MALKIA MWENYE CHOMBO YAZINDULIAWA RASMI MO FINANCE



Wanawake mbalimbali watakiwa kujitokeza kuchukua mikopo ya bajaji itakayowasaidia kujikimu kimaisha ili wasiwe magoli kipaji kwenye familia zaoa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Melt  Group na Mo Finance Fatema Dewji amesema wamezindua rasmi Kampeni ya Malkia mwenye Chombo, mradi wa kipekee unaolenga kuwawezesha wanawake kwa kuwapatia Bajaj mpya kwa mkopo wa masharti nafuu. 

"Mpango huu unaendeleza dhamira ya Melt ya kushiriki katika maendeleo ya jamii na kubadilisha maisha ya wanawake wengi kujikimu kimaisha na kuwa na maendeleo yao binafsi.

“Malkia mwenye Chombo ni mwendelezo wa desturi ya METL ya kuinua jamii. Tuna furaha kuona familia nyingi sana zimewezeshwa kupitia miradi yetu, na kampeni hii ni hatua nyingine muhimu ya kuinua kundi kubwa zaidi.”

"Anapochukua mkopo tuna hakikosha tunamlipia mafunzo ya udereva katika Chuo cha NIT na kumpatia mafunzo ya biashara kwa kumkutanisha na wafanya biashara mbalimbali watakaompa njia ya nini anatakiwa kufanya na wapi anatakiwa kufika.

Kwa upande mwingine, Soumya Das, Makamu wa Rais wa Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini - Bajaj Auto Ltd India, alisifu kampeni hiyo na kubainisha kuwa mpango huu wa kutoa nafasi kwa wanawake unafuatwa na kampuni ya Bajaj pia. 

“Sisi kutoka Bajaj Auto tunafurahi kwamba mshirika wetu mashuhuri wa usambazaji, MeTL Group, leo anazindua mpango wa ‘Malkia Mwenye Chombo.’ Mpango huu unalingana na juhudi zetu kutoka Bajaj Auto za kusaidia wafanyakazi wetu kufanikiwa katika taaluma zao. 

Katika viwanda vyetu, tuna mistari ya uzalishaji inayojumuisha wanawake pekee wakitengeneza pikipiki kubwa na magari ya umeme.”Aidha, Bw. Ashish Joshi, Mtendaji Mkuu wa kanda wa MeTL, alisisitiza upekee wa mpango huu, akionyesha jinsi juhudi za pamoja za MeTL, Bajaj na MO Finance zitakavyowezesha wanawake na kukuza uhuru wao wa kifedha.

“Chini ya mpango huu, MeTL Bajaj itazingatia uwezeshaji wa vitendo kwa kutoa mafunzo ya kuendesha Bajaj RE 4S, kutoa elimu, kuhusu sheria za barabarani, na kuwasaidia washiriki kupata leseni za kuendesha Bajaj kutoka kwa mamlaka husika. Hii inahakikisha kuwa wanawake wanakuwa na ujuzi na sifa zinazohitajika kwa ajili ya usafiri na ujasiriamali.”Hafla ya uzinduzi inatoa fursa kwa wanawake kufanikisha uhuru wa kifedha na kujenga maisha endelevu kwa ajili yao na wapendwa wao.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA