HELLO CHINESE S2 LANGO LA KIMATAIFA LA UTADUNI WA KICHINA

Lango la Kimataifa la Utamaduni wa Kichina
Kwa kuangalia wigo na upana wa mawasiliano ya kiutamaduni, kipindi cha “Hello Chinese” kimevuka mipaka ya kijiografia na lugha, na kuufanya utamaduni wa Kichina kufika nje ya mipaka na hatimae kuufikia ulimwengu. Msimu huu kipindi hiki kimeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Kituo cha Elimu na Ushirikiano wa Lugha (Wizara ya Elimu ya Jamhuri ya Watu wa China) na StarTimes. Kipindi hiki kinawapa fursa watu kutoka nchi na tamaduni mbalimbali nafasi ya kuwasiliana na kuelewa utamaduni wa Kichina, hivyo kimepelekea kupanua kwa kiasi kikubwa wigo wa usambazaji wake na kuuruhusu ulimwengu kuona China yenye taswira mbalimbali na yenye nguvu na uhai. Kufungua siri za kujifunza KichinaIdara ya "Usomaji na Uandishi wa Kichina" imeandaa njia za kujifunza kulingana na hatua ya kila mwanafunzi. Kipindi hiki cha “Hello Chinese” kinawaongoza wanafunzi hatua kwa hatua—kujifunza matamshi ya herufi, mikato yake, na hatimae kuunda sentensi kamili. Mbinu hii inawawezesha wapenzi wengi wa lugha ya Kichina kuelewa, kujifunza, na kutumia herufi za Kichina kwa ufasihi, na pia kuwafanya waone usahihi na uhalisia wa maelezo katika lugha ya Kichina, hivyo kuwafanya waone kujifunza Kichina ni jambo la kufurahisha.Kuongeza Upatikanaji:
Matangazo kupitia vituo mbalimbaliIli kuendana na ratiba tofauti za watazamaji, inarusha matangazo yake kupitia vituo mbalimbaliST Sino Drama: itaonesha kipindi hiki kuanzia Jumatano hadi Jumapili saa 16:50 GMT, na kurudiwa saa 5:50 GMT na saa 11:50 GMT kwenye siku inayofuata.ST Guide E: itaonesha kipindi hiki kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa saa 17:00 GMT, na kurudiwa saa 11:00 GMT na saa 22:00 GMT kwenye siku inayofuata. “Hello Chinese” siyo tu kipindi, bali pia ni daraja linalounganisha dunia na China. Kupitia kipindi hiki, unaweza kuhisi undani wa utamaduni wa Kichina, kujifunza lugha ya Kichina yenye haiba, na unaweza kuvutiwa na China. Tunatarajia ushiriki wako na kuanza pamoja safari hii, safari yenye mvuto!

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA