KIZIMKAZI HOSPITALI MATIBABU BURE CHAKULA BURE WAGONJWA HAWATAKI KURUDI NYUMBANI

Wakazi wa Kizimkazi wajivunia kituo cha afya chenye hadhi ya hospitali huduma bure kwa wote Na Brigitter
WAKAZI wa Kizimkazi Mkunguni, Zanzibar, wameeleza furaha na fahari yao kutokana na uwepo wa Kituo cha Afya kilichojengwa kwa viwango vya kisasa chenye hadhi ya hospitali, kinachotoa huduma zote bure kwa wananchi. Kituo hicho kilizinduliwa rasmi tarehe 3 Januari 2025 na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk Jakaya Mrisho Kikwete, na kilianza kutoa huduma tarehe 1 Februari 2025. Tangu kuanzishwa kwake, kituo hicho kimekuwa kikihudumia idadi kubwa ya wakazi, kutoka watu 70 kwa siku mwanzoni hadi kufikia zaidi ya watu 3,000 kwa sasa.
Akizungumza na Amonlin wakati wa ziara ya wahariri waliokuwa wakikagua miradi ya maendeleo visiwani Zanzibar, Daktari Mkuu wa kituo hicho, Dkt. Tamimu Hammad Said, amesema kuwa huduma zote zinatolewa bila malipo yoyote. "Wagonjwa wanaolazwa wanapata huduma zote bure, ikiwemo chakula. Kina mama wanaojifungua pia wanahudumiwa bila gharama yoyote. Tunajivunia kutoa huduma bora kwa wakazi wote wa eneo hili na maeneo ya jirani," amesema Dkt. Tamimu.
Ameongeza kuwa kituo hicho kimekuwa msaada mkubwa kwa jamii na kimepunguza kwa kiasi kikubwa vifo vya wajawazito na watoto, sambamba na kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya za msingi. Wakazi wa Kizimkazi nao wametoa pongezi kwa serikali kwa uwekezaji huo wa afya, wakieleza kuwa huduma bora na za karibu zimeleta unafuu mkubwa kwao, hasa kwa wale wasio na uwezo wa kusafiri umbali mrefu kutafuta matibabu.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Othuman Ally amesema wanajivunia kuwepo kwa Kituo cha Afya chenye hadhi ya Hospital na kutoa huduma bure kwa wananchi.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA