TUNU HALISI ASHINDA BASATA RISING STAR AWARDS

BASATA Yamtangaza Tunu Halisi, Atatunga Wimbo wa AFCON 2027
Na Brigitte DAR ES SALAAM:BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limemtangaza msanii chipukizi Tunu Halisi kuwa mshindi wa shindano la Basata Rising Star Awards, huku akipangiwa jukumu la kutunga wimbo maalum kwa ajili ya michuano ya AFCON 2027.
Akizungumza na Habari Leo, Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA, Edward Buganga, amesema kuwa miongoni mwa nyimbo tatu zitakazorekodiwa na wasanii watakaopatikana kupitia programu hiyo, mmoja utahusu mashindano ya AFCON 2027.
Buganga ametoa kauli hiyo katika hafla ya kukabidhi tuzo iliyofanyika katika Kituo cha Utamaduni cha Ufaransa jijini Dar es Salaam, ambapo Tunu Halisi ametangazwa mshindi wa mwezi wa tatu kupitia mpango wa kuibua na kukuza vipaji vya wasanii wachanga.
Kwa upande wake, mshindi huyo, Tunu Halisi, ameeleza shukrani zake kwa BASATA na Watanzania kwa kumuunga mkono, akiahidi kuja na kazi bora zitakazogusa nyoyo za wengi.
Naye Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Addo November, amesisitiza umuhimu wa programu ya Basata Rising Star Awards, akieleza kuwa imekuwa chachu ya kukuza vipaji na kuinua tasnia ya muziki nchini.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA