CRDB BANK YAKUTANA NA WANA HISA YAWEKA WAZI MAFANIKIO YAO

CRDB Banki Yakutana na Wawekezaji, Yaweka Wazi Mafanikio ya 2025 na Mwelekeo wa 2026
Benki ya CRDB Bank imekutana na wawekezaji pamoja na wadau mbalimbali kwa lengo la kujenga ushirikiano imara na kuimarisha mahusiano ya kimkakati yatakayochochea ukuaji endelevu wa sekta ya fedha na uchumi kwa ujumla.
Kupitia kongamano hilo, benki hiyo iliwasilisha mafanikio ya utendaji wake kwa mwaka 2025 pamoja na mwelekeo wake wa mwaka 2026, huku ikiendelea kusisitiza dhamira yake ya kuwahudumia wadau kwa ubora zaidi.
Akizungumza baada ya kongamano hilo, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Profesa Neema Mori, amesema benki hiyo imeendelea kutekeleza mpango mkakati wake kwa mafanikio, huku mwaka huu ukiwa ni mwaka wa nne wa utekelezaji wa mkakati huo.
“Tumeleta pamoja wadau wetu ili kuwaeleza tumetoka wapi na tunakwenda wapi. Tumewasilisha mafanikio ya utendaji wetu wa mwaka 2025 pamoja na mwelekeo wetu wa mwaka 2026, lakini pia tumeshirikisha maono yetu ya kuendelea kuwahudumia wadau wetu kwa ubora zaidi,” amesema Profesa Mori. Aidha, amesema benki hiyo imeendelea kuweka mkazo katika kujenga ushirikiano na wabia mbalimbali pamoja na kuwekeza kwa watumishi wake ili kuongeza ufanisi wa huduma na kuimarisha ushindani katika sekta ya fedha.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Abdulmajid Nsekela, amesema kongamano hilo limekuwa sehemu muhimu ya kujadili mikakati ya pamoja ya kukuza uhimilivu wa benki hiyo ili kuendelea kutoa huduma bora kwa Watanzania na kuchochea mabadiliko chanya ya kiuchumi.
Amesema ushirikiano kati ya benki, wawekezaji na wadau mbalimbali utaendelea kuwa chachu ya kujenga uchumi imara na wenye ushindani nchini.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA