Posts

Showing posts from June, 2025

AJIRA ZAIDI YA 2000 ZATENGENEZWA MAONESHO YA AJIRA YA CHINA NCHINI TANZANIA 2025

Image
Wizara ya Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa China wanaofanya shughuli zao nchini, imeingia makubaliano ya kutoa ajira kwa zaidi ya vijana 2,000 wa Kitanzania, ikiwa ni juhudi za kutatua changamoto ya ajira nchini. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu),Ridhiwani Kikwete, amesema kuwa ushirikiano huo unalenga kuwawezesha vijana kufahamu aina ya ajira zilizopo kupitia kampuni mbalimbali za Kichina zinazofanya kazi nchini Tanzania. "Kwanza kabisa, kijana anapaswa kufahamu aina ya ajira zilizopo na kuweza kuchangamkia nafasi hizo kupitia makampuni yaliyo tayari kuajiri. Lengo kuu ni kupunguza changamoto ya ajira na kuwawezesha vijana wetu," amesema Ridhiwani Kikwete. Aliongeza kuwa Wizara inasisitiza ushiriki wa vijana kwa wingi ili kunufaika na nafasi hizo, ambapo baadhi ya mchakato wa mahojiano (in...

MSAMA ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA UKONGA

Image
Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama leo Juni 29, 2025 amefika katika Ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala na kuchukua Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga. Amekabidhiwa Fomu hiyo na Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Ilala, Chief Sylvester Yaredi.

MSAMA VIDEO INAYOSAMBAA INALENGO LA KUNICHAFUA NI VITA YA UBUNGE

Image
Mkurugenzi wa Msama Promotions Alex Msama amewaomba watanzania kupunguza Habari zinazozagaa mitandaoni kuwa amefukuzwa kwenye nyumba yake ya Upanga Dar es Salaam. Amesema kuwa "Video zinazosambaa zinatumika na watu wasio na Nia njema na Mimi na Wana lengo la kunichafua hasa kipindi cha vita za ubunge"amesema Alex Msama

AHMED ASAS AKUTANA NA ASKOFU ROMANUS JIMBO LA IRINGA

Image
Jumatatu yenye baraka kukutana na Mhashamu Baba Askofu Romanus Elamu Mihali, wa Jimbo Kuu Katoliki la Iringa. Furaha kubwa kukutana na kiongozi wa kiroho mwenye hekima, unyenyekevu na moyo wa Upendo.

KIPINDI KIPYA CHA KATUNI ZA 3D NDANI YA STARTIMES

Image
Hivi karibuni, vijana na watoto wamepata dirisha jipya na la kusisimua la kuifahamu tamaduni za Kichina kupitia kipindi kipya cha katuni za 3D kiitwacho Let’s Go Beijing, kilichotayarishwa na StarTimes. Kipindi hiki kinatangazwa kwa sasa katika vituo mbalimbali vya televisheni barani Afrika na kimefanikiwa kuvutia fikra na hisia za watoto kwa kuwasilisha urithi wa kihistoria na kitamaduni wa Beijing kwa njia ya kuvutia na ya kuburudisha. Mpangilio wa kipindi hiki umegawanyika katika vipengele vitatu vya kusisimua: “The Grand Canal Explorer” — safari ya kuvutia inayowapeleka watazamaji katika safari ya kurudi nyuma kwenye historia kupitia Mfereji Mkuu wa Beijing-Hangzhou, ikiwapa fursa ya kuona uzuri na historia ya eneo Kaka’s Silk Road Adventure inaleta mtazamo wa kipekee unaoongeza mvuto wake wa kitamaduni kwa kuwaleta pamoja watangazaji kutoka Afrika na wahusika wa katuni watoto. Muundo huu wa “mtoto mwongoza safari + mtangazaji wa Kiafrika” huleta mazingira ya joto n...

STEVE NYERERE HESHIMU MAMLAKA UHURU WA MAONI UNA UKOMO

Image
Anaandika @stevenyerere2 “Mheshimiwa Rais @samia_suluhu_hassan, hongera sana kwa ziara yako wilayani Meatu. Haiwezekani kila mtu akajiona ana haki ya kusema chochote, mahali popote, na wakati wowote. Watu wanasahau kuwa uongozi ni hekima, busara na uvumilivu – lakini kwa wajinga na wasioelewa, huona kama wako juu ya sheria. Haiingii akilini mtu kusimama mbele ya Rais wake, mbele ya Mwenyekiti wake wa chama, na kusema anammdai. Huo siyo uungwana wala heshima. Watu wa aina hiyo wapo wengi Mheshimiwa Rais, lakini leo umeonyesha sura yako halisi kama Kiongozi Mkuu wa nchi na Mwenyekiti wa Chama. Umeonyesha makali yako – hongera sana. Ninaamini sasa watajipanga upya, lakini kamwe hawataweza. Tufike mahali tutambue kuwa kuna dola, kuna mamlaka, kuna serikali – hakuna aliye juu ya dola. Huwezi kuzuiwa kusema, lakini hakuna uhuru usio na mipaka. Wamezidi sana!”– Steve Nyerere.

JUKWAA LA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI WAMUUNGA MKONO RAIS SAMIA

Image
JUKWAA la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam limetangaza maazimio saba ya kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu. Wanawake hao pia wameeleza dhamira yao ya kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha Rais Samia anarejea madarakani kwa ushindi wa kishindo, wakisema amekuwa kinara wa maendeleo na mtetezi wa wanawake nchini. Akizungumza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 15, Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Rehema Sanga amesema wanawake hao wameungana kwa sauti moja kutokana na imani yao kwa uongozi wa Rais Samia. “Tunaona fahari kuwa na Rais mwanamke ambaye amefungua fursa za kiuchumi kwa wanawake, amesimamia amani, na ameleta mageuzi ya kweli katika sekta mbalimbali. hatuna sababu ya kutoyatangaza mafanikio haya na kuhakikisha anaendelea kuongoza taifa letu,” amesema Rehema. Akizungumzia maazimio hayo, Rehema amesema yamelenga kuonyesha mshikamano kueneza m...

MJUMBE WA KAMATI KUU CCM NAMELOK SOKOINE APOKELEWA KWA KISHINDO ARUSHA

Image
Mjumbe wa Kamati Kuu CCM, Namelok Sokoine Apokelewa kwa Kishindo Arusha, Aahidi Kulinda Heshima Aliyopewa na Mwenyekiti Dkt. Samia Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Mheshimiwa Namelok Edward Sokoine, leo tarehe 14 Juni 2025 amepokelewa kwa shangwe kubwa na umati wa wananchi wa Mkoa wa Arusha. Akizungumza baada ya mapokezi hPayo, Mheshimiwa Sokoine alimshukuru kwa dhati Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa heshima kubwa aliyoitoa kwa wana Arusha na Wilaya ya Monduli kwa ujumla. “Ninamshukuru sana Mwenyekiti wetu Dkt. Samia kwa kutupa heshima hii kubwa. Na mimi kwa niaba ya wana Arusha, naahidi kulinda heshima hii na kuhakikisha tunaendeleza jitihada za kuleta maendeleo kwa wananchi wetu,” alisema Sokoine. Aidha, aliwaomba wananchi wote wa Arusha kusimama pamoja na CCM na Mwenyekiti wao Dkt. Samia katika uchaguzi ujao, akisisitiza kuwa kazi kubwa ipo Oktoba. “Kazi ni moja tu — Oktoba tunasimama na mama,” alisisitiza Mhe. Sokoine ...

KUENDESHA NA MAFANIKIO :SIFARI ISIYO YA KAWAIDA

Image
Kuendeshwa na Mafanikio: Safari Isiyo ya Kawaida Wanasema bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi, lakini kwenye biashara bahati inakujaka pale unapo piga mahesabi sahihi nakuwekeza jitihada” anasema Laurence Mollel, dereva wa teksi aliyewahi kuwa mfanyakazi wa kawaida kwenye kampuni ya bima, jijini Arusha. Mwaka 2021, Mollel aliacha kazi yake ya ofisini bila mpango madhubuti wa biashara — ila tu alijua moja: kazi ya kukaa nyuma ya dawati haikuwa ikimsaidia kifedha.“Kazi ilikuwa ya kurudia rudia, muda ulikuwa mgumu, na mshahara haukuwa ukikidhi maisha,” anasema Mollel. Alichukua uamuzi wa kubadilisha maisha: alinunua gari lililotumika na akajiunga na Indrive. “Nilitaka udhibiti wa muda na kipato changu. Ride-hailing ilinipa nafasi hiyo,” alieleza. Mwaka mmoja baadaye, maisha yake yalikuwa tofauti. Alinunua gari la pili na kulikodisha kwa dereva mwingine, akiongeza kipato zaidi. Alipoanza kuona magari ya watalii kama Land Cruiser yakikatiza barabara za Arusha, ndoto yake...

VIONGOZI WA DINI ACHENI SIASA MAKANISANI HUWEZI KUTUMIKIA MABWANA WAWILI

Image
Viongozi wa Dini Waaswa Kuheshimu Mamlaka, Waepuke Kuingiza Siasa Kanisani Dar es Salaam Viongozi wa dini nchini, hususan wachungaji, wamehimizwa kuheshimu mamlaka zilizopo kwa kutambua kuwa mamlaka hizo zimewekwa na Mungu, na hivyo waepuke kutumia nyumba za ibada kama majukwaa ya kisiasa. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, muandaaji wa Tamasha la Pasaka na Krismasi, Alex Msama, alisema ni muhimu kwa watumishi wa Mungu kutofautisha kati ya kazi ya kiroho na masuala ya kisiasa. "Huwezi kutumikia mabwana wawili. Kama umeamua kuingia kwenye siasa, basi acha uchungaji. Vivyo hivyo, ukiwa mchungaji, acha siasa," amesema Msama. Amesisitiza kuwa majukwaa ya kiroho yanapaswa kutumika kwa ajili ya kuhubiri Injili, kuwahimiza watu kuacha maovu, na kuwaongoza kumrudia Mungu ili taifa liendelee kuwa na upendo na amani. Akirejea maandiko matakatifu katika Warumi 13, Msama alisema wale wanaohasi mamlaka waliowekwa wanamhasi Mungu mwenyewe. "Maand...

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA

Image
"Ukosefu wa Fedha, Uongozi Dhaifu Vyatajwa Kuvuruga Uhai wa Taasisi za Vijana" Dar es Salaam. Ukosefu wa fedha, masharti magumu kutoka kwa wafadhili, kutokuwa na maarifa ya kutosha ya uendeshaji wa taasisi na rasilimali zake ni miongoni mwa changamoto zinazochangia taasisi nyingi zinazoanzishwa na vijana kufa kabla ya kufikia malengo yake. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Her Initiative, Lydia Charles, katika hafla ya kuhitimisha mafunzo ya uongozi kwa taasisi 20 zinazoongozwa na vijana kupitia programu ya Adaptive Leadership Program chini ya mradi wa Ustawi Lab. Amesema changamoto hizo zimekuwa kikwazo kikubwa kwa vijana wanaotamani kuleta mabadiliko chanya katika jamii kupitia taasisi zao, jambo lililowasukuma kuanzisha mafunzo hayo ya uongozi ili kuwajengea uwezo wa kimfumo na kimkakati. "Tuliona kuna haja ya kuimarisha uwezo wa viongozi vijana kwa kuwapatia mbinu za kukabiliana na changamoto mbalimbali, kuboresha mifumo ya taasisi zao...