MKUTANO MKUU WA TEF KUFANYA KESHO
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) wametangaza kufanya Mkutano Mkuu wa Mwaka unatarajia kufanyika kesho Novemba 7 mwaka huu katika ukumbi wa NSSF uliopo Ilala jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Deodatus Balile amesema kuwa Mkutano huo wa nane utahudhuliwa na zaidi ya wanachama 168 ambao tayari wamethibitisha kushiriki katika Mkutano huo.
"Mkutano mkuu 8 utafunguliwa kesho na Mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Habari Teknolojia, Mawasiliano na habari Jerry Silaa, kwa mara ya kwanza tangu awe Waziri wa Wizara hiyo atakutana na kuongea na waandishi na Wahariri.
"Tutakuwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Robert Chalamila na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mpogolo wote wamethibitisha kuwepo na kujadili pamoja nasi.
"Katika Mkutano huu tunatarajia kujadili na kuingiza wanachama wapya zaidi ya 20 wenye vigezo na masharti ambapo mwanachama anatakiwa kuwa na cheti cha diploma na uzoefu wa kutosha katika Tasnia ya habari."amesema Balile
Pia ameongeza kuwa "Mada kuu zitakazo zungumziwa ni Utendaji wa vyombo vya habari, Katika taaluma yetu tumepatia wapi na tumekosea wapi? Kuna mitandao ya kijamii ambayo inafanya kazi kwa weledi kulingana na taaluma.
"Kufundisha na ubora wa kutengeneza na kuchakata habari, kubadilishana uzoefu, hali ya uchumi wa vyombo vya habari na kuacha kulia Lia na kulalamika mitandaoni kwa kukaa na kujadili jinsi ya kutatua changamoto na kuweka mikakati nini cha kufanya.
Uwelezi unatuhusu waandishi wote na wahariri kwa kuchakata habari Bora na yenye ushawishi kwenye jamii.Maadili katika kutengeneza habari za ajali kuacha kusambaza picha zisizo na maadili katika vyombo vya habari.
"Kukamatwa kwa waandishi wa habari wengi wao tumegundua ni wamitandao ya kijamii bila kujua mipaka na misingi ya waandishi wa habari kujua na kufata misingi ya waandishi katika utendaji kazi.
Mwandishi wa habari Mkongwe Salim Salim amesema kuwa waandishi wanatakiwa kuwa na Nidhamu katika kazi kwa kuzingatia Mavazi na weledi katika kazi.
"Nidhamu katika Mavazi mwandishi anapaswa kujua nini anavaa wapi sio Mkutano wa Waziri Mkuu mtu unaenda na tisheti imeandikwa I love you au nguo za vyama kwenye kukava kazi za Uchaguzi."amesema Salim


Comments
Post a Comment