Posts

WASHIRIKI 20 BSS WATINGA KAMBINI

Image
Washiriki 20 watinga kambini Bongo Star Search DAR ES SALAAM: WASHIRIKI 20 kutoka Kenya Uganda Congo na Tanzania waliochaguliwa kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania pamoja na nchi kadhaa za Afrika Mashariki na Kati wamewasili rasmi kambini katika ufukwe wa Ndege Beach jijini Dar es Salaam kuanza safari yao ya kutwaa ushindi vipaji la Bongo Star Search (BSS). Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Azam Media jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Benchmark Production na muandaaji wa shindano hilo, Rita Paulsen, amesema msimu wa mwaka huu umebeba ushindani mkubwa zaidi kutokana na kiwango cha juu cha vipaji vilivyojitokeza wakati wa usaili. Rita amesema kundi hilo linajumuisha Watanzania 10, Wakenya watatu, Waganda wawili, Wakongo watatu, pamoja na kundi moja la wachezaji wa dansi na mchekeshaji mmoja kutoka Mbeya. “Washiriki wa mwaka huu wana viwango vya juu sana. Kuna tofauti kubwa ukilinganisha na misimu iliyopita, jambo linaloonesha ukuaji wa sekta ya buruda...

HAKUNA MWENYE UHAKIKA WA KUIONA 2030

Image
“Hakuna Mwenye Uhakika wa Kuiona 2030” Steve Nyerere Atoa Onyo kwa Wanasiasa MSANII na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao, Steve Nyerere, amekemea tabia ya baadhi ya watu kuanza kujadili na kupanga viongozi wa uchaguzi wa mwaka 2030, akisema hakuna mwenye uhakika wa kufika mwaka huo isipokuwa kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Akizungumza kuhusu mwenendo wa kisiasa unaoendelea nchini, Steve Nyerere amesema vijana wengi wa Kitanzania hawana muda wa kufikiria nani atakuwa Rais mwaka 2030, bali wanahitaji kuona maendeleo ya kweli yanayogusa maisha yao ya kila siku. “Watu wanaanza kupanga viongozi wa 2030 kana kwamba wana uhakika wa kuifikia siku hiyo. Maisha ni mafupi na yote yako mikononi mwa Mungu,” amesema Steve Nyerere. Aidha, amesema vijana wengi wanachohitaji kwa sasa ni ajira, elimu bora, mazingira mazuri ya biashara pamoja na huduma muhimu za kijamii, badala ya siasa zisizoleta manufaa kwa wananchi. Steve Nyerere amesisitiza kuwa viongozi na wadau wa siasa w...

IZO MOTORS YAZINDUA BETRI ZA KISASA AJIRA KWA VIJANA

Image
IZO Motors Yazindua Betri za Kisasa, Zaajiri Zaidi ya Vijana 50 Kampuni ya IZO Motors Company Limited imesema imeendelea kuchangia kukuza ajira kwa vijana baada ya kutoa ajira kwa zaidi ya vijana 50 kupitia shughuli zake za uuzaji na usambazaji wa betri pamoja na matairi kwa jumla na rejareja. Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 12, 2026, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Izo Mahenge, alisema kampuni hiyo imezindua rasmi betri mpya za izo Battery, ambazo zimetengenezwa kwa teknolojia ya kisasa na ubora wa hali ya juu kwa matumizi mbalimbali. Mahenge amesema betri hizo zimeandaliwa kwa uwezo mkubwa wa kuhifadhi na kutoa nguvu, huku zikidumu kwa muda mrefu katika mazingira tofauti ya matumizi. “Tumetengeneza betri hizi kwa kuzingatia viwango vya ubora wa hali ya juu ili kuhakikisha mtumiaji anapata bidhaa yenye ufanisi mkubwa. Biashara ni ushindani, hivyo tumejikita zaidi katika ubora na utofauti wa bidhaa yetu,” amesema Mahenge. Aidha, alieleza kuwa betri hizo zinazali...

CRDB BANK FOUNDATION WAENDELEA KUWEZESHA VIJANA GO GREEN NA IMBEJU

Image
Benki ya CRDB kwa kushirikiana na CRDB Foundation imeendelea kuonesha dhamira yake ya kuwawezesha vijana kiuchumi baada ya kuchagua vijana zaidi ya 458 kuingia katika awamu ya kwanza ya mafunzo maalumu ya biashara na teknolojia kupitia programu ya Go Green na Imbeju. Programu hiyo inalenga kuwajengea vijana uwezo katika biashara, huduma za kidijitali, uwekezaji pamoja na uchumi wa kijani ili kuwawezesha kujiajiri na kuchangia maendeleo ya taifa kupitia shughuli endelevu zinazolinda mazingira. Akizungumza kuhusu programu hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Foundation, Tully Esther Mwambapa, amesema vijana waliofanikiwa wamepatikana baada ya kupitia mchakato wa uchambuzi uliofanywa na jopo la wataalamu kutoka taasisi mbalimbali za serikali na sekta binafsi. Mwambapa amesema vigezo vilivyotumika ni pamoja na ubunifu wa biashara, uwezo wa mradi kujiendesha pamoja na mchango wake katika kuhifadhi mazingira. Kwa upande wao, baadhi ya vijana walionufaika na mpango huo wameeleza kuwa...

AZAM YAENDELEA KUTOA ELIMU YA USALAMA DAIMA WILAYA YA TEMEKE

Image
Kakulu: elimu ya usalama itaokoa Maisha ya wananchi Na Brigitte DAR ES SALAAM: MBUNGE wa Jimbo la Mbagala, Burchard Kakulu amesema elimu ya usalama barabarani inayotolewa kwa waendesha bodaboda ni muhimu katika kuokoa maisha ya wananchi pamoja na kuchochea maendeleo ya taifa. Kakulu amesema hayo kwenye uzinduzi wa mwendelezo wa kampeni ya Usalama Daima chini ya Azam Mediai iliyofanyika katika viwanja vya Zakhiem Mbagala, Temeke Dar es Salaam, kampeni inayolenga kufika mitaani, wilayani, mikoani na nchi nzima kuhamasisha usalama barabarani kwa madereva wa bodaboda na watumiaji wa barabara kwa ujumla. “Katika maisha hata ungekuwa na maono mazuri, ndoto kubwa na mawazo mazuri kiasi gani, kama hauko salama kiafya havina maana yoyote. Elimu wanayopewa vijana hawa maofisa usafirishaji sio tu muhimu kwao bali hata sisi watumia huduma,” amesema Kakulu. Kwa upande wake, Meneja wa Mawasiliano na Mahusiano wa Azam Media⁠, Christina Korosso amesema kampeni hiyo inalenga kuhakikisha el...

CRDB BANK YAKUTANA NA WANA HISA YAWEKA WAZI MAFANIKIO YAO

Image
CRDB Banki Yakutana na Wawekezaji, Yaweka Wazi Mafanikio ya 2025 na Mwelekeo wa 2026 Benki ya CRDB Bank imekutana na wawekezaji pamoja na wadau mbalimbali kwa lengo la kujenga ushirikiano imara na kuimarisha mahusiano ya kimkakati yatakayochochea ukuaji endelevu wa sekta ya fedha na uchumi kwa ujumla. Kupitia kongamano hilo, benki hiyo iliwasilisha mafanikio ya utendaji wake kwa mwaka 2025 pamoja na mwelekeo wake wa mwaka 2026, huku ikiendelea kusisitiza dhamira yake ya kuwahudumia wadau kwa ubora zaidi. Akizungumza baada ya kongamano hilo, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Profesa Neema Mori, amesema benki hiyo imeendelea kutekeleza mpango mkakati wake kwa mafanikio, huku mwaka huu ukiwa ni mwaka wa nne wa utekelezaji wa mkakati huo. “Tumeleta pamoja wadau wetu ili kuwaeleza tumetoka wapi na tunakwenda wapi. Tumewasilisha mafanikio ya utendaji wetu wa mwaka 2025 pamoja na mwelekeo wetu wa mwaka 2026, lakini pia tumeshirikisha maono yetu ya kuendelea kuwahudum...

MWILI WA KIJANA JAMES TEMBA AMBAYE ALIUWAWA NA KUKATWA KICHWA WAAGWA KKKT TABATA

Image
Mwili wa kijana James Temba ambaye aliuawa kisha mwili wake kukatwa kichwa, ukiwa ndani ya Kanisa la KKKT Tabata Magengeni jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ibada ya kumuaga marehemu. Mwili wake ulikutwa kwenye Mto Msimbazi, eneo la Kipawa, Ilala jijini Dar es Salaam ukiwa hauna kichwa ambapo anatarajiwa kusafirishwa kwenda Moshi mkoani Kilimanjaro.