Posts

Showing posts from February, 2026

HASHEEM THABEET ASHINDA URAIS TBF

Image
Mchezaji Nyota wa Basketball Hasheem Thabeet amechaguliwa kuwa rais wa chama cha mpira wa kikapu tanzania (TBF) baada ya kushinda kinyanganyiro icho katika uchaguzi uliofanyika Dodoma siku ya jumamosi tarehe 28 Katika uchaguzi huo Hasheem Thabit ameibuka mshindi baada ya kupata kura 34 kati ya 60 zilizopigwa na wajumbe Wengine walioshinda katika nafasi kinyangario icho ni pamoja Makamu wa rais - mohamed Kisui Katibu mkuu -Mwenza Fiston Kabinda Kaimu katibu mkuu- Saimon Mirondo Hashem kwa sasa anachezea team ya kikapu ya Dar City ambayo inatarajiwa kucheza fainali za BAL Kwenye michezo itakayochezwa kuanzia March 27 huko South Africa..

KWA AZAM PESA NA BURUDANI AZAM TV KIMEWAKA SOKO NI MOKO

Image
Azam yazindua kampeni ya “Soko Limewaka”: Burudani bora na uhifadhi salama wa fedha kwa bei nafuu KATIKA jitihada za kusaidia jamii kutunza na kuhifadhi fedha zao kwa usalama zaidi sambamba na kupata burudani bora, kampuni ya Azam TV kwa kushirikiana na Azam Pesa imezindua kampeni maalum ijulikanayo kama “Soko Limewaka”. Kampeni hiyo inalenga kuwaunganisha wananchi katika mfumo mmoja rahisi unaowezesha kupata burudani ya kiwango cha juu huku wakifurahia huduma za kifedha kwa njia ya simu zao. Kupitia mpango huu, wateja wanapata fursa ya kutazama michezo, katuni, muziki na makala mbalimbali ndani ya Azam TV kwa gharama nafuu. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Meneja Mauzo wa Azam TV, Sebastian Mwaikambo, alisema kampeni ya Soko Limewaka imewaunganisha wateja wote katika sehemu moja, akisisitiza kuwa kila aliyewasha kifaa chake amekuwa sehemu ya mabadiliko hayo makubwa. Aliongeza kuwa lengo kuu ni kumfikia kila mwananchi na kuhakikisha wote wanafurahia burudani...

AZAM TV KIMEWAKA SOKO NI MOKO

Image
AZAM TV yatangaza rasmi uzinduzi wa kampeni yetu mpya ya Kimewakaa Soko ni moko! Lengo letu ni kuiweka AzamTV kama kituo kimoja cha burudani bora kabisa. Pamoja na hayo kuongeza thamani kwa wateja wetu AzamTV kushirikiana na kampuni dada AzamPay. Ushirikiano huu ni zaidi ya promosheni ni hatua muhimu kuelekea kuwapa Watanzania huduma bora zaidi za burudani na malipo kwa urahisi, ili wateja wetu wafurahie huduma zetu bila usumbufu. Na ushirikiano huu kwa pamoja tunauita "Kimewakaa! SokoNiMoko... Cha Juu Zaidi!" AzamPesa. Malengo ya Kampeni Kwanza, tunataka kuimarisha nafasi ya Azam TV kama nyumba ya burudani bora, mpira, sinema, tamthilia, vipindi vya watoto na familia, vyote sehemu moja. Pili, tunalenga kuwapa wateja urahisi wa malipo, kwa kuwahamasisha wateja wa AzamTV kutumia AzamPesa kwa malipo ya haraka, salama, na yenye urahisi zaidi. Tatu, tunawakaribisha watumiaji wa AzamPesa kujiunga na AzamTV, kupitia ofa maalum, cashback, na vivutio vinavyofanya buruda...

CRDB NA TUME YA MADINI WAINGIA MAKUBALIANO

Image
Makubaliano Maalum ya Kihistoria Yafungua Milango ya Mitaji, Teknolojia na Ukuaji wa Wachimbaji Wadogo Dar es Salaam Katika hatua ya kihistoria na mageuzi ya Sekta ya Madini nchini, Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini leo Februari 23, 2026 imesaini Makubaliano Maalum na Benki ya CRDB yatakayorahisisha upatikanaji wa huduma za fedha kwa wachimbaji wadogo wa madini. Akizungumza katika hafla hiyo ya kihistoria iliyofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es Salaam, Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde (Mb) ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa utashi na uongozi thabiti unaoendelea kuibadilisha Sekta ya Madini kuendelea kuwavutia wawekezaji . Waziri Mavunde amesisitiza kuwa hatua hiyo ni mwendelezo wa juhudi za makusudi za Serikali kujenga mazingira rafiki kwa wachimbaji wadogo wa madini kwa kuimarisha uchimbaji, biashara, kuongeza ufanisi, na kuimarisha mchango wa sekta katika Pato la Taifa (GDP)...

BODI YA MIKOPO YAUNGANA NA CRDB KUKUZA UCHUMI WA VIJANA KIDIGITALI

Image
Brighitte DAR ES SALAAM Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Tanzania imesema imeimarisha ushirikiano na sekta binafsi kwa lengo la kuongeza ushiriki wa vijana katika uchumi wa kidijitali na kuwajengea uwezo wa kujiajiri. Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Upangaji Mikopo wa bodi hiyo, Dkt. Peter Mmari, amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya kuunganisha taasisi za umma na sekta binafsi ili kuongeza tija katika uwekezaji wa rasilimali watu. “Muungano huu unalenga kuboresha huduma na kuongeza tija ya uwekezaji katika rasilimali watu,” amesema Dkt. Mmari. Ameeleza kuwa tangu kuanzishwa kwa bodi hiyo mwaka 2004, zaidi ya Watanzania milioni 1.1 wamenufaika na mikopo yenye thamani ya takribani Sh trilioni 8.5, ikiwa ni sehemu ya uwekezaji mkubwa wa Serikali katika kujenga nguvu kazi yenye ujuzi na weledi. Kwa mujibu wa Dkt. Mmari, maboresho ya mifumo ya kidijitali pamoja na usimamizi madhubuti yameongeza makusanyo ya marejesho hadi zaidi ya S...

JKCI NA MOI KUFANYA KAMBI YA SIKU TANO BURE ARUSHA LUTHERAN

Image
JKCI na MOI Waanzisha Kambi Maalum ya Uchunguzi wa Mifupa na Mishipa ya Fahamu Bure Arusha Brighitte DAR ES SALAAM HOSPITALI ya Arusha Lutheran Medical Center (ALMC), inayosimamiwa na Taasisi ya Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), inatarajia kufanya kambi maalum ya siku tano ya uchunguzi wa magonjwa ya mifupa na mishipa ya fahamu bila malipo. Kambi hiyo itafanyika kuanzia Februari 23 hadi 27, 2026 katika Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Center (ALMC), mkoani Arusha, ikiwa na lengo la kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuwapatia huduma za kibingwa karibu na maeneo yao. Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI katika hospitali hiyo, Dkt. Tatizo K. Waane, amesema kuwa madaktari bingwa watano watashiriki katika kambi hiyo, huku wakitarajia kuhudumia wagonjwa takribani 200 kwa siku. “Tunawaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kupatiwa uchunguzi na ushauri wa kitaalamu kuhusu afya zao. Tu...

BENKI YA CRDB YAZINDUA KAMPE YA KIMPANGO WAKO 2026

Image
Benki ya CRDB Yazindua Kampeni ya 'Benki Kimpango Wako' kwa Mwaka 2026, Yasherehekea Mafanikio ya Mwaka 2025 Baada ya mwaka wa 2025 kuwa na ufanisi mkubwa katika biashara, ambapo Benki ya CRDB ilipata faida ya zaidi ya shilingi trilioni 1.04, leo benki hiyo imezindua kampeni ya mwaka 2026 inayoitwa ‘Benki Kimpango Wako’. Kampeni hii inalenga kuboresha huduma kwa wateja kwa kupunguza muda wa kukamilisha miamala na kuwapa wateja uwezo wa kujihudumia kwa urahisi kutoka mahali popote duniani, wakati wowote wanapotaka. Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, aliwashukuru wateja, wawekezaji, wabia wa kimkakati, na wadau wote kwa imani waliyonayo kwa benki hiyo. Alieleza kuwa mafanikio ya mwaka 2025 yamechangiwa na ushirikiano mzuri kutoka kwa wateja binafsi, wajasiriamali, mashirika na serikali. Nsekela alisema, “Mwaka jana tumepata faida kubwa na tutaendelea na azma yetu ya kuboresha maisha ya Watanzania na uchu...

UNDP YAWAZAWADIA WANAFUNZI 20 SH MILIONI 70 STUDENT FOUNDERS FELLOWSHIP

Image
UNDP Tanzania Yawazawadia Wanafunzi Wajasiriamali 20 Zaidi ya Shilingi Milioni 70 Kupitia Awamu ya Pili ya Youth Ignite Student Founders Fellowship Wanafunzi wajasiriamali ishirini kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini wamepatiwa zawadi za fedha taslimu zaidi ya Shilingi milioni 70 kufuatia shindano la uwasilishaji wa mawazo ya biashara lililoandaliwa chini ya mpango wa Youth Ignite Student Founders Fellowship – Awamu ya Pili. Mpango huo unatekelezwa kupitia Programu ya FUNGUO iliyo chini ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) nchini Tanzania, kwa ufadhili wa pamoja wa Serikali ya Uingereza kupitia Ofisi ya Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo (FCDO), Umoja wa Ulaya (EU) na Serikali ya Finland. Shindano hilo liliwakutanisha wanafunzi 30 kutoka taasisi mbalimbali za elimu ya juu nchini, waliowasilisha mawazo bunifu ya biashara yenye mchango chanya kwa jamii mbele ya jopo la majaji. Tukio hilo limeelezwa kuwa hatua muhimu katika kuimarisha ujas...