MJUMBE WA KAMATI KUU CCM NAMELOK SOKOINE APOKELEWA KWA KISHINDO ARUSHA
Mjumbe wa Kamati Kuu CCM, Namelok Sokoine Apokelewa kwa Kishindo Arusha, Aahidi Kulinda Heshima Aliyopewa na Mwenyekiti Dkt. Samia
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Mheshimiwa Namelok Edward Sokoine, leo tarehe 14 Juni 2025 amepokelewa kwa shangwe kubwa na umati wa wananchi wa Mkoa wa Arusha.
Akizungumza baada ya mapokezi hPayo, Mheshimiwa Sokoine alimshukuru kwa dhati Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa heshima kubwa aliyoitoa kwa wana Arusha na Wilaya ya Monduli kwa ujumla.
“Ninamshukuru sana Mwenyekiti wetu Dkt. Samia kwa kutupa heshima hii kubwa. Na mimi kwa niaba ya wana Arusha, naahidi kulinda heshima hii na kuhakikisha tunaendeleza jitihada za kuleta maendeleo kwa wananchi wetu,” alisema Sokoine.
Aidha, aliwaomba wananchi wote wa Arusha kusimama pamoja na CCM na Mwenyekiti wao Dkt. Samia katika uchaguzi ujao, akisisitiza kuwa kazi kubwa ipo Oktoba.
“Kazi ni moja tu — Oktoba tunasimama na mama,” alisisitiza Mhe. Sokoine huku akishangiliwa na wananchi waliohudhuria.




Comments
Post a Comment