MSHINDI WA MPIRA MREFU KUONDOKA NA GARI
Mashindano ya gofu ya Kombe la Mkuu wa Majeshi ‘NMB CDF Trophy’ yanatarajiwa kufanyika Oktoba 4-6,2024, huku mchezaji atakayefanikiwa kupiga ‘hole in one’ atapewa zawadi ya gari aina ya Toyota Harrier yenye thamani ya sh milioni 70 na kwenda kupumzika hoteli ya Serena . Gari hiyo imekabidhiwa leo Septemba 27,2024 na Meneja Mkuu wa Toyota kwa kwa Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu Lugalo, jijini Dar es Salaam, Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo. Akizungumzia mashindano hayo yatakayofanyika katika viwanja vya klabu Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu Luwongo amesema mchezaji atayepiga ‘hole in one’ atakabidhiwa gari yake muda huo huo na italipiwa kila kitu. Ameeleza lengo mashindano kuwa ni kumuenzi mlezi wa klabu ambaye ni Mkuu wa Majeshi ambapo kwa sasa ni Jenerali Jacob Mkunda na siku ya kufunga ndiye atakuwa mgeni rasmi. Amesema kuwa pamoja kumuenzi Mkuu wa Majeshi lakini pia ni muendelezo wa sherehe za kuzaliwa kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambayo kila mwaka huadh...