutokana na hitilafu ya kiufundi iliyotokea. Treni hiyo iliondoka Dodoma majira ya saa 2:15 usiku na kupata hitilafu katika eneo la Mtaa wa Mshikanano, Kata ya Kihonda Mkoani Morogoro. Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano ,Jamila Mbarouk ilieleza kuwa hitilafu za kiufundi zilitokea majira ya saa 4:33 usiku nakushughulikiwa kwa muda wa takribani saa moja na kusababisha treni hiyo ya abiria kutoka Dodoma kuchelewa kuwasili Dar Es Salaam kwa wakati uliopangwa. Aidha Shirika lilisema kuwa tremi iliyobeba viongozi na wananchi wengine walitoka Dodoma saa moja usiku baada ya kushiriki sherehe za uzinduzi wa SGR waliwasili Dar es Salaam kwa muda uliopangwa bila hitilafu yoyote. “TRC inazingatia usalama wa abiria kabla na wakati wa safari ili kuepusha ...