KWA AZAM PESA NA BURUDANI AZAM TV KIMEWAKA SOKO NI MOKO

Azam yazindua kampeni ya “Soko Limewaka”: Burudani bora na uhifadhi salama wa fedha kwa bei nafuu
KATIKA jitihada za kusaidia jamii kutunza na kuhifadhi fedha zao kwa usalama zaidi sambamba na kupata burudani bora, kampuni ya Azam TV kwa kushirikiana na Azam Pesa imezindua kampeni maalum ijulikanayo kama “Soko Limewaka”. Kampeni hiyo inalenga kuwaunganisha wananchi katika mfumo mmoja rahisi unaowezesha kupata burudani ya kiwango cha juu huku wakifurahia huduma za kifedha kwa njia ya simu zao. Kupitia mpango huu, wateja wanapata fursa ya kutazama michezo, katuni, muziki na makala mbalimbali ndani ya Azam TV kwa gharama nafuu. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Meneja Mauzo wa Azam TV, Sebastian Mwaikambo, alisema kampeni ya Soko Limewaka imewaunganisha wateja wote katika sehemu moja, akisisitiza kuwa kila aliyewasha kifaa chake amekuwa sehemu ya mabadiliko hayo makubwa.
Aliongeza kuwa lengo kuu ni kumfikia kila mwananchi na kuhakikisha wote wanafurahia burudani bora kwa bei nafuu. “Tunaongeza thamani kwa wateja wetu kwa kuwapatia mambo makubwa ndani ya kifurushi kimoja,” amesema.
Kupitia kampeni hiyo, mteja anayelipa Sh28,000 hupandishwa hadi kifurushi cha Sh35,000, huku aliyelipa Sh19,000 akipandishwa hadi kifurushi cha Sh28,000. Aidha, mteja wa kifurushi cha Sh35,000 hurudishiwa Sh7,000 na kupata kifurushi cha Sh28,000, hali inayowezesha wananchi wengi zaidi kupata huduma bora kwa kipindi cha hadi miezi mitatu.
Kwa upande wake, Mkuu wa Masoko wa Azam Pesa, Hussein Simba, alisema kampeni hiyo inalenga kujenga mfumo mmoja ulio rahisi kwa wateja, kuongeza matumizi ya huduma za kifedha kidijitali na kuchochea ukuaji wa uchumi, iwe sokoni au nyumbani. Alisisitiza kuwa kupitia miamala ya simu, Watanzania sasa wanaweza kufurahia burudani kwa wote kwa urahisi na usalama zaidi, akiongeza kuwa Soko limewaka kwa kiwango cha juu zaidi.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA