PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU
Wanandoa watashauriwa kuwa na mitoko ya pamoja kujua mwenzio anapenda kula nini kuvaa na kunywa ili kuendelea kudumisha ndoa yao, Ndoa bora ni ushirikiano, siyo mashindano. Akizungumza mwaandaaji wa Usiku huo wa wanandoa The Pinnacle of Mentorship & Excellence Award (PIMEA) Dkt Christine Mbelwa amesema Lengo la Usiku wa Wanandoa nikuwakutanisha na kubadilishana mawazo kuhusiana na kukumbusha baadhi ya mambo ya ndoa. "Moja ya majukumu ambayo Mungu amenikabidhi mimi pamoja na mume wangu ni kujenga ndoa na mahusiano imara kupitia uandishi wa vitabu, semina, makongamano na mafundisho mbalimbali. "Usiku wa Wanandoa ni moja ya jukwaa kuu tunalotumia kwa lengo la kuboresha, kuponya na kuokoa ndoa. Tunawakusanya wanandoa pamoja, kuwapa mafundisho ya vitendo ana kwa ana, kuruhusu maswali na kutoa majibu ya moja kwa moja. Amesema Zaidi ya mafundisho, wanandoa hupata nafasi ya kufurahi pamoja kwa kushiriki vinywaji, michezo na burudani mbalimbali. Shughuli hi...