Posts

Showing posts from July, 2025

BAADA YA JINA LAKE KUKATWA; ALEX MSAMA ATOA NENO

Image
Siku moja tu baada ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuondoa jina lake miongoni mwa watia nia wa Jimbo la Ubunge Ukonga jijini Dar, aliyetia nia, Alex Msama ametoa neno zito. Msama ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Msama Promotions & Dira Media ametoa neno kwa kuwataka watia nia wote waliokatwa majina yao nchini kote kutoa ushirikiano kwa wale ambao majina yao yanakwenda kupigiwa Kura za Maoni ngazi ya kata na hatimaye kumpata mgombea mmoja atakayepeperusha bendera ya CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2025. Huyu hapa Alex Msama: "Nilitia nia kuomba kuteuliwa na chama changu kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga. Lakini isivyo bahati jina langu halikurudi. "Siyo kwamba sifai. Nafaa ila jina langu halikurudi. Kwa wakati huu wamepatikana wengine ambao wamepewa nafasi na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya chama chetu ili kuendelea na mchakato. "Sisi sote ni wana CCM. Kwa hiyo wote tuna sifa ila waliopitishwa wanafaa kwa sasa. Nawaomba wat...

UNYONYESHAJI MAZIWA YA MAMA WAPIGA HATUA CHANGAMOTO BADO ZIPO

Image
Unyonyeshaji wa maziwa ya mama wapiga hatua, lakini changamoto bado zipo Dar es Salaam Viwango vya unyonyeshaji wa maziwa ya mama nchini Tanzania vinaendelea kuimarika, huku asilimia ya watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya mama pekee ikiongezeka kutoka asilimia 58 mwaka 2018 hadi asilimia 64 mwaka 2022. Kadhalika, watoto wanaonyonyeshwa ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa wameongezeka kutoka asilimia 58 mwaka 2018 hadi asilimia 70 mwaka 2022, hatua inayotajwa kuwa na mchango mkubwa katika afya na maendeleo ya mtoto. Takwimu hizo zilitolewa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk. Seif Shekalaghe, wakati wa uzinduzi wa wiki ya Unyonyeshaji wa maziwa ya Mama Duniani, ambapo pia amezindua Mwongozo wa Kitaifa wa Kuzuia na Kutibu Ukondefu na Uvimbe utokanao na Ukondefu Mkali (Nutritional Oedema). Kwa niaba ya Dk. Shekalaghe, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – TAMISEMI (Afya), Prof. Tumaini Nagu, amesema pamoja na mafanikio hayo, bado kuna changamoto ya watoto...

CCM YASISITIZA KUHESHIMU SHERIA ILI KUEPUSHA MACHAFUKO KATIKA UCHAGUZI

Image
CCM yasisitiza Kuheshimu Sheria Ili Kuepusha Machafuko Katika Uchaguzi Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesisitiza umuhimu wa kufuata sheria na taratibu za uchaguzi ili kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unakuwa huru, wa haki na wa amani. Chama hicho pia kimeeleza utayari wake wa kukubali matokeo yoyote yatakayotokana na uchaguzi, mradi yapatikane kwa mujibu wa taratibu halali. Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Zanzibar, Khamis Mbeto Khamis, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. “Endapo sheria zitazingatiwa kikamilifu, hakutakuwa na sababu ya machafuko. Amani na utulivu ni matokeo ya kuheshimu taratibu zilizowekwa kisheria,” alisema Khamis. Aidha, amesisitiza kuwa ni wajibu wa vyama vyote vya siasa pamoja na wadau wengine wa uchaguzi kuhakikisha kuwa wanaheshimu sheria za uchaguzi ili kulinda mshikamano wa kitaifa. Khamis pia ameonya dhidi ya jaribio lolote la kuingilia au kuhujumu kazi ya Tume...

SAMIA CUP 2025 YAZINDULIWA RASMI ZAWADI NONO KUTOLEWA

Image
Samia Netball Cup 2025 yazinduliwa rasmi: zawadi nono kumnufaisha mwanamke kupitia michezo Mashindano ya mpira wa netball kwa Mkoa wa Dar es Salaam yanayojulikana kama Samia Cup 2025 yamezinduliwa rasmi leo. Akizungumza na Habari Leo, mwandaaji wa mashindano hayo ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Twende Pamoja na Mama Spoti Promotion, Kasimu Ahmad, amesema kuwa lengo la mashindano haya ni kutoa fursa kwa wanawake na mabinti kushiriki katika michezo ya netball huku wakipata nafasi ya kujiimarisha kiafya na kiuchumi. “Kumekuwa na michezo mingi lakini kwa wakati huu tumeona ni muhimu kuja na mashindano ya netball kwa kuwa wanawake pia wanastahili jukwaa la kuonesha vipaji vyao. Ni sehemu ya kumuunga mkono Rais Samia kwa juhudi zake katika kuinua wanawake kupitia michezo,” amesema Kasimu. Katika mashindano hayo, mshindi wa kwanza atazawadiwa Shilingi Milioni 5, kombe na medali. Mshindi wa pili atapata Shilingi Milioni 3 na medali, huku mshindi wa tatu ataondoka na Shilingi Mil...

WAANDISHI WAPEWA NONDO WATAKIWA UMAKINI KIPINDI CHA UCHAGUZI NA TAARIFA FEKI

Image
Waandishi Watakiwa Kuwa Makini na Habari za Uchaguzi Katika Kipindi cha AI na Taarifa Feki Tunapokaribia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, waandishi wa habari nchini wametakiwa kuwa makini na namna wanavyoripoti taarifa, hasa katika zama hizi za teknolojia ya akili bandia (AI) ambazo zimeongeza kasi ya kusambaa kwa taarifa za uongo, chuki na uchochezi mitandaoni. Wito huo umetolewa katika warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), kwa kushirikiana na mpango wa #defyhatenow kupitia Global Action for Peacebuilding (GAPI) na kwa ufadhili wa GIZ. Warsha hiyo iliwaleta pamoja waandishi wa habari mbalimbali nchini na kuwapa mafunzo juu ya fact-checking, usalama wa habari mitandaoni, matumizi salama ya AI, na mbinu za kuandika taarifa zinazojenga amani wakati wa uchaguzi. Akizungumza katika warsha hiyo, Njokii Kariuki kutoka taasisi ya Global Peace Initiative ya Nairobi, Kenya, alieleza kuwa baadhi ya taarifa huundwa kwa makusudi ili kuchochea...

MBOWE UMEONYESHA UKOMAVU NA UZALENDO

Image
Anaandika @stevenyerere2 [Mbowe] Umeonyesha Ukomavu mkubwa sana Umeonyesha Uzalendo kwenye Taifa lako ,Hukuangalia LOLOTE Mbele yako zaidi ya kuhakikisha Taifa letu linasonga Mbele,..Maendeleo Hayana Itikadi Maendeleo ni Faida kwa kila Mtanzania,.,.,.. Mh @freemanmbowetz Wewe ni Ni mfano wa kuigwa kwa wanasiasa na wapenda Siasa kuna la kujifunza kupitia wewe hasa vijana wanaozania Siasa ni kupinga Tu Kutukana, kukosoa,..na wanasahau Siasa ni Umoja wa kweli kwenye Kuhakikisha Taifa linasonga mbele,... Dira si jambo la Mtu Dira ni jambo kubwa kwa maslahi ya Taifa letu, mh Mbowe leo Umeonyesha Upo kwa Ajiri ya Maendeleo ya Taifa letu, Nimeona kila kona Wanasiasa Uchwara, Wana harakati Uchwara wanakubeza kwa hili wanashindwa kutofautisha kuwa Wewe ni mwenyekiti Mstafuuu Una haki Ya Kushiriki kwenye kila Jambo lenye Tija kwa Maslahi ya Taifa,... Kazi ya Kutetea au Kushiriki kazi za chama chao Unaweza lakini shuhuri Za Chama zenye Tija na Maslahi ya Ya Watanzania, Lakini Sio shuhu...

VETA YAJA NA KONA YA WATOTO SABASABA

Image
Chuo Cha Mafunzo na Ufundi Stadi VETA) Songea imekuja na kona ya watoto katika maonesho ya 49 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kwa lengo la kuibua vipaji na kuwafundisha misingi ya maisha. Faulata Mutalemwa ambaye ni Mwalimu kutoa VETA Songea amesema kupitia kona hiyo ya watoto wanajifunza vitu mbalimbali ikiwemo stadi za mikono mbalimbali na kuondoka nazo. Akitaja stadi hizo amesema ni pamoja na ushonaji, urembo pamoja na masuala ya umeme. "Kupitia kona ya watoto mtoto anaweza kujifunza vitu mbalimbali vya namna ya kuchana nywele, kutunza ngozi yake, namna ya kushona nguo zake pamoja na kudhiifadhi"amesema Mutalemwa. Kwa upande wa eneo la umeme amesema mtoto anajifunza namna ya gani taa inawaka huku akifuata hatua nyepesi. Aidha ametoa wito kwa wazazi, walezj kutembelea katika Banda la Veta ili watoto wao waweze kujifunza vitu mbalimbali vinavyohusu maisha.

JESSICA: MADARASA YA UONGOZI KWA VIJANA YAMEZAA VIONGOZI

Image
Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM TAIFA Ndg. Jessica Mshama amesema kuwa Madarasa ya uongozi yanayoendeshwa na Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) yamekuwa chachu ya kuoka Viongozi wapya ambao baadhi yao wamejitokeza kugombea nafasi mbalimbali za kiuongozi. Ndg. Jessica Mshama aliyasema hayo wakati wa mahojiano na Watangazi wa Kipindi cha Sentro cha Clouds Tv kilichofanyika Jana 08 Julai, 2025 katika studio za Clouds Tv Jijini Dar es Salaam.

JESSICA: CCM INAJALI UONGOZI WA VIJANA

Image
Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM TAIFA Ndg. Jessica Mshama amesema Chama Cha Mapinduzi kinajali sana uwezo wa Vijana katika uongozi ndio maana kinawaamini na kuwapa nafasi za juu za kiuongozi. Ndg. Jessica ameonesha uthabiti wa CCM katika uongozi wake kwa kuitofaugisha na vyama vingine kutokana na kuwaamini Vijana katika nafasi mbalimbali za kiuongozi na kwamba ushindi wa CCM hautokani kwa bahati mbaya kwa sababu kimejenga zaidi kwa Vijana. Kuhusu suala la Uchaguzi, Ndg. Jessica Mshama amesema kuwa Viongozi wa Juu wa Jumuiya ya UVCCM wamekuwa wakiratibu Mikutano inayohusisha Ziara zao katika Mikoa mbalimbali kwa ajili ya kuhamasisha Vijana kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali pamoja na kujiandaa kupiga kura ifikapo Oktoba 2025. Ndg. Jessica Mshama aliyasema hayo wakati wa mahojiano na Watangazi wa Kipindi cha Sentro cha Clouds Tv kilichofanyika Jana 08 Julai, 2025 katika studio za Clouds Tv Jijini Dar es Salaam.

MNAOCHUKUA FOMU JIPIMENI WENYEWE KWA AJILI YA WATANZANIA AU KWENDA KUPIGA PICHA BUNGENI

Image
"Umechukua fomu kwa ajili ya watanzania, au unataka kupiga picha bungeni?" – Steve Nyerere Ahoji Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao, Steve Mengele maarufu kama Steve Nyerere, ametoa kauli nzito kuhusu wimbi la vijana maarufu kuchukua fomu za kugombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025. Kupitia mahojiano maalumu, Steve Nyerere amewataka vijana hao kujiuliza kwa dhati: “Je, umechukua fomu kwa ajili ya kuwatumikia Watanzania au unataka kupiga picha bungeni?” Ameeleza kuwa ni jambo jema kuona vijana wakijitokeza katika siasa, lakini akasisitiza kuwa siasa si jukwaa la kutafuta umaarufu au fursa za binafsi, bali ni wito unaohitaji moyo wa kweli wa huduma kwa wananchi. "Nafasi ya uongozi si ya kupigia picha bungeni. Ni wajibu, ni dhamana, na ni lazima uwe na moyo wa kweli wa kuwatumikia wananchi," amesema. Kauli hiyo imekuja katika kipindi ambacho kumeibuka wimbi la vijana wenye ushawishi mkubwa kwenye mitandao ya kij...

VETA ILIVYO WAWEZESHA WATANZANIA KUJIAJILI

Image
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imesema inajivunia mageuzi makubwa iliyoyafanya katika sekta ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi nchini ambayo yamewezesha Watanzania wengi kujiajiri na kuajiriwa. Hayo yamebainishwa na Mkurungezi Mkuu wa VETA, Anthony Kasole Wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya 49 ya Kimataifa ya kibiashara Sabasaba yanayoendelea. Amesema VETA imekuwa ikitoa ujuzi katika maeneo ambayo yanawagusa watanzania kuweza kujiajiri na kuajiriwa katika sekta mbalimbali. “Kwa sasa VETA tunatoa ujuzi katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwa wale watu wanaohudumia wazee .majumbani , takribani watu 700 wameweza kuhitimu mafunzo na kupata ajira”amesema CPA Kasole Aidha amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuweza kuweka msisitizo katika elimu ya mafunzo na Ufundi stadi . Amesema kupitia msisitizo huo VETA wameweza kuona manufaa makubwa sana na kuweza kufaidika na kutekeleza mambo mengi ....

ACER YAJIZATITI KUPANUA SOKO AFRICA MASHARIKI KWA TEKNOLOJIA YA KISASA NA USAMBAZAJI WA HUDUMA ZAKE

Image
Acer Yajitanua Afrika Mashariki: Yaleta Teknolojia ya Kisasa kwa Biashara, Elimu na Burudani ya Kidijitali Kampuni ya kimataifa ya teknolojia, Acer Inc., imetangaza rasmi kuanza upanuzi mkubwa wa shughuli zake katika ukanda wa Afrika Mashariki. Kupitia hatua hii ya kimkakati, Acer inalenga kuimarisha upatikanaji wa teknolojia ya kisasa, kuanzia kwa kompyuta za matumizi ya kila siku, vifaa vya kielimu, hadi vifaa vya hali ya juu kwa wapenzi wa michezo ya mtandaoni (gaming). Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Grigory Nizovsky, Makamu wa Rais wa Acer kwa Kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika, alisema kuwa kampuni hiyo inalenga kuwezesha maendeleo ya kidijitali kwa biashara, taasisi za elimu, na kaya binafsi kupitia suluhisho zinazoongeza tija, ubunifu, na urahisi wa mawasiliano ya kiteknolojia. “Tunahitaji teknolojia isiyo na mipaka, inayoondoa vikwazo na kuweka watu karibu. Dhamira yetu ni kuleta mageuzi ya kidijitali yanayozingatia mahitaji ya soko la Afrika Mashariki,” a...

PURA YAWAITA WAWEKEZAJI KUJA KUWEKEZA KWENYE NISHATI SAFI

Image
NA Brighitte Davis MAMLAKA ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), imetoa wito kwa wawekezaji kuja kuwekeza katika masuala ya Nishati Safi kutokana na kuwepo mikakati imara, mazingira wezeshi, amani na utulivu inayotoa fursa kwa maendeleo ya kiuchumi. Pia ameweka wazi kwamba kutokana na kuwepo kwa mazingira wezeshi, amani na utulivu shughuli za uzalishaji katika mkondo wa Juu wa Petrol kwenye nyanja ya ajira imeongezeka kutoka asilimia 55 hadi 85. Mhandisi Charles Sangwene ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa PURA, amebainisha hayo leo, Julai 9, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kutembelea mabanda yaliyopo katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam. “Tangu mwaka 2017 tumekuwa tukishiriki maonesho haya na mwaka huu yamekuwa mazuri kutokana na kuendeshwa kidigitali na tutaendelea kushiriki kwa mafanikio makubwa na kwa mwaka huu tumepata maswali mazito kutoka kwa wananchi wanaofika kutembelea banda letu kuhusu ni...

PIMEA YAWAPA HESHIMA WANAWAKE WAIMBAJI NA WACHUNGAJI

Image
Upendo Nkone Rose Muhando, Shusho na Bahati Bukuku watunukiwa tuzo za heshima katika hafla ya PIMEA Katika tukio lililojawa na sifa, vicheko na machozi ya furaha, mastaa wakubwa wa muziki wa Injili nchini Tanzania—Rose Muhando, Christina Shusho na Pastor Bahati Bukuku—wamepokea tuzo za heshima kupitia hafla ya The Pinnacle of Mentorship & Excellence Awards (PIMEA) iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ya kipekee ilifanyika katika Makumbusho ya Taifa, Posta, ambapo zaidi ya wanawake 15 waliotukuka katika huduma ya kiroho walitambuliwa kwa kazi zao kubwa katika jamii. Mkurugenzi na mbeba maono wa tuzo hizo, Dk Christine Mbelwa, alieleza kuwa lengo kuu la PIMEA ni kuthamini na kutambua mchango wa wanawake waliotoa maisha yao kwa ajili ya huduma ya Injili. "Wanawake hawa wamevumilia, wamehudumu kwa moyo na kazi yao imeigusa jamii kwa kiwango kikubwa," amesema Dk Christine kwa msisimko mkubwa. "Tunataka kizazi kijacho kijifunze kuwa kuna wanawake...

VIJANA CCM NDIO CHAMA PEKEE CHENYE IMANI NA VIJANA

Image
asilimia 60 ya walioshinda walikuwa vijana. Hii ni ishara kuwa vijana hawasubiri kupangiwa tena, bali wanajitokeza na kuaminiwa na wananchi. Ukomo wa viti maalum kwa wanawake umeongeza ushiriki wa vijana wanawake, jambo linaloimarisha usawa wa kijinsia na ujumuishwaji. 5. RAIS DKT. SAMIA: KIONGOZI WA MFANO KWA VIJANA Chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, vijana wamekuwa mstari wa mbele katika ajira, elimu, diplomasia, sanaa na michezo. Kauli mbiu yake ya “Kazi na Utu, Tunasonga Mbele” si maneno tu, bali ni dira ya kweli ya maendeleo. Ameanzisha fursa nyingi zinazowalenga vijana, akiwemo kuwa Rais wa kwanza mwanamke kuwateua vijana wengi katika nafasi za uongozi wa juu serikalini. HITIMISHO: CCM NI CHAMA CHA LEO NA KESHO, HASA CHA VIJANA CCM ni chama makini, chenye misingi imara na maono ya mbali. Ni chama pekee kinachotambua kuwa taifa linalojenga vijana leo lina uhakika wa kupata viongozi bora kesho. Ni wakati wa vijana kujitokeza kwa wingi, kuchukua fomu, kush...

MSAMA AREJESHA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA UKONGA

Image
MSAMA AREJESHA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA UKONGA Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama leo July 01, 2025 amefika katika Ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam na kurejesha Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga baada ya kuijaza kikamilifu. Fomu hiyo imepokelewa na Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Ilala, Chief Sylvester Yaredi.