Posts

Showing posts from April, 2026

AZAM TV YAZINDUA KAMPENI YA "USALAMA DAIMA" KUOKOA MAISHA YA MADEREVA BODABODA

Image
Azam Media Yazindua Kampeni ya “Usalama Daima” Kuokoa Maisha ya Madereva Bodaboda Kampuni ya Azam Media Limited imezindua rasmi kampeni ya usalama barabarani yenye kauli mbiu “Usalama Daima, Azam TV Milele”, ikiwa na lengo la kutoa elimu na ujuzi kwa watumiaji wa vyombo vya moto, hususan madereva wa bodaboda, ili kupunguza ajali zinazoweza kuepukika. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika Kimara, Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Afisa Uendeshaji Mkuu wa Azam Media Limited, Yahya Mohamed, alisema kuwa kampeni hiyo inalenga kuwajengea uwezo madereva kwa kuwapatia mafunzo maalum pamoja na nyenzo muhimu za usalama barabarani. Ameeleza kuwa utekelezaji wa kampeni hiyo utaendelea katika maeneo mbalimbali nchini hadi kufikia mwezi Septemba mwaka huu, huku madereva bodaboda wakihusishwa moja kwa moja ili kuhakikisha wanapata elimu ya matumizi salama ya barabara pamoja na umuhimu wa vifaa kinga. Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Divisheni ya Maso...

JACKLINE WOLPER: SAFARI YA NYOTA ILIYOJAA UMAARUFU, MAPENZI, UJASIRIAMALI NA ULEZI

Image
KWA zaidi ya muongo mmoja sasa, jina la Jackline (Jacqueline) Wolper Massawe limekuwa likitawala kurasa za burudani nchini Tanzania. Ni jina linalobeba taswira ya uigizaji mahiri, mitindo ya kuvutia, mafanikio ya kibiashara, pamoja na maisha binafsi yaliyogusa hisia za wengi. Mwanzo wa Safari ya Kifani Jacqueline Wolper alizaliwa Desemba 1988 mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro. Safari yake ya sanaa haikuanza jukwaani wala mbele ya kamera, bali ndani ya saluni ya nywele alipokuwa akifanya kazi za kujipatia riziki. Bahati ilimgonga mwaka 2007 alipotambuliwa na nguli wa filamu za Bongo Movies, Lucy Komba, aliyemuona kipaji chake na kumpa nafasi ya kwanza katika filamu Ama Zako Ama Zangu. Hapo ndipo safari ya Wolper ilipoanza rasmi. Kupitia bidii, nidhamu na kipaji, Wolper aliendelea kung’ara katika filamu nyingi zikiwemo Family Tears, Red Valentine, Kipenzi Changu, Chaguo Langu, Surprise, Candy, Taxi Driver na nyingine zaidi ya 30. Leo, anahesabika kama mmoja wa waigizaji wanaw...

NANCY SUMARI: MREMBO ANAYELETA MAPINDUZI SEKTA YA ELIMU KALIMANI APP

Image
Nancy Sumari: Kutoka Urembo hadi Mapinduzi ya Elimu ya Kidijitali kwa Watoto Viziwi WENGI wanamkumbuka Nancy Sumari kama mrembo aliyewahi kutwaa taji la Miss Tanzania 2006 na baadaye kutangaza jina la nchi kimataifa kupitia Miss World Africa. Lakini leo, anajitokeza upya si kwa urembo bali kwa mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu jumuishi kupitia teknolojia. Kupitia kampuni yake ya JengaHub, Nancy amezindua rasmi Kalimani App, jukwaa la kidijitali linalolenga kuwasaidia watoto wenye ulemavu wa kusikia kujifunza kwa urahisi zaidi, popote walipo. Teknolojia Inayogusa Maisha Akizungumza na Amonline jijini Dar es Salaam, Nancy alisema kuwa programu hiyo imetengenezwa kwa kusaidia watoto viziwi. “Kalimani App inatumia lugha ya alama ya Tanzania kufundisha kusoma, kuandika na kuhesabu, pamoja na kuwajengea watoto ujuzi wa kidijitali,” ameeleza. Programu hiyo inatarajiwa kuanza kutumika katika shule za kawaida na maalum katika mikoa sita nchini, hatua inayolenga kupu...

ODEMBA AJA NA SAUTI YA MITINDO WANAUME JITOKEZENI

Image
Odemba aja na ‘Sauti ya Mitindo’, awaasa wanaume kujitokeza DAR ES SALAAM:MISS na Mwanamitindo wa kimataifa Miriam Odemba ametangaza kuanzisha jukwaa jipya la mitindo lijulikanalo kama Sauti ya Mitindo, litakalolenga kukuza vipaji vya wanamitindo wa kiume na wa kike nchini. Akizungumza jijini Dar es Salaam, Odemba amesema jukwaa hilo ni sehemu ya kurejesha mchango wake katika tasnia ya urembo baada ya kunufaika na fursa mbalimbali tangu alipoanza safari yake. Amesema anatoka Temeke District na kwamba mafanikio yake yametokana na juhudi pamoja na msaada wa watu mbalimbali waliomuamini tangu mwanzo. Kwa sasa Odemba ni mama wa mtoto mmoja wa kike, Iris Piedimonte, ambaye amesema anaonesha kipaji cha urembo na michezo ya tenisi. Aidha, alimshukuru Rita Paulsen kwa mchango wake mkubwa, akieleza kuwa tangazo alilowahi kutunukiwa na mwanamama huyo lilimfungulia milango ya mafanikio. Odemba alikumbusha kuwa mwaka 1997 aliibuka mshindi wa Miss Temeke na baadaye kushinda Miss Tan...

CRDB BANK YANGARA TUZO KIMATAIFA

Image
BENKI ya CRDB Bank imepata heshima ya kutambuliwa kimataifa baada ya kushinda tuzo ya benki bora katika utoaji wa huduma za kifedha kwa wateja maalum (Private Banking) kutoka kwa Euromoney, hatua inayodhihirisha ukuaji wa sekta ya fedha nchini Tanzania. Akizungumza leo Aprili, 21 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa kupokea tuzo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dk. AbdulMajid Nsekela, amesema mafanikio hayo yanaweka Tanzania katika nafasi nzuri ya kuaminika zaidi kimataifa. Ameeleza kuwa ushindi huo unasaidia kuongeza imani kwa wawekezaji wa ndani na nje. “Tuzo hii inaonyesha uimara wa mifumo ya kifedha nchini, hali inayochochea wawekezaji wengi zaidi kuichagua Tanzania kama sehemu salama ya kuwekeza na kuhifadhi mitaji yao,” amefafanua Dk. Nsekela. Aidha, amesema mafanikio hayo yanatokana na usimamizi madhubuti wa sekta ya fedha unaofanywa kwa ushirikiano kati ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Wizara ya Fedha Tanzania, ambazo zimeweka sera rafiki zinazokuza ubo...

CRDB YAZINDUA MSIMU WA PILI WA GRADUATE TRAINESS KUANDAA VIJANA VIONGOZI

Image
DAR ES SALAAM Katika juhudi za kukuza vipaji vya vijana na kuandaa viongozi wa baadaye katika sekta ya fedha, Benki ya CRDB imezindua rasmi msimu wa pili wa programu ya Graduate Trainees, hatua inayolenga kuwawezesha vijana wenye uwezo kuingia na kung’ara katika soko la ajira. Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Abdulmajid Mussa Nsekela, alisema kuwa CRDB inaendelea kuwekeza kwa vijana wenye uwezo, ubunifu na maono mapana ili kuimarisha uongozi wa sasa na wa siku zijazo. Amefafanua kuwa programu hiyo ya miaka mitatu inalenga kutafuta na kukuza vipaji kutoka ndani na nje ya nchi, ikiwahusisha vijana kutoka Tanzania pamoja na mataifa ambayo benki hiyo inafanya shughuli zake, ikiwemo Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), pamoja na maeneo mengine kama Dubai. Kwa mujibu wa Nsekela, zaidi ya maombi 4,800 yalipokelewa mwaka huu, lakini baada ya mchakato mkali wa ushindani, vijana 26 pekee ndio waliofanikiwa kuchaguliw...