Posts

Showing posts from December, 2024

NABII MALISA AMSHUKURU DKT SAMIA KWA KURUHUSU HUDUMA ZA KIROHO

Image
  CHUNGAJI wa Kanisa la Madhabau ya Hatma, Nabii Clear Malisa, amemshukuru Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan kwa serikali yake kwa kutoa uhuru wa kuabudu bila kuchagua. Malisa ameyasema hayo mapema leo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuzungumzia mkesha mkubwa unaotarajia kufanyika leo kanisani kwake  Ubungo Kibangu. "Rais Samia amekuwa na ushirikiano mkubwa kwetu viongozi wa dini, tunamshukuru kutobagua dhehebu lolote"amesema Malisa. Hata hivyo, Malisa ameutabiri mwaka 2025 utakuwa mwaka wa neema zaidi kwa Taifa la Tanzania katika nyanja ya uchumi  ikiwemo kupanda kwa shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola za Kimarekani. Pia ameongeza kwa kutoa utabiri anaofanya, kiongozi huyo kwa kiroho amesema ni Utashi ambao Mungu amempa na kuhaidi kutoa utabiri juu ya mambo mbalimbali ikiwemo uchaguzi mkuu wa hapo mwakani kupitia kwenye mkesha utakaofanyika kanisani leo. Aidha Nabii  Malisa amewataka watanzania kipindi hiki cha...

TGNP WASHEHRREKEA MIAK 30 YA BEIJINGNA DIRA 2050

Image
 Na Brighitte Davis  MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) umesherehekea miaka 30 ya Beijing katika kongamano la wanawake na uongozi Dar es Salaam leo huku ukihimiza umuhimu wa wanawake kuendelea kujitokeza kwa wingi  katika uchaguzi mkuu ujao kugombea nafasi mbalimbali za uongozi. Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Lilian Liundi amesema wanayo furaha kuona uchaguzi wa serikali za mitaa namna wanawake wengi wameitikia na kushika nafasi za wenyeviti akisema anaamini data zitaendelea kuongezeka. Amesema takwimu zinaonesha asilimia 6.5 tu ya wanawake waliochaguliwa kwenye uchaguzi wa 2019 ni madiwani, na kwamba asilimia 2.1 ya wanawake waliochaguliwa Tanzania nzima walishika nafasi ya wenyeviti wa vijiji, 6.7 wenyeviti wa vitongoji na 12.6 wenyeviti wa mtaa, takwimu hizo zikionesha hawajafikia asilimia wanazotazamia. “Tunayo imani kwamba kuna uchaguzi wa mwaka ujao data zitakuwa tofauti lakini hapa tunayo mifano ya wanawake waliopasua miamba kwenye uchaguzi...

EWURA YAPIGA MARUFUKU KUKATWA MAJI WEKENDI

Image
  Na Brigitte Davis MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imesema ni  marufuku kwa mamlaka za maji nchini kukata maji mwishoni mwa wiki kwasababu kufanya hivyo ni kama unyanyasaji. Hayo yamesemwa Dar es Salaam leo  na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma  wa EWURA, Titus Kaguo kwenye semina kwa Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya habari nchini (JOWUTA). Amesema kitendo cha mtu kukatiwa maji kuanzia Ijumaa saa 12  jioni au Jumamosi na Jumapili hairuhusiwi kiutaratibu na kiudhibiti.  "Mtu anayefanya hivyo asifanye tena kwasababu anaweza kuchukuliwa hatua za kisheria ili kuwajibika kwa kile anachokifanya,"amesema. Amesema Watanzania wajenge utamaduni wa kusoma mikataba ya huduma kwa wateja kwani inawapa wajibu wa wao wafanye nini na mamlaka zifanye nini. Kaguo amesema mamlaka zimekuwa hazihamasishi mikataba hiyo ili Watanzania wasiibuke na kuanza kudai haki zao. Pia, amesema  kuwa wakati wa usomaji wa mita za maji, ofisa wa mamlaka y...

URBAN BY CITY YASHINDA TUZO YA HOTEL BORA

Image
  Urban by CityBlue, Dar es Salaam Yashinda Tuzo ya Consumer Choice kwa Hoteli Bora ya Huduma Bora na Mwangaza nchini Tanzania (4-Star) Urban by CityBlue, Dar es Salaam, sehemu ya portifolio maarufu ya CityBlue Hotels, imetunukiwa Tuzo ya Consumer Choice kwa Hoteli Bora ya Huduma Bora na Mwangaza nchini Tanzania (4-Star). Tuzo hii ya heshima inatambua muundo wa kipekee wa hoteli, uzoefu wa kipekee wa wageni, na dhamira ya kutoa huduma za kiwango cha kimataifa. Iko katikati ya jiji lenye vionjo vya maisha ya Dar es Salaam, Urban by CityBlue imekuwa ikisherehekewa kwa uzuri wake wa kisasa, vifaa vya kisasa, na ukarimu wa Kitanzania. Kutambuliwa kwa hoteli hii kunasisitiza kujitolea kwake katika kuweka viwango vipya katika tasnia ya huduma za kifahari katika kanda hii. Khalil Hamadi, mkurugenzi wa kampuni inayosimamia Urban by CityBlue, Dar es Salaam alisema: “Tunajivunia kuona mafanikio haya, ambayo yanatufanya kuendelea kuhamasika na kupiga hatua kubwa zaidi katika ubora wa huduma n...

KAMPUNI YA JAN INTERNATIONAL IMETUNZA WATEJA WAKE

Image
Kampuni ya kuuza magari ya Jan international Ltd imewatunza wateja wake  wanne gari, pikipiki, jokofu na simu ikiwa ni sehemu  ya kurudisha kwa jamii na kuwashukuru kwa kuwaunga mkono. Washindi hao wametokana na droo waliyoichezesha juzi baada ya kampeni ya kuendesha zoezi hilo iliyofanyika kwa zaidi ya mwezi mmoja kwa kukusanya karasi walizopewa wajaze watu wote waliokwenda kununua magari kwenye kampuni hiyo. Washindi hao ni Edwin Godwin alishinda gari aina ya Harrier anaconda, Harun Rajabu alishinda pikipiki, Agnes Nganile alishinda jokofu na tv inchi 52 na Issa Tambuu alishinda simu aina ya Iphone 16 pro max. Mshindi wa gari Godwin alisema ametoka kununua gari mwezi uliopita na wakati anapewa karatasi ajaze hakuamini alikuwa anaona kama anapoteza muda wake akiamini huwa wanachaguliwa na kueleza furaha yake baada ya kuona ni kweli. "Mwanzoni sikuamini kumbe ni kweli, nashukuru sana Jan kwa kututhamini wateja wao msimu huu wa sikukuu mmetutia moyo na kutuhamasisha kuendelea k...

DULLA MBABE KUSAFISHA NGUMI MAUGO

Image
 Na Brighitte Davis BONDIA wa ngumi za kulipwa, Abdallah Pazi 'Dullah Mbabe' amesema anaenda kumstafisha  ngumi mpinzani wake, Mada Maugo katika pambano la 'Taji la Mama Samia' litakalofanyika Desemba 26, mwaka huu. Dullah Mbabe atapanda ulingoni kuzichapa pambano kuu  dhidi ya Maugo la raundi nane, uzito wa juu ( kilo 76) litakalofanyika Muleba Mkoani Kagera. Akizungumza Dar es Salaam leo katika uzinduzi wa pambano hilo, Dullah Mbabe amesema baada ya kukaa kimya muda mrefu bila kupanda ulingoni awamu hii amejipanga kuja kuleta mapinduzi  katika ngumi kwa kumchakaza mkongwe huo mwenzake. "Nimejipanga  salama kiafya naendelea vizuri, naenda katika vita dhidi ya Mada Maugo, baada ya kupoteza mapambano machache ikiwemo la Erick Katompa naenda kuonyesha kazi mkoani Kagera,"amesema. Amewatoa hofu wakazi wa Muleba na kuwataka wakae mkao wa kula wategemee mambo mazuri kutoka kwake kwani siku hiyo atamuonyesha kazi kwa sababu mara ya kwanza alimtengua  kiuno awamu ...

WAAJIRI WAIMIZWA KUONGEZA NA KUZINGATIA UTU MAHALA PA KAZI

Image
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza waajiri nchini kuongeza umakini na kuzingatia misingi ya utu mahali pa kazi ili iwe motisha na chachu kwa watumishi kuongeza ubunifu na ufanisi kazini. Dkt. Biteko amesema hayo wakati akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Phillip Mpango katika usiku wa Tuzo kwa mwajiri Bora wa mwaka 2024 ambapo Kampuni ya bia nchini (TBL) imeibuka mshindi wa jumla ikifuatiwa Kampuni ya Barick Gold huku Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA ikishika nafasi ya tatu.  Amewapongeza waandaaji wa tuzo hizo na kuwataka kupanua wigo wa makundi ya ushiriki huku akisisitiza umuhimu wa utoaji wa motisha mahala pa kazi ili watumishi waongeze ari ya kufanya kazi kwa viwango na ubora wajuu.  “ mwajiri anachokihitaji kwa mwajiriwa ni muda na ujuzi wake basi. Hivyo, waajiri ongezeni umakini na utu mahali pa kazi na mkifanya hivyo, waajiriwa ambao wanatumia muda mwingi kazini, wataongeza ubunifu na ufanisi ...

MFALME MZEE YUSUPH KUPEWA MAUWA YAKE DISEMBA 8

Image
  MSANII  wa muziki wa taarabu nchini Mzee Yusuph ‘Mfalme wa Taarabu’ anatarajia kupewa mauwa yake kwa kuupigania muziki huo katika tamasha  la muziki huo linalotarajia kufanyika Disemba 8, 2024 jijini Dar es Salaam. Akizungumza na habarileo Mzee Yusuph alisema kuwa watu wengi wanapenda kuwapa watu mauwa yao wakiwa wametangulia mbele za haki kwake ni tofauti. “Napewa mauwa yangu na ninayapokea kwa sababu najuwa kuwa nastaili maua haya, nimefanya muziki wa taabu kwa muda Mwingi lakini hakuna mwanaume yupo muda mrefu kwenye huu muziki zaidi yangu. "Mashabiki zangu na watu mbalimbali wanaopenda kazi zangu niwaombe na niwakaribishe katika tamasha maalumu la kunipa mauwa yangu kwa Mchango wangu kwenye tasnia ya muziki wa taarabu. “Kuna muda muziki wa taarabu ulikuwa kama umelala hakuna anayeweza kuuamsha kama Mzee Yusuph niwaambie tu watu wajitokeze kwa wingi Disemba 8 waone muziki unavyozaliwa upya huku nikipokea mauwa yangu.”alisema Mfalme Mzee Yusuph Aidha ameongeza kuwa at...