Posts

Showing posts from November, 2024

WAAJIRI WAIMIZWA KUONGEZA NA KUZINGATIA UTU MAHALA PA KAZI

Image
  WAAJIRI WAIMIZWA  KUONGEZA  NA KUZINGATIA UTU MAHALA PA KAZI Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza waajiri nchini kuongeza umakini na kuzingatia misingi ya utu mahali pa kazi ili iwe motisha na chachu kwa watumishi kuongeza ubunifu na ufanisi kazini. Dkt. Biteko amesema hayo wakati akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Phillip Mpango katika usiku wa Tuzo kwa mwajiri Bora wa mwaka 2024 ambapo Kampuni ya bia nchini (TBL) imeibuka mshindi wa jumla ikifuatiwa Kampuni ya Barick Gold huku Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA ikishika nafasi ya tatu.  Amewapongeza waandaaji wa tuzo hizo na kuwataka kupanua wigo wa makundi ya ushiriki huku akisisitiza umuhimu wa utoaji wa motisha mahala pa kazi ili watumishi waongeze ari ya kufanya kazi kwa viwango na ubora wajuu.  “ mwajiri anachokihitaji kwa mwajiriwa ni muda na ujuzi wake basi. Hivyo, waajiri ongezeni umakini na utu mahali pa kazi na mkifanya hivyo...

JUMUIYA ZA USAFIRISHAJI MAJINI WATAKIWA KUSHIRIKIANA KUIMARISHA SEKTA YA USAFIRISHAJI

Image
  Jumuiya ya Mamlaka za Usimamizi wa Usafiri majini Barani Afrika zimetakiwa kushirikiana na kuungana ili kuimarisha usalama wa sekta ya usafirishaji majini na hivyo kuchochea maendeleo ya Uchumi katika nchi husika. Wito huo umetolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko Leo Disemba 29,2024 wakati akifungua Kongamano na Mkutano Mkuu wa mwaka wa Jukumuiya ya Mamlaka za Usimamizi na Usafirishaji Majini Barani Afrika unaofanyika kwa siku tatu, Jijini Dar es Salaam. Dkt. Biteko amewashauri washiriki kutumia mkutano huo kama fursa ya kubuni na kupanga mikakati mipya ya kuelekea katika mafanikio kupitia sekta hiyo ambapo amesisitiza kuwa ushirikiano miongoni mwa washiriki na kujadiliano juu ya kuwezesha masuala mbalimbali na sekta ya usafirishaji litakuwa suluhisho la changamoto mbalimbali zilizopo. “Kila mmoja wetu atumie fursa ya mkutano huu kujiwekea malengo yatakayo tuwezesha kufikia azima ya kuboresha usalama na kuimarisha sekta ya usafirishaji wa majini”...

MALKIA MWENYE CHOMBO YAZINDULIAWA RASMI MO FINANCE

Image
Wanawake mbalimbali watakiwa kujitokeza kuchukua mikopo ya bajaji itakayowasaidia kujikimu kimaisha ili wasiwe magoli kipaji kwenye familia zaoa. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Melt  Group na Mo Finance Fatema Dewji amesema wamezindua rasmi Kampeni ya Malkia mwenye Chombo, mradi wa kipekee unaolenga kuwawezesha wanawake kwa kuwapatia Bajaj mpya kwa mkopo wa masharti nafuu.  "Mpango huu unaendeleza dhamira ya Melt ya kushiriki katika maendeleo ya jamii na kubadilisha maisha ya wanawake wengi kujikimu kimaisha na kuwa na maendeleo yao binafsi. “Malkia mwenye Chombo ni mwendelezo wa desturi ya METL ya kuinua jamii. Tuna furaha kuona familia nyingi sana zimewezeshwa kupitia miradi yetu, na kampeni hii ni hatua nyingine muhimu ya kuinua kundi kubwa zaidi.” "Anapochukua mkopo tuna hakikosha tunamlipia mafunzo ya udereva katika Chuo cha NIT na kumpatia mafunzo ya biashara kwa kumkutanisha na wafanya biashara mbalimbali watakaompa njia ya nini a...

RC CHALAMILA WANANCHI JITOKEZENI KWA WINGI KUPIGA KURA NOVEMBA 27, 2024

Image
Chalamila amesema Mkoa unajumla ya mitaa 564 ambayo itashiriki uchaguzi huo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana Wilaya ya Ilala amewataka wananchi hususani wa Mkoa huo kujitokeza kwa wingi kupiga kura Novemba 27,2024 ili kupata kiongozi atakayewaletea maendeleo. Aidha RC chalamila amesema vituo vya uchaguzi vitafunguliwa saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 jioni, Mkoa unajumla ya mitaa 564 ambayo itashiriki katika uchaguzi huo pia Mkoa umejipanga vizuri katika kuhakikisha unawafikia watu wengi zaidi kwa kuongeza vituo vya kupiga kura katika mitaa. Vilele amevitaka vyombo vya Habari kutoa taarifa sahihi za uchaguzi na kuhamasisha wananchi kupiga kura. Sanjari na hilo RC Chalamila amewataka wananchi pamoja na vyama vya siasa kushiriki uchaguzi huo kwa kuzingatia 4R za Rais Samia yenye maana ya Maridhiano, Ustamilivu, Mageuzi na Kujenga upya "Lazima tujenge siasa zenye ustamilivu, siasa ambayo tuna...

MSAMA KUMSOMESHA MTOTO WA MAREHEMU FREDY

Image
  MKURUGENZ I wa Msama Promotion Alex Msama amejitolea   mtoto wa  Marehemu Msanii wa Bongo Movie Fredy Gordon Kiluswa miaka mitatu. MKURUGENZI wa Msama Promotion Alex Msama amejitolea kumsomesha mtoto wa  Marehemu Msanii wa Bongo Movie Fredy Gordon Kiluswa miaka mitatu. Akizungumza Mshehereshaji katika msiba wa Fredy Mc Dkt Cheni amesema kuwa Msama ametoa ahadi hiyo baada ya Steve Mengere  'Steve Nyerere' kusema atamsomesha mtoto huyo kwa mwaka mmoja. "Msama amesema kuwa atampokea Steve Nyerere kwa kumsomesha mtoto huyo kwa mwaka mmoja ndipo Msama akasema atampokea Steve Nyerere kwa kumsomesha miaka mitatu jina la mtoto anayejulikana kwa jina la Kenzo ambaye kwa sasa yupo darasa la pili."amesema Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Msama Promotion Alex Msama amesema kuwa ameguswa na Msiba huo wa kijana mdogo hivyo ameamua kuchangia kumsomesha mtoto kama sehemu ya faraja kwa familia hiyo. "Ni kijana mdogo ameondoka mapema sana binafsi nimemfahamu kup...

TANZANIA MWENYEJI MKUTANO WA SABA WA TASAC USAFIRI MAJINI

Image
  Nagitte Davis  Dar es salaam. Tanzania  kupitia  shirika la uwakala  wa Meli Tanzania (TASAC) imeteuliwa  kuwa  nchi mwenyeji kwenye  wa Makutano wa  saba (7) wa akimataifa wa jumuiya ya  Mamlaka za usimamizi wa usafiri  Majini Barani Afrika utakaofanyika kuanzia tarehe  29 novemba  hadi 10 Disemba 2024 jijini Dar es salaam. Akizungumza na waandishi wa habari Waziri  wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema lengo la mkutano  huo ni kujadili  masuala muhimu  ya maendeleao ya udhibiti na usimamizi wa usalama wa usafiri majini hatani afrika. Amesema  kipaumbele kikiwa ni mustakabali wa usafiri wa majini ma kuongeza ushirikiano baina ya nchi na wanachama. "Kauli mbiu ya mkutano huo ni ' Kuimarisha mustakabali wa sekta ya usafiri majini barani Afrika, ushirikianao katika teknolojia na ubunifu  ili kupunguza hewa ukaa, kuimarisha  usalama wa mazingira,  na  mazingira  ya sekta ...

TAMASHA LA FILAMU BEIJING AFRICAN LAZINDULIWA DAR

Image
Na Brigitte Davis Msimu wa Matangazo ya Tamthiliya na Filamu za Televisheni za Beijing Afrika umefunguliwa rasmi   Dar es Salaam, ukiongozwa na Idara ya Televisheni na Redio ya Beijing.  Tamasha hilo linaadhimisha miaka 10 ya ushirikiano thabiti kati ya Beijing na nchi za Afrika kupitia maonyesho ya filamu bora, likiimarisha urafiki na mawasiliano ya kiutamaduni kati ya China na Afrika. Sherehe za uzinduzi zimefanyika Dar es Salaam na kuhudhuriwana viongozi kutoka Idara ya Televisheni na Redio ya Beijing, Bodi ya Uendelezaji wa Filamu ya Tanzania, Baraza la Sanaa la Tanzania (Basata) na wadau mbalimbali wa sekta ya filamu kutoka pande zote mbili. Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Televisheni na Redio ya Beijing, Dong Dianyi, amesema kuwa tamasha hili limekuwa daraja muhimu la mawasiliano ya kiutamaduni kati ya China na Afrika.  “Miaka kumi iliyopita, tamasha hili lilianza barani Afrika, na sasa limekuwa alama ya urafiki wa kweli kati ya watu wa pande hizi mbili. Tunatazam...

NICE TO MEET YOU IMEZINDULIWA RASMI KUONESHWA SWAHILI PLUS

Image
Na Brigitte Davis TAMTHILIA ya 'Nice to Meet you' inayowakutanisha waigizaji  Lulu Abas 'Lulu Diva' na Hemed Suleiman 'Hemed 'PHD' waliokuwa na uhasama imezinduliwa rasmi na kuwafanya wao kumaliza tofauti zao. Wawili hao inasemekana walianza tofauti zao tangu walipokuwa lokesheni wakirekodi Tamthilia hiyo iliyowahusisha na ugomvi wao kuendelea hadi kwenye maisha yao ya kawaida. Lakini wawili hao wameombana msamaha na kuendelea na maisha yao baada ya kumaliza tofauti zao hizo. Akizungumza na waandishi wa habari Hemed PHD alisema kuwa yeye ndio aliyebeba thamthilia hiyo ya 'Nice to meet you' itakayo kuwa inarushwa Startimes kupitia chanel ya Swahili Plus. "Ushiriki wangu katika tamthilia hii Mimi  ndio muhusika Mkuu na nimeigiza kama mtumishi wa Mungu nimeigiza humo ndo unatakiwa kumfatilia kuanzia uzinduzi rasmi hadi tamthilia yenyewe Watanzania wajiandae kumuona Saimon Mlokole. "Natoa shukrani zangu kwa wote tulioshirikiana ni tamthilia yen...

OVAH YANAPINGA MANENO YA UDHALILISHAJI

Image
Na Brigitte Davis TAASISI ya Ovah Tanzania imesema inapinga maneno ya udhalilishaji yanayotolewa kwa wanawake kwenye maeneo ya wazi ya kijamii kwa kuwa kuyachukulia kawaida  kunamfanya mwanamke  ajihisi hayuko salama. Hayo yamesemwa Dar es Salaam juzi na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Modesta Joseph kwenye uzinduzi wa mradi wa Jamii Salama Initiative (JSI) utakaotumika kutoa elimu dhidi ya maneno ya udhalilishaji kwa wanawake, program itakayofanywa kwa ushirikiano na taasisi nyingine mbalimbali. Modesta alisema baadhi ya maneno wanayoitwa wanawake kwenye maeneo ya Masoko, kwenye vituo vya mabasi a mitaani yakiwemo Chura, Paka na mengine yanayoashiria udhalilishaji yanapaswa kukemewa na kila mmoja kwa usalama wao. "Ni maneno machafu ambayo yamekuwa yakiwafanya wanawake wengi hawana amani, tumekuja na mradi wa JSI ili tuendelee kutoa elimu kwa madereva, masokoni na maeneo mengine ya wazi umuhimu wa kuheshimiana na kulindana ili kutengeneza jamii salama,"alisema. Alisema pia, w...

DRAMAAND MOVIE BROADCAST SEASON IN AFRICA

Image
Beijing TV Dramas&Movies Broadcasting Season in Africa--Celebrating a Decade of Cultural Exchange, Ushering in a New ChapterContent:In September 2024, the Forum on China-Africa Cooperation in Beijing reaffirmed the commitment to deepen ties between China and African nations, working towards a shared future.  Media continues to play a pivotal role in this collaboration, serving as a bridge for cultural exchange and information-sharing.  On November 18, the “Beijing TV Dramas&Movies Broadcasting Season in Africa” will launch, bringing a fresh wave of acclaimed shows under the “Beijing Audiovisual” brand to African audiences, promoting greater understanding between Chinese and African peoples. A Decade of Stories Bringing China and Africa TogetherSince its inception in 2014, the “Beijing TV Dramas&Movies Broadcasting Season in Africa” has introduced high-quality Chinese TV shows to over 30 African countries in languages including English, French, Portuguese, and Swahi...

AAT NGAZI USALAMA ELIMU BARABARANI KWA WANAFUNZI NI MUHIMU

Image
Naibu Kamishna wa Polisi Kamanda Kikosi Maalumu Usalama barabarani Kamanda DCP Ramadhani Ngazi amesema suala la elimu ya  usalama barabarani kwa wanafunzi ni muhimu kuwapa ili kupunguza ajali zisababishwazo na uzembe wa madereva. Amesema elimu kwa Wanafunzi  ni jambo linalohitaji kuunganisha nguvu za pamoja ili kuokoa kundi hilo  kwa bahati mbaya wao  ni miongoni mwa watumia na wako hatarini   zaidi wanapovuka barabra za maeneo ya shulea na majumbani . Akizungumza na wanafunzi na walimu katika shule saba za Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, wakati akifunga mafunzo ya Tathmini za shule zilizopatiwa elimu hiyo  Naibu Kamishna wa Polisi Kamanda Kikosi Maalumu Usalama barabarani Ramadhani Ngazi  amesema kuwa Wametoa mafunzo ya mwezi mmoja katika shule 11 zilizopo katika Wilaya ya Ilala na Kinondoni. "Mafunzo waliyopatiwa baadhi ya waalimu na wanafunzi yanakwenda kuwa chachu kubwa kwa wengine  kupunguza ajali za barabarani husasani kwa w...

MKUTANO MKUU WA TEF KUFANYA KESHO

Image
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) wametangaza kufanya Mkutano  Mkuu wa  Mwaka  unatarajia kufanyika kesho Novemba 7 mwaka huu katika ukumbi wa NSSF uliopo Ilala jijini Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Deodatus Balile amesema kuwa Mkutano huo wa nane utahudhuliwa na zaidi ya wanachama 168 ambao tayari wamethibitisha kushiriki katika Mkutano huo. "Mkutano mkuu 8 utafunguliwa kesho na Mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Habari  Teknolojia, Mawasiliano na habari Jerry Silaa, kwa mara ya kwanza tangu awe Waziri wa Wizara hiyo atakutana na kuongea na waandishi na Wahariri. "Tutakuwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Robert Chalamila na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mpogolo wote wamethibitisha kuwepo na kujadili pamoja nasi. "Katika Mkutano huu tunatarajia kujadili na kuingiza wanachama wapya zaidi ya 20 wenye vigezo na masharti ambapo mwanachama anatakiwa kuwa na cheti cha diploma na uzoefu wa kutosha katika Tasnia ya habari."amesema Balile Pia am...

MSIMU WA SITA HELLO! MR RIGHT DKT KUMBUKA NDANI

Image
Shindano la Hello Mr Right! msimu wa sita limezinduliwa rasmi vijana wakihimizwa kutumia nafasi ya kufuatilia kujifunza namna ya kupata wenza sahihi wa maisha yao. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Godfrey Lugalabam 'Gara B' amesema kuwa msimu huu umekuja kitofauti kwa kuongeza watu wapya wa kutoa mafunzo huku  Kaulimbiu yao ikiwa ni  'Usione so' "Lengo ni kuwakutanisha watu wanaotafuta wenza na kuwaunganisha pamoja waweze kutimiza malengo yao ya kujenga familia ya pamoja."amesema Gala B Kwa upande wake mtangazaji wa kipindi cha Hello! Mr Right Aliya Mohammed amesema kuwa Shindano hilo huchukua wadada 12 ambapo watatafuta wenza wao ambao kwao ni Mr Right! mmoja. "Watu wasichukulie Hello! Mr Right kama Shindano la kiuni hapana Shindano hili lina maadili yote na ndio sababu tunawakutanisha kisha  kuwapa ushirikiano katika kutimiza kiapo cha ndoa."amesema Swalehe Nasoro 'Dokta Kumbuka' amesema kuwa atakuwepo kwaajili ya kuw...