HAKUNA MWENYE UHAKIKA WA KUIONA 2030

“Hakuna Mwenye Uhakika wa Kuiona 2030” Steve Nyerere Atoa Onyo kwa Wanasiasa MSANII na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao, Steve Nyerere, amekemea tabia ya baadhi ya watu kuanza kujadili na kupanga viongozi wa uchaguzi wa mwaka 2030, akisema hakuna mwenye uhakika wa kufika mwaka huo isipokuwa kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Akizungumza kuhusu mwenendo wa kisiasa unaoendelea nchini, Steve Nyerere amesema vijana wengi wa Kitanzania hawana muda wa kufikiria nani atakuwa Rais mwaka 2030, bali wanahitaji kuona maendeleo ya kweli yanayogusa maisha yao ya kila siku.
“Watu wanaanza kupanga viongozi wa 2030 kana kwamba wana uhakika wa kuifikia siku hiyo. Maisha ni mafupi na yote yako mikononi mwa Mungu,” amesema Steve Nyerere. Aidha, amesema vijana wengi wanachohitaji kwa sasa ni ajira, elimu bora, mazingira mazuri ya biashara pamoja na huduma muhimu za kijamii, badala ya siasa zisizoleta manufaa kwa wananchi. Steve Nyerere amesisitiza kuwa viongozi na wadau wa siasa wanapaswa kuelekeza nguvu zao katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi badala ya kuanza kampeni za mapema zisizo na tija kwa taifa. Kauli hiyo imeibua mjadala miongoni mwa wananchi na vijana wengi wakisema kuwa kipaumbele kikubwa kinapaswa kuwa maendeleo na ustawi wa maisha ya Watanzania.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA